Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Arguments hizi nime zisikia sana ni za kijinga mno, huoni kuwa tuna mashirika mengi ya nje yana routes zake Tz na yanapitia kenya yakirudi au kwenda katika nchi mbalimbali , kitendo cha kuzuia ndege kutoka Tanzania kuingia Kenya means mashirika yote hayo hayata weza kutua Kenya yakitokea Tanzania hivyo effects ni kubwa, hatua ya serikali ni sahihi sana.
Mkuu kwa hiyo ndege za Tanzania ni pamoja na Swiss air inayopitia Nairobi kuja bongo? Sina hakika Kama Kuna ndege inatua kwanza Dar then Nairobi Kisha inarudi kwao
 
Nasikia wameufyata ila kwanini Wakenya ukigusa KQ wanasanda kama wameshikwa kende ...hata Mkwere alipunguzaga tu route wakanyooka vibaya ...

Ndio mjue hilo shirika hata kama linaendeshwa kwa hasara lakini taifa linapata faida kwa milango mingine muhimu zaidi ...
Nilishawahi kuwaambia wakenya hakuna nchi hata moja ktk A.mashariki na Kati inayoweza kupimana ubavu na TANZANIA . TANZANIA ni sawa na china ya Afrika mashariki misingi yake ni Imara sana hata wakisusia Mali za TANZANIA bado wataumia Zaid wao
 
Sasa hivi (PM2:57) waziri wa Afya Kenya(Muthai Kagwe) kama sijakosea kuandika jina lake, yuko anahutubia , miongoni mwa jambo ambalo anazungumzia ni hili suala, kwa machache anadai kuwa wao hawajazui ndege wala mtanzania kuingia Kenya, anakiri kuwa wao hawana uwezo huo wa kuzuia Mtanzania au ndege ya Tanzania kuingia Kenya, aidha anaendelea kwa kusema kuwa Tanzania ni mdau muhimu sana wa maendeleo ya Kenya, amedai kuwa leo asubuhi wameongea na mh Kamwerwe/re waziri husika wa Tanzania na kuomba hili jambo liishe haraka sana kwani wao hawajafunga anga kwa ajili ya Tanzania bali wameruhusu baadhi ya nchi na kesho jumapili wataendelea kutoa orodha ya nchi nyingine ambazo zitaruhusiwa kuingia Kenya. Pia mdahalo unaendelea baadhi ya wajumbe wanasisitiza ni lini ili suala litaisha maana ni kosa kubwa sana kuizuia Tanzania, majibu ni yaleyale kuwa wao wameomba Tanzania kwa dhati kabisa hili jambo liishe haraka sana maana wao hawakulenga kama serikali ya Tanzania ilivyolipokea. Pia amewaeleza wakenya kuwa ifikapo kesho wanatumaini watakuwa wamepata majibu mazuri kutoka Tanzania na hili jambo litakuwa limeisha.
Hawana lolote , baada ya kuona wamejibiwa Kwa jibu Kali mno na TANZANIA ndio wakaona bora Kesho tutangaze nchi zingine ili waonekane kumbe TANZANIA walipanga kuitangaza awamu ya pili shida ya kenya anapenda kuiga Sera za marekani wakati ubavu wa kushindana na TANZANIA japo Kwa wiki hana ,mbabe wa Afrika mashariki cku zote atabaki TANZANIA tu na hakuna Afrika mashariki bila ya TANZANIA.
 
Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Macharia amesema anga la Kenya limefunguliwa rasmi leo tayari kupokea Ndege kutoka Nje baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi mitatu kupisha corona huku akisema hawajazuia Ndege za Tanzania kuingia Kenya ila walikuwa wanaweka sawa tu masuala ya Kiitifaki.

“Tumemaliza sintofahamu ambayo imetokea, tunaamini kabla ya siku haijaisha leo Watanzania wataanza kuingia Kenya na wao wataturuhusu kwenda kwao, hatukuwahi kuzuia Ndege zao wala wao hawakuwahi kutuzuia ni matatizo madogo tu yalitokea”-WAZIRI MACHARIA
( via Citizen)
 
Blah blah blah

Vindege vya mozambique ni mavi au nini?

Mizigo ya TZ 90% inapitia Nairobi,deal with it...Ndege za mizigo unazijua?

Na Nairobi kuna facilities ku-process mizigo,sio mozambique uwanja mavi zaidi ya KIA...

Ukisikia Nairobi Airport ni regional hub uelewe hilo,nobody is joking here!

Mtalii akitoka Ulaya,ni lazima apite Nairobi ndio aje TZ,shortest.....

Ukimzungusha J'burg basi huyo mzungu atabaki SA haruki huku mavini maana SA kuna mbuga inazizunguka za TZ mara 20....

We are playing with fire here...

Hawa viazi waje na majibu sahihi na kuhakikisha we win this na sio hizi shortcuts za mavichaa walizochukua
Ndio shippers na importer watabadilisha flights nyingine. Business sio static ni dynamic mzee.
Na ndio maana hata tz wame order ndege ya mizigo kuzia hii dependence.
Kwani sababu ya kuzuia KQ hii mizigo haitofika bongo!?
Kama ni ishu ya Hao watalii watapanda KLM, turkey, Emirates, Swiss na nyingine. Kote KQ ilipokuwa inaenda flight za kuja bongo zipo. So Relax.
Yani wao waanzishe, alafu sisi ndo tuapologise na kuwaita kwenye table, hiyo ni weakness na inferiority. Atakayeona analoose na kuzidiwa atajishusha
 
Mzee

Nani kakwambia tumekuja duniani kumpenda yeyote?

We are not obligated to love anyone,na wao Kenya hawapo obligated to love anyone whatsoever!

Infact,love ndio mwanzo wa upumbavu kama huu sisi Watz tumekua emotional kwa hatua aliyochukua Kenya...

Tunachotaka ni hela za Wakenya na uchumi wetu wa importation ya mizigo na Watalii inapita JKIA kwa zaidi ya 90%!

We dont have to love each other,the love of capitalism solves all these nonsenses you are talking about here!

Is love pay anybody?If no,then fvck it!
Utanyooka tu mwaka huu wewe na vibaraka wenzako unazan hii serikali ya kufanyia majaribio ?. Jamaa zako uliokua unawapigania washatubu huko wamekosea wanaomba yaishe haraka nakesho alfajir wanaitangaza TANZANIA ila Kwa kuzuga ili wasionekane kama wamepigishwa goti wataweka na nchi kadhaa mfano Malawi ili kuficha haibu huku wewe ukibaki unaendelea kuteseka maana ulidai TZ itapata hasara. Unaonekana hata changamoto zako huwezi kukabiliana nazo kama hujui jibu sahihi Kwa wakati sahihi
 
Kiwango chetu cha interactions ni kikubwa na tunategemeana. Hao wengine madhara si makubwa kama tukibaniana wenyewe.
Tanzania imekurupuka ila kwa Magufuli hilo ni jambo la kawaida. Kiongozi asiye na uvumilivu wala staha kwa 100%. Kumbe Tanzania imeanza chokochoko muda hadi malori ya mbao yalishagataifishwa na Magufuli!
 
Bro, Ethiopia na the rest ot EA combined bado JKIA anatuacha mbali

Unafananisha Nairobi na uchafu wa Addis aisee? Kua serious wewe
Kwahiyo tuwe subjected kwa kenya sababu JKIA ni flight hub EA au!? Nonsense
Nampongeza JPM kwa sababu analinda pride ya nchi kutokana na GoK. Kwani unahisi Kenya hii haita waumiza.
Let's wait and see badala ya kulalamika tu na kukosoa.
Mbona china na US wanapigana trade ban kila siku
 
Nilishawahi kuwaambia wakenya hakuna nchi hata moja ktk A.mashariki na Kati inayoweza kupimana ubavu na TANZANIA . TANZANIA ni sawa na china ya Afrika mashariki misingi yake ni Imara sana hata wakisusia Mali za TANZANIA bado wataumia Zaid wao
Siyo A. Mashariki tu, Afrika nchi nyingi zikifika kwa Tanzania zinanywea, hili halijaanza leo bali lina miaka kedekede, chanzo cha hadhi hii ni Mungu tu kutuepushia mambo mbalimbali mabaya na kutupa mema ikiwemo mshikamano (achana na siasa za CCM na CDM ambazo zinalenga kutugawa), mazingira mazuri ya kilimo na ufugaji, upendo wa asili wa kibinadamu, kuukataa Udini na Ukabila na Ukanda km wenzetu(Rwanda, Burundi, Kenya, Nigeria, Somalia nk) mbali hayo hatuna baa la njaa au sehemu kuna njaa ya kutisha kama ilivyo huko kwa wengine(rejea Kaunti ya Turkana huko Kenya njaa kali, Sudan Kusin, Ethiopia) hatuna majanga kama Nzige ( rejea Uganda, Kenya, Sudan na Ethiopia) huko Kenya kaunti ya Kware sasa wamevamiwa na Kunguni raia wanahama makazi maana hali ni ngumu Kunguni wamewanyonya watu hadi kiasi cha kutisha, Alshababu wanawawinda Wakenya huko Garrisa ( watu hawalali ndani) Ukirejea Afrika ya Kati huko mabomu na gurunedi na risasi vinaulizana nani atangulie kumwaga damu ya Waafrika wenzetu. Ukirudi upande wa kusini mwa Afrika utayakuta mataifa km Zimbabwe hali ni mbaya sana pia. Yaani ya kuandika ni mengi sana, Waafrika wote tunapitia changamoto nyingi lakini Tanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu maana tuna unafuu sana wa maisha. Ingekuwa si wizi wa wanasiasa na ubinafsi wao naamini tungekuwa tunaongoza kwa kila kitu hapa Afrika.
 
Mkuu Kenya wametangaza first round nchi 11,je dunia hii Ina nchi ngapi?Je hizo nchi zingine zimereact Kama sisi? Kwa nini sisi tujione tumefungiwa?Huoni kuwa tumeonesha utoto na kutojiamini?Tumeshindwaje kuvuta subra kidogo tuone mwisho wake? Kwangu Mimi logic was simple kwamba Kama hawataki ndege zetu ziende Kenya kwa sababu zitapeleka wtz kwa kuwa Wana corona,je KQ ingekuja bongo kupakia akina nani? I think mihemuko tumeiweka mbele than anything ease
Kama hujui TANZANIA ndio nchi ya kuleta mlingano wa nguvu Kwa nchi yeyote hapa Afrika mashariki , kwahiyo utakaposema mbona wengine hawajafanya hivi huko kupungukiwa Kwa akili ,Yani umedhurumika kiuchumi unasubiri Burundi au kongo alalamike nawe ndo ulalamike du!! Ninyi ndio wale darasani mulikuwa munasema afadhali Mimi nimepata wastani wa 20 kuliko juma kapata 15 unashindwa kukumbuka kila mmoja aliletwa na mzazi wake tena Kwa wakati tofauti.unapaswa uangalie maslahi yako bila ya kuangalia je Malawi nae amedhurika au hapana ukiona Malawi au Burundi kadhurika useme bc kumbe sipo pekeyangu huko ni kukomaa kuanzia shingoni kuja chini .
 
Arguments hizi nime zisikia sana ni za kijinga mno, huoni kuwa tuna mashirika mengi ya nje yana routes zake Tz na yanapitia kenya yakirudi au kwenda katika nchi mbalimbali , kitendo cha kuzuia ndege kutoka Tanzania kuingia Kenya means mashirika yote hayo hayata weza kutua Kenya yakitokea Tanzania hivyo effects ni kubwa, hatua ya serikali ni sahihi sana.
Hatua ya mihemko tu! KQ ni mojawapo was ndege ambazo hazitoruhusiwa kuingia Kenya as long as zimetoka Tanzania... logic imekuingia?
 
Ndio shippers na importer watabadilisha flights nyingine. Business sio static ni dynamic mzee.
Na ndio maana hata tz wame order ndege ya mizigo kuzia hii dependence.
Kwani sababu ya kuzuia KQ hii mizigo haitofika bongo!?
Kama ni ishu ya Hao watalii watapanda KLM, turkey, Emirates, Swiss na nyingine. Kote KQ ilipokuwa inaenda flight za kuja bongo zipo. So Relax.
Yani wao waanzishe, alafu sisi ndo tuapologise na kuwaita kwenye table, hiyo ni weakness na inferiority. Atakayeona analoose na kuzidiwa atajishusha
WA-TZ uthubutu ni tatizo letu kubwa kupita maelezo
 
Kwahiyo tuwe subjected kwa kenya sababu JKIA ni flight hub EA au!? Nonsense
Nampo geza JPM kwa sababu analinda pride ya nchi kutokana na GoK. Kwani unahisi Kenya hii haita waumiza.
Let's wait and see badala ya kulalamika tu na kukosoa.
Mbona china na US wanapigana trade ban kila siku
Mzee,you dont have to like anybody !

We have to love the money,by any means neccesary!

We have to be subjected to money only and nothing else!

Emotions na blah blah zingine peleka Chato huko na ma-emotions yenu ya kike!

JKIA ni hub yetu ya hela,by any means neccesary we have to protect our interests!

We are still sleeping,we will never learn!

Ruka ruka ,piga garagaza,rusha tako hapa na kule,bado jawabu la Korona Tanzania hatuna!

Dunia inatuuliza na evidence hatuna,kaanza Kenya ku-ban,watafata wengine wote....ndio utaelewa dunia haiendeshwi kwa akili mufilisi za Chattle!
 
Kama hujui TANZANIA ndio nchi ya kuleta mlingano wa nguvu Kwa nchi yeyote hapa Afrika mashariki , kwahiyo utakaposema mbona wengine hawajafanya hivi huko kupungukiwa Kwa akili ,Yani umedhurumika kiuchumi unasubiri Burundi au kongo alalamike nawe ndo ulalamike du!! Ninyi ndio wale darasani mulikuwa munasema afadhali Mimi nimepata wastani wa 20 kuliko juma kapata 15 unashindwa kukumbuka kila mmoja aliletwa na mzazi wake tena Kwa wakati tofauti.unapaswa uangalie maslahi yako bila ya kuangalia je Malawi nae amedhurika au hapana ukiona Malawi au Burundi kadhurika useme bc kumbe sipo pekeyangu huko ni kukomaa kuanzia shingoni kuja chini .
Mkuu hivi ndege gani ya Tanzania ambayo imekuwa ikitua viwanja vya Kenya hapo kabla hadi tuone leo tumedhulumika kiuchumi
 
Mzee,you dont have to like anybody !

We have to love the money,by any means neccesary!

We have to be subjected to money only and nothing else!

Emotions na blah blah zingine peleka Chato huko na ma-emotions yenu ya kike!

JKIA ni hub yetu ya hela,by any means neccesary we have to protect our interests!

We are still sleeping,we will never learn!

Ruka ruka ,piga garagaza,rusha tako hapa na kule,bado jawabu la Korona Tanzania hatuna!

Dunia inatuuliza na evidence hatuna,kaanza Kenya ku-ban,watafata wengine wote....ndio utaelewa dunia haiendeshwi kwa akili mufilisi za Chattle!
So what!? let see kama kama hatutapata hizo hela, kwahiyo tuwe watumwa sababu ya hela!?
We unahisi uamuzi wetu na wao hautawapa loss? Tunachotaka no win win trade deals na sio nonsense. Wao wametumia corona kujustify, sisi tumeenda direct
Route zipo nyingi tu sio lazima JKIA, ndio maana nikasema trade ni dynamic sio static mzee.
 
Yes it makes losses but revenue have been growing or you do not know the difference between revenues and profit?

Wewe ndo useme, ulipoongea route ya pesa mingi ulimaanisha nini wakati kila siku KQ wanatangaza losses.? Yes mapato yameongezeka, lakini matumizi pia yameongezeka sijui kama umeliona hilo.?
 
Mkuu hivi ndege gani ya Tanzania ambayo imekuwa ikitua viwanja vya Kenya hapo kabla hadi tuone leo tumedhulumika kiuchumi
Kwani tukisema ndege za TANZANIA unajua Atcl tu ? C kuna precision air .kudhurumika kupo kama unafatilia mambo ya kiuchumi utaona athari zake .athari zake wakenya watakuja Tz lakini wa Tz hawatoenda kwahiyo hata kama kulikuwa na waTZ wameajiliwa Kenya hawatoenda ila wakenya watafanya kazi bongo nyengine watalii wataweza kwenda Kenya kisha kuja TANZANIA ila waliokua Tz hawatoweza kwenda Kenya kwahiyo itapelekea watalii wengi wakitaka kuja TANZANIA kisha wamalizie Kenya wataghairi zipo nyingi kwenye hiyo hila
 
Back
Top Bottom