Serikali ya Tanzania yatoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa barakoa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Serikali ya Tanzania imesema mtu anaweza kuvaa barakoa ili kujikinga na magonjwa yanayosambaa kwa njia ya hewa ikiwemo kifua kikuu.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Februari 5, 2021 na katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Mabula Mchembe alipotembelea hospitali za rufaa za Bugando na Sekou-Toure na kubainisha kuwa hospitali hizo hazina wagonjwa wa Covid-19.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Profesa Mchembe amewataka wananchi kuondoa hofu ya uwepo wa wagonjwa katika hospitali hizo.

Akijibu swali kuhusu uvaaji wa barakoa, Katibu mkuu huyo amesema mtu yeyote anayehisi yuko kwenye eneo hatarishi kwa maambukizi ya magonjwa yanayosambaa kwa njia ya hewa ikiwemo kifua kikuu avae barakoa.

“Uvaaji wa barakoa siyo kwa ajili ya kuzuia virusi vya corona kama wengi wanavyofikiria, bali ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya maradhi yanayoambukiza kwa njia ya hewa,” amesema.

Akitoa taarifa kwa katibu mkuu huyo kwa nyakati tofauti, Kaimu mkurugenzi wa Bugando, Dk Fabian Massaga amesema hospitali hiyo haina mgonjwa yeyote wa Covid 19 kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema hospitali hiyo inapokea wagonjwa wenye changamoto ya kupumua inayotokana na maradhi mengine ikiwemo shinikizo la damu, uzito uliopitiliza na kifua kikuu.

Maelezo kama hayo pia yametolewa na mganga mfawidhi wa hospitali ya Sekou-Toure, Dk Bahati Msaki aliyesema hakuna mgonjwa wa corona hospitalini hapo.

“Tunao wagonjwa watano wenye changamoto ya kupumua inayotokana na maradhi mengine,” amesema Dk Bahati.

Pamoja na kukagua utoaji wa huduma, ziara ya Profesa Mchembe Hospitali za Bugando na Sekou-Toure ililenga kupata ukweli iwapo hospitali hizo zina mgonjwa wa Covid 19.
 
Asante analogia. Umeleta hii habari. Nimeisona kule opera news. Huyu wa Jalalani anasema kuwa kuna changamoto za njia ya hewa kwa watu wanene ie over weight , kifua kikuu , wenye high blood pressure etc.

Anasahau kuwa those are the predisposing condition for corona virus attack! St,,-=./'pid tangu dunia iumbwe hatujawahi vaa barakoa kwa sababu ya kujikinga na kifua kikuu, yeye anasema tuvae kwa ajili ya TB!

COVID-19 is a new disease. Currently there are limited data and information about the impact of many underlying medical conditions on the risk for severe illness from COVID-19. Based on what we know at this time, adults of any age with the following conditions might be at an increased risk for severe illness from the virus that causes COVID-19:

 
JIONGEZE...
Ila kiukweli watanzania mungu anatulinda Sana Sanaa.kwa life style yetu hii.
 
Mungu tuu atusimamie katika hili watu hawajali kabisa aisee mpaka inasikitisha sijui wanaamini katika nini...
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom