Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
1,533
2,000
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefuta kibali cha ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua katika viwanja vya ndege vya Zanzibar, Dar es Salaam na Kilimanjaro kuanzia tarehe 1 Agosti 2020. Maamuzi haya yametolewa kama majibu (reciprocal basis) kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa na serikali ya Kenya ya kuzuia ndege kutoka shirika la ATCL (Air Tanzania Company Limited) kuingia nchini Kenya kwa madai ya kuanza kuruhusu nchi zenye maambukizi madogo ya corona.

Maelezo zaidi yametolewa kwenye barua hii iliyoambatanishwa.

EeRnSVRX0AAdnzD.jpeg
 

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
12,593
2,000
Pagumu sana hapa! MKAPA ndio alikuwa anaweza kumshauri Magufuli sasa hayupo Yaani diplomasia ya Kenya na Tz ipo pabaya sana.

Ego itaua uhusiano wa hizi nchi mbilii japo wanajidai marafiki kinafiki lakini tushafikaa mbalii aiseee sasa hivi raia wa Tanzania wataanza kutimuliwa Kenya

MKAPA majirani wote hawajaja kumzika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom