#COVID19 Serikali ya Tanzania yatoa Katazo la Misongamano isiyokuwa ya lazima kukabiliana na UVIKO

mikusanyiko isiyo ya lazima, elewa hiyo lugha chief....
Kwahiyo watu kujazana kwenye madaladala hadi tunashindwa kupata hewa safi nako ni mkusanyiko wa lazima?

Ndo maana watu wanasema lengo la serikali ni kuzuia makongamano ya kudai katiba mpya sio kuzuia maambukizi maana kama serikali ingekuwa serious na maisha ya Watanzania basi ingezuia rasmi mikusanyiko yoyote au kuweka masharti makali kwenye mikusanyiko.
 
Kwanini haitoi takwimu za wanaougua na kufariki kwa malaria? Na kwanini haikatazi watu kutoka nje usiku kwenye mbu?!

- [Fahamu kwa undani nadharia ya ‘Lockdown YOYO effect’ , mchezo wa kujaza maji ndoo ilitoboka

Pumzika kwa amani JPM😫😫😫

Uchuro mtupu watuache tukashangilie kivyetuvyetu. WHO wanazingua toka kitambo sisi tunaingia uwanjani na tunatoka fresh tu. Akuna mtu aliyefariki. Wasitutishe kwani delta ndo nani, Tanzania tuondokane na kuburuzwa ondoeni hofu. Wanatangaza delta kama kiama vile akati poa tu
Tunalazimishwa kucheza mdundo ambao hata hatuusikii asee...
 
Naomba nimwulize mheshimiwa Dorothy Gwajima: Hivi barakoa kama inamkinga mtu na virusi vya corona kwa nini isimkinge na ukimwi au gonoria au kaswende!! Maana yangu ni kwamba kama mtu akijishonea kondomu kwa kutumia vitambaa wanavyotumia kutengeneza barakoa, halafu akaiwekea elastic kwenye mdomo ili mtu akivaa ibane vizuri, je itazuia virusi vya ukimwi au itazuia bacteria waletao gonoria kwenye tendo la ngono! Msinicheke, nina maana yangu! Maana yangu ni kwamba tunavalishwa barakoa isiyokuwa na ulinzi wowote dhidi ya virusi!! Vaa kondomu ya material ya barakoa halafu uende kwa changudoa mwenye gonoria uone kama kesho yake kama hautatoa usaha mbeleni!! Virusi vya corona ni vidogo zaidi ya bacteria wa gonoria! Kama bacteria wanaweza kupenya kwenye kitambaa cha barakoa, virusi vya corona vitapenya kwa urahisi zaidi. Huu ni ukweli lakini watu wa adanganywa wajikinge kwa barakoa wakati barakoa haiwezi kumkinga mvaaji wake!! Ndiyo maana watumishi wa afya wameambukizwa sana corona duniani kote wakati ni waaminifu kuvaa barakoa!! Barakoa ni biashara, siyo kinga mathubuti!! Vinginevyo watengeneze pia kondomu kwa material ya barakoa!! Mh Gwajima karibu ujibu!
 
View attachment 1863511
View attachment 1863512

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

TAMKO LA KATAZO LA MISONGAMANO ISIYOKUWA YA LAZIMA

Tarehe 22 Julai, 2021 - Dar es Salaam.

Ndugu Wananchi, kama tunavyofahamu Tanzania iko kwenye mapambano ya kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 ikiwa ni wimbi la 3 la mlipuko huu tangu uingie nchini Machi, 2020. Itakumbukwa kuwa Wizara ya Afya na Viongozi wa Serikali kwa ujumla wake kwenye ngazi mbalimbali wamekuwa wakitoa taarifa, elimu na kuhamasisha juu ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya UVIKO-19.

Ndugu Wananchi, Serikali inatambua kuwa wananchi walio wengi wamekuwa wasikivu, wakiitikia na kutekeleza miongozo yote ya kujikinga na kuwakinga wengine ingawa kwenye baadhi ya maeneo mwitikio umekuwa siyo wa kuridhisha. Hali hii imeendelea kuchangia kuongezeka kwa maambukizi na hatimaye kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa waliolazwa ambapo kufikia tarehe 21/07/2021 katika vituo vya huduma za afya kote nchini kulikuwa na wagonjwa 682 waliokuwa wanaugua maradhi ya UVIKO-19. Aidha, watalaamu wa afya wameendelea kupambana kwa moyo mmoja kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wakati lakini hata hivyo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakipoteza maisha.

Ndugu Wananchi, Wizara itaendelea kutoa takwimu hizi ili kwa pamoja tuendelee kufuatilia hali halisi ya mwenendo wa ugonjwa huu huku tukiendelea kuchukua hatua za kutosha. Aidha, ili kuimarisha zaidi kasi ya kupambana na kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19
natamka kuwa, kuanzia leo tarehe 22/07/2021 nimekataza shughuli zote za misongamano yote isiyo ya lazima na ile yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na kitaifa. Naelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwapa ushirikiano Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya Mwaka 2009 na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya shughuli zenye ulazima.

Ndugu Wananchi, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wake wote itaendelea kutoa elimu na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo yote ya afya. Aidha, natoa wito kwa wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya Chanjo kama ambavyo Mheshimiwa Waziri Mkuu alivyotoa taarifa jana tarehe 21/07/2021. Leo hii wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo tayari kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma ya Chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa hiari na bila malipo. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Ndugu Wananchi, Wito wangu tuendelee kushikamana kwenye mapambano ya kutokomeza kabisa adui UVIKO-19 kwa kuzingatia utekelezaji wa afua zote za kujikinga na kuwakinga wengine zikiwemo;

  1. Kuhakikisha sehemu zote zinazotoa huduma za kijamii zinakuwa na miundombinu ya huduma ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kama maji hakuna kuwe na matumizi ya vitakasa mikono.
  2. Wananchi wote wanaotoa huduma za kijamii na wanaofika kupata huduma za kijamii wahakikishe wamezingatia afua za kinga zikiwemo kuvaa barakoa safi na salama.
  3. Kwenye maeneo ya huduma za kijamii zinazokutanisha watu kadhaa kupata huduma kanuni ya kuepuka misongamano izingatiwe kwa kuchukua tahadhari zote.
  4. Kwenye vyombo vya usafiri utaratibu wa kuepuka kubeba abiria kwa kusongamana uzingatiwe na kabla abiria hao hawajaingia kwenye chombo husika kuwe na utaratibu wa kuhakikisha wamezingatia tahadhari zote za kujikinga na kuwakinga wengine.
  5. Vilevile, nawakumbusha Wananchi tuendelee kuzingatia lishe bora, kufanya mazoezi na kutumia tiba asili zilizosajiliwa na baraza la tiba asili pasipo kuchelewa kufika kwenye vituo vya huduma kwa ushauri wa kitaalamu.
Aidha, natoa wito kwa viongozi wa serikali na wa sekta binafsi na taasisi zake zote kuonesha mfano kwa wananchi jinsi ambavyo wao wanatekeleza maagizo ya kuchukua tahadhari za kinga dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19. Vilevile, natoa wito wananchi kujiepusha na taarifa zozote kuhusu UVIKO-19 kupitia watoa taarifa wasio rasmi.
Mh waziri, umewahi kutembelea shule za bweni za serikali na kujionea watoto wanalala wawili kila kitanda, na double decker zikitenganishwa umbali wa futi 2? Unaiona (ukichungulia dirishani tokea V8 lako) mibanano ya abiria kwenye magari ya usafiri wa umma dar? Mikoani umeongelea lolote kuhusu minada na magulio? Vipi umati wa watu kwenye barabara za mijini zilizo fungwa kuruhusu wamachinga? Tangazo lako ni shinikizo kuhalarisha kukamatwa kwa Mbowe. Serikali haina uchungu na raia wake na ndio maana wizara yako inajivua kuwajibika kwa madhara ya chanjo za Corona.
 
1. Je tuendelee kutumia chachandu kama Dawa? Kama vile ambavyo ulituaminisha kuwa ni Dawa ya Corona na kusababisha watu watengeneze Chachandu na kutuuzia kwa bei ya Juu.

2. Tuendelee kujifukiza na kuharibu mapafu kwa ule mvuke kwa mchanganyiko usioeleweka?

Au sasa tunafanyaje? Maana hili jina la Gwajima sijajua lina maana gani ila nahisi lina usanii sanii flani hivi.

View attachment 1863528

View attachment 1863529
Kwa hivyo vibali vitakuwa na kinga ya virus? Kwa nini pasiwe na standard guidelines? Eg misiba watazika ndugu wasiozidi kadhaa, harusi ukumbi uzidi waalikwa kadhaa, mikutano ya kisiasa ya nje stop, ya ndani umbali uwe kadhaa, nk nk. Mnaingiza siasa kwenye utaalamu, matokeo mnadharaulika.
 
View attachment 1863511
View attachment 1863512

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

TAMKO LA KATAZO LA MISONGAMANO ISIYOKUWA YA LAZIMA

Tarehe 22 Julai, 2021 - Dar es Salaam.

Ndugu Wananchi, kama tunavyofahamu Tanzania iko kwenye mapambano ya kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 ikiwa ni wimbi la 3 la mlipuko huu tangu uingie nchini Machi, 2020. Itakumbukwa kuwa Wizara ya Afya na Viongozi wa Serikali kwa ujumla wake kwenye ngazi mbalimbali wamekuwa wakitoa taarifa, elimu na kuhamasisha juu ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya UVIKO-19.

Ndugu Wananchi, Serikali inatambua kuwa wananchi walio wengi wamekuwa wasikivu, wakiitikia na kutekeleza miongozo yote ya kujikinga na kuwakinga wengine ingawa kwenye baadhi ya maeneo mwitikio umekuwa siyo wa kuridhisha. Hali hii imeendelea kuchangia kuongezeka kwa maambukizi na hatimaye kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa waliolazwa ambapo kufikia tarehe 21/07/2021 katika vituo vya huduma za afya kote nchini kulikuwa na wagonjwa 682 waliokuwa wanaugua maradhi ya UVIKO-19. Aidha, watalaamu wa afya wameendelea kupambana kwa moyo mmoja kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wakati lakini hata hivyo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakipoteza maisha.

Ndugu Wananchi, Wizara itaendelea kutoa takwimu hizi ili kwa pamoja tuendelee kufuatilia hali halisi ya mwenendo wa ugonjwa huu huku tukiendelea kuchukua hatua za kutosha. Aidha, ili kuimarisha zaidi kasi ya kupambana na kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19
natamka kuwa, kuanzia leo tarehe 22/07/2021 nimekataza shughuli zote za misongamano yote isiyo ya lazima na ile yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na kitaifa. Naelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwapa ushirikiano Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya Mwaka 2009 na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya shughuli zenye ulazima.

Ndugu Wananchi, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wake wote itaendelea kutoa elimu na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo yote ya afya. Aidha, natoa wito kwa wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya Chanjo kama ambavyo Mheshimiwa Waziri Mkuu alivyotoa taarifa jana tarehe 21/07/2021. Leo hii wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo tayari kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma ya Chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa hiari na bila malipo. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Ndugu Wananchi, Wito wangu tuendelee kushikamana kwenye mapambano ya kutokomeza kabisa adui UVIKO-19 kwa kuzingatia utekelezaji wa afua zote za kujikinga na kuwakinga wengine zikiwemo;

  1. Kuhakikisha sehemu zote zinazotoa huduma za kijamii zinakuwa na miundombinu ya huduma ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kama maji hakuna kuwe na matumizi ya vitakasa mikono.
  2. Wananchi wote wanaotoa huduma za kijamii na wanaofika kupata huduma za kijamii wahakikishe wamezingatia afua za kinga zikiwemo kuvaa barakoa safi na salama.
  3. Kwenye maeneo ya huduma za kijamii zinazokutanisha watu kadhaa kupata huduma kanuni ya kuepuka misongamano izingatiwe kwa kuchukua tahadhari zote.
  4. Kwenye vyombo vya usafiri utaratibu wa kuepuka kubeba abiria kwa kusongamana uzingatiwe na kabla abiria hao hawajaingia kwenye chombo husika kuwe na utaratibu wa kuhakikisha wamezingatia tahadhari zote za kujikinga na kuwakinga wengine.
  5. Vilevile, nawakumbusha Wananchi tuendelee kuzingatia lishe bora, kufanya mazoezi na kutumia tiba asili zilizosajiliwa na baraza la tiba asili pasipo kuchelewa kufika kwenye vituo vya huduma kwa ushauri wa kitaalamu.
Aidha, natoa wito kwa viongozi wa serikali na wa sekta binafsi na taasisi zake zote kuonesha mfano kwa wananchi jinsi ambavyo wao wanatekeleza maagizo ya kuchukua tahadhari za kinga dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19. Vilevile, natoa wito wananchi kujiepusha na taarifa zozote kuhusu UVIKO-19 kupitia watoa taarifa wasio rasmi.
Katazo hili ni la hila na lina lengo la kukomoa kikundi cha wanaotaka katiba mpya. Vipi mikusanyiko ya michezo, ibada, sherehe, ziara za rais na viongozi wa serikali na CCM? Je kuna mikusanyiko isiyo ya lazima?
 
Imetoa behewa za kupereka mashabiki wa mpira kwenda kusamba UVIKO19 Mkoani Kigoma
 
Back
Top Bottom