Serikali ya Tanzania yatamba ukuaji wa uchumi na pato la Taifa

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,884
22,601
Serikali ya Tanzania imesema uchumi wa taifa umekuwa kwa asilimia 7.0 katika mwaka 2018 na kufanya iwe nchi ya kwanza kwa ukuaji wa uchumi kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolea leo Jumanne Desemba 31, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk Philip Mpango wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2019 na tathimini ya awali ya utekelezaji wa bajeti kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20.

Waziri Mpango amesema katika kipindi cha Januari - Juni 2019, pato la taifa lilikuwa kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na asilimia 6.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Amesema Tanzania ilikua nchi ya tano katika ukuaji wa uchumi Sadc ikitanguliwa na Eritria ambayo uchumi wake ulikuwa kwa asilimia 12.2, Rwanda (8.6), Ethiopia (7.7) na nchi ya Ivory Coast iliyofikisha asilimia 7.4.

Amesema ukuaji huo ulichochewa na kuongezeka kwa uwekezaji hasa katika miundombinu ya barabara, reli, na viwanja vya ndege, kutegemea kwa upatikanaji wa nishati ya umeme, kuimarika kwa huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa madini.

“Kingine ni kuongezeka kwa mazao ya kilimo kutokana na hali nzuri ya hewa lakini sekta zilizokuwa kwa kasi katika kipindi cha kwanza cha 2019 ni ujenzi ambayo imefikia asilimia 16.5, uchimbaji wa madini yenye asilimia 13.7, habari na mawasiliano 10.7, maji asilimia 9.1 pamoja na sekta ya usafirishaji na uhifadhi mizigo iliyofikisha asilimia 9.0,” amesema Mpango.

Kwa mujibu wa Waziri, ukuaji wa uchumi katika mwaka husika unaonekana kupitia upatikanaji wa huduma bora zaidi kwa wananchi zilizotolewa na serikali yao ikilinganishwa na ilivyokuwa katika mwaka uliotangulia.
 
Yaani kama ni shamba la ngano limemea mazao(pato la taifa) kuna gugu moja pia linaitwa Deni la taifa more than 50. Trillion vyote vimekua pamoja.

Mpaka aje bwana wa mavuno aling'oe gugu hilo.
 
Yaani kama ni shamba la ngano limemea mazao(pato la taifa) kuna gugu moja pia linaitwa Deni la taifa more than 50. Trillion vyote vimekua pamoja.

Mpaka aje bwana wa mavuno aling'oe gugu hilo.
Deni linabebeka na lina lipika

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda uchumi wa chato sio wa watanzania
Haya maneno ungeyasema mbele ya watazania live wangeondoka na kichwa chako

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani unadhani ulivyo mvivu wa kutafuta hela na ulikuwa unategemea ile ya tuma kwenye namba hii itasoma jina la Kassim, au unatapeli kwa kuiba taarifa za shule na kuanza kuwatapeli Wazazi wa Wanafunzi, au ulizoea kufanya ujambazi au ulizoea kuwatapeli Wanyonge. That time no longer atis Everything thing changes.
Saizi tapeli uone kitakachotokea kwenye Serikali ya JPM.
Fanya kazi acha kuishi kwa ujanjajanja utaiachia laaaana Familia yako.
 
Still sijaona mahali ambapo IMF imeomba msamaha. hizo habari hazija kuwa published bado.

Kila ulichoandiaka ni statistics za SADC... not IMF. Sipingi uchumi wa nchi kupanda.. ni jambo zuri sana.. ipa hapounaposema IMF imeomba msamaha ndio napashangaa.
 
Kwani unadhani ulivyo mvivu wa kutafuta hela na ulikuwa unategemea ile ya tuma kwenye namba hii itasoma jina la Kassim, au unatapeli kwa kuiba taarifa za shule na kuanza kuwatapeli Wazazi wa Wanafunzi, au ulizoea kufanya ujambazi au ulizoea kuwatapeli Wanyonge. That time no longer atis Everything thing changes.
Saizi tapeli uone kitakachotokea kwenye Serikali ya JPM.
Fanya kazi acha kuishi kwa ujanjajanja utaiachia laaaana Familia yako.
Hawa ukawa wanamatatizo sana

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom