Serikali ya Tanzania yasema maduka ya kubadilisha fedha yatafunguliwa baada ya uhakiki kukamilika

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Serikali ya Tanzania yasema maduka ya kubadilisha fedha yatafunguliwa baada ya uhakiki kukamilika

Friday May 17 2019


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewatuliza wamiliki wa maduka ya kubalisha fedha ambayo hivi karibuni yalifungwa, kwamba yatafunguliwa baada ya Benki Kuu (BoT) kukamilisha uhakiki.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 18, 2019 jijini Arusha katika ufunguzi wa semina ya wanahisa wa Benki ya CRDB, Majaliwa amesema BoT inakamilisha taratibu za kutolewa vibali kwa baadhi ya maduka hayo.

"Msiwe na mashaka vibali vitatoka hivi karibuni kwa maduka maalum ili kuendelea kutoa huduma lakini pia kuna benki zinatoa huduma nzuri ya kubadilisha fedha ikiwepo benki ya CRDB,” amesema

Awali Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameishauri CRDB kuteua moja ya matawi yake jijini Arusha kufanya kazi hadi usiku ili kutoa huduma ya kubadilisha fedha.

Amesema Arusha ni Jiji la kitalii, ili kuondoa adha kwa watalii huduma ya kubadilisha fedha zinapaswa kuboreshwa zaidi.

Hivi karibuni BOT kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama waliendesha operesheni ya kufunga maduka ya kubadilisha fedha, katika majiji ya Arusha na Dar es salaam na manispaa ya Moshi na kusababisha adha kwa watu kwa wananchi na wageni.

 
Unajua uchafu ulikuwa unafanywa na haya maduka?10% ndo walikuwa waaminifu na ndo maana wana hakiki sasa.

Kizazi cha nyoka hiki kinachotetea uovu masaa 24

Majizi yote tulieni dawa iingie vizuri
Mkuu nipo chato hapa taa nyekundu imewaka na upande wa pili wanapita punda, ohoooooo naona baba punda kaamua kumpeleka kileleni mama punda! Inabidi tuwasubiri wamalizane ndio tupite!!! Dah jamani huu utalii wa ndani.
 
Hakuna uchafu wowote zwazwa wewe! Kama kulikuwa na uchafu kwanini wasikamatwe na kupandishwa kizimbani juha wewe?

Kuna uchafu kama wa huyo nduli wa kuua Watanzania, kukwapua 2.4 trillions hazina na maovu yake mengine chungu nzima?

Unajua uchafu ulikuwa unafanywa na haya maduka?10% ndo walikuwa waaminifu na ndo maana wana hakiki sasa.

Kizazi cha nyoka hiki kinachotetea uovu masaa 24

Majizi yote tulieni dawa iingie vizuri
 
Hii awamu watu ndio wanaongea sana kuliko action, yaani sifa zimezidi kuliko vitendo
 
Unajua uchafu ulikuwa unafanywa na haya maduka?10% ndo walikuwa waaminifu na ndo maana wana hakiki sasa.

Kizazi cha nyoka hiki kinachotetea uovu masaa 24

Majizi yote tulieni dawa iingie vizuri
Hufahamu kitu unasimuliwa
Elezea kama unaelewa bureau operations

Mkuu hujui lolote lile kwenye biashara na Huna elimu ya biashara

Unasikiliza maneno ya wanasiasa unawashwa mdomo na kuandika eti "ungejua walivyokuwa wanafanya bureau"

Wewe ni mpumbavu kabisa, Soko la pesa linaongozwa na Market forces of demand and supply katika modern economy
 
Mzalendo keshashindwa kuongoza nchi, kinachofanywa hapa ni kumfichia aibu 2020 arudi kutawala kuondoa aibu ya kuwa Rais wa kwanza kutawala muhula mmoja..

Ukibisha nieleze kauli ya kumalizia dk 45 zilizobaki inamaanisha nini?
 
Back
Top Bottom