#COVID19 Serikali ya Tanzania yashirikiana na Kampuni ya China kujenga maabara ya kupima virusi vya Corona

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1645496209618.png

Februari 18, balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki alienda kwenye maabara mpya iliyojengwa na serikali ya Tanzania ili kupima virusi vya Corona huko Dar es Salaam. Hivi sasa maabara hii inafanya majaribio ya PCR na kingamwili.

Serikali ya Tanzania imeiajiri Kampuni ya BGI ya China ambayo inaongoza duniani katika ujenzi na usimamizi wa maabara kutekeleza mradi huo, kutokana na pendekezo la Ubalozi wa China nchini Tanzania.

Inaaminika kuwa Shirika la Ndegela Tanzania litapata fursa ya kurejesha safari za ndege za abiria kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou, China, wakati maabara hiyo mpya itakapoanza kufanya kazi kutokana na upimaji wenye uhakika zaidi wa virusi vya Corona.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania Bw. Ladislaus Matindi vilevile ameonesha matarajio hayo wakati balozi alipofanya ukaguzi.
 
Hiyo maabara mpya imejengwa wapi?
 
Nchini Zanzibar wao waliingia mkataba na shirika la ndege fly Dubai wakaletewa more advanced ukishuka na kupita au kwenda kupanda ndege inakupima na majibu ni papo kwa hapo.

Na inasemekana ndiyo mashine ya kwanza barani Africa.
 
Nchini zanzibar wao waliingia mkataba na shirika la ndege fly Dubai wakaletewa more advanced ukishuka na kupita au kwenda kupanda ndege inakupima na majibu ni papo kwa hapo.

Na inasemekana ndiyo mashine ya kwanza barani Africa.
Sasa kama kuna technology ya kupima corona kwa kutumia simu za mkononi na majibu sahihi yakapatina Papo kwa papo , kuna faida gani kwa nchi kwenda kuongeza madeni China ya kujenga kiwanda eti cha kupima corona? Acheni upuuzi huo!! Nendeni na wakati.
 
274570083_150123567433524_9028660031127190961_n.png

Februari 18, balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki alienda kwenye maabara mpya iliyojengwa na serikali ya Tanzania ili kupima virusi vya Corona huko Dar es Salaam. Hivi sasa maabara hii inafanya majaribio ya PCR na kingamwili.

Serikali ya Tanzania imeiajiri Kampuni ya BGI ya China ambayo inaongoza duniani katika ujenzi na usimamizi wa maabara kutekeleza mradi huo, kutokana na pendekezo la Ubalozi wa China nchini Tanzania.

Inaaminika kuwa Shirika la Ndegela Tanzania litapata fursa ya kurejesha safari za ndege za abiria kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou, China, wakati maabara hiyo mpya itakapoanza kufanya kazi kutokana na upimaji wenye uhakika zaidi wa virusi vya Corona.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania Bw. Ladislaus Matindi vilevile ameonesha matarajio hayo wakati balozi alipofanya ukaguzi.
 
Sasa kama kuna technology ya kupima corona kwa kutumia simu za mkononi na majibu sahihi yakapatina Papo kwa papo , kuna faida gani kwa nchi kwenda kuongeza madeni China ya kujenga kiwanda eti cha kupima corona? Acheni upuuzi huo!! Nendeni na wakati.
Punguza upuuzi.
Hakuna kitu kama hicho, ukisoma kitu jiongeze ujue sababu na etc.

Kama programu tumishi ya simu ingekuwa na uwezo huo sidhani kama dunia na wataalam wangeweza kukaa kimya.

Hizo ni zenu kwa ajili ya watengenezaji kupata pesa kila mnapo_downloads.
 
Punguza upuuzi.
Hakuna kitu kama hicho, ukisoma kitu jiongeze ujue sababu na etc.

Kama programu tumishi ya simu ingekuwa na uwezo huo sidhani kama dunia na wataalam wangeweza kukaa kimya.

Hizo ni zenu kwa ajili ya watengenezaji kupata pesa kila mnapo_downloads

Wewe unaishi dunia gani? Hiyo technology inatumika hivi sasa hapo visiwani Zanzibar!! Halafu kwa ujinga wako unadhani haiwezekani!
 
Back
Top Bottom