Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema mpaka sasa hakuna Mtanzania aliyeuawa katika machafuko yaliyotokea nchini Afrika Kusini.
Profesa Kabudi ameyasema hayo leo Jumatano, Septemba 4, 2019 katika hafla maalum ya kuwaaga vijana 100 wanaokwenda nchini Israel kwa ajili ya mafunzo ya kilimo kwa vitendo.
Amesema Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Damas Ndumbaro amekuwa nchini humo kwa ajili ya kufuatilia mambo kadhaa na mpaka sasa hakuna taarifa ya kifo wala madhara kwa Mtanzania yeyote.
"Serikali ya Tanzania inaunga mkono tamko la Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa linalolaani mauaji ya Waafrika yanayoendelea hivi sasa. Taarifa zilizopo mpaka sasa hakuna Mtanzania aliyepata madhara," amesema Kabudi.
Aidha Kabudi amewataka Watanzania kutolipiza kisasi kwa wageni waishio hapa nchini.
"Tutawalinda, wapo salama wao na mali zao zitakuwa salama. Mahusiano kati ya nchi hizi mbili yataendelea," amesema Kabudi.
Pamoja na hayo, Wabunge wa Tanzania wametaka Bunge liahirishe shughuli zilizopangwa kwa siku ya leo Jumatano Septemba 4, 2019 ili wajadili vurugu zilizojitokeza nchini Afrika Kusini zinazowahusisha Waafrika.
Wabunge hao waliozungumzia suala hilo bungeni ni Elibariki Kingu (Singida Magharibi- CCM), Oscar Mukasa (Biharamuro Magharibi- CCM), John Heche (Tarime Vijijini-Chadema) na Godluck Mlinga (Ulanga Mashariki-CCM).
Aliyeanza alikuwa ni Mlinga wakati wa maswali na majibu ambaye aliwataka Waafrika Kusini kukumbuka kuwa isingekuwa Waafrika kuwa pamoja wangekuwa bado wanaimba mapambio ya makaburu.
Hata hivyo, baada ya maswali na majibu Kingu aliomba mwongozo wa Spika na kusema ametumiwa taarifa na Mtanzania aliyeko Afrika Kusini kuwa maduka yake yamechomwa.