Serikali ya Tanzania yazindua mradi wa akili bandia

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271

Dodoma. Serikali ya Tanzania imezindua mradi wa maabara ya akili bandia (artificial intelligence) utakaosaidia kurahisisha shughuli za maendeleo nchini.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah akizindua mradi huo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

“Kama hivi wengi tunavyoangalia dunia za sasa hivi wenzetu wameshakwenda mbele zaidi. Sometimes (wakati fulani) unakuta watu wanavyokwenda makazini wanajibiwa na robot, unapopanda lifti, mwendo kazi,” amesema.

Naibu Waziri huyo amesema teknolojia hiyo inatumika hata mashambani ambapo badala ya kwenda mtu linatumika robot na maofisini.

Amesema kwa nchini ni maabara ya pili kuanzishwa ambapo hivi sasa wapo katika utafiti wa kuangalia ni jinsi gani teknolojia hiyo mpya inavyoweza kutumika.

Abdullah amesema ni vyuo viwili ambavyo vimeingia katika mradi huo ambavyo ni Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha jijini Arusha na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Profesa Emmanuel Luoga amesema mradi huo mkubwa wa kisayansi utakaosaidia maendeleo.

“Tunajua katika nchi yetu tunaelekea katika uchumi wa kidigitali, mapinduzi ya nne ya viwanda haya yote hayawezi kutekelezeka bila matumizi ya Tehama. Akili Bandia ni moja ya akili ya juu katika kuleta mapinduzi katika viwanda,”amesema.

Kiongozi wa mradi huo katika chuo cha Udom, Dk Ally Nyamawe amesema mradi huo una nguzo tatu ambazo ni kufanya tafiti, mafunzo na ubunifu.

“Mradi unatarajia kutoa mafunzo kwa wanafunzi wawili wa PHD (shahada ya udaktari) na wawili wa masters (shahada ya uzamivu),” amesema.
 
Waanze kuwaweka barabaranu kama trafiki.
Itapunguza urefu wa kwamba wallahi!

1643098091793.png
 
Wakat serkali inashadadia mlengo huu iwazie pia hali ya ajira itakuwaje kama tu kwa hali ya kawaida iko hivi. Bas mwelekeo huu uende sambamba na kuoanua sekta binafs kumeza wasomi kukabiliana na tatzo la ajira. La sivyo havitatekelezeka kwa amani.
 
Back
Top Bottom