Serikali ya Tanzania yapiga Marufuku ndoa kufanyika bila ya vyeti vya kuzaliwa kuanzia 1/5/2017

Mwakyembe Mwakyembe msomi, Waziri wa Sheria , mbunge wa kyela hivi Waziri wangu unauhakika gani kuwa Serikali yako ilikwisha to a vyeti vya kuzaliwa Kwa RAIA wake wote ?
 
Kuna wakati huyu waziri wa Sheria tena Daktari wa Falsafa anaongea mambo chechefu kiasi cha kutoweza kumtofautisha na konda au dereva toyo. Professional zao zimebaki kwenye makaratasi yanayoitwa vyeti tu lakini alichosomea huoni akiki apply kuwasaidia Watanzania. Kauli kama hizi zina expose uwezo finyu wa kufikiri na kufanya maamuzi yenye maslahi endelevu kwa Taifa letu. Ijulikane hapigii mbwa mluzi wala ng'ombe ambao wakiusikia wana respond tu bali anazitoa kauli kwa watu wenye akili timamu wenye uwezo wa kuchambua na kufanya assessment ya kila neno na kufanya conclusion. Ili kiongozi aheshimike basi atathmini athari za kauli na matamko anazotoa kwa watanzania. Tumeona kauli za viroba zilivyoleta athari kubwa kwani implementation approach haikuwa na common strategy bali kila RPC alifanya alivyojua akilini mwake. Aseme pia kuoa bila birth certificate kumeleta madhara gani tangu Uhuru na sisi tulioko kwenye ndoa ambao hatuna birth certificate tutahesabiwa kuwa ndoa haina vigezo au vipi. Je nani mwenye mamlaka ya kusema ndoa imekidhi viwango au la?; ni Cheti cha kuzaliwa?. Tunako kwenda ni gizani zaidi kuliko tulikotoka
 
Kumbe mpaka leo wameshindwa kupanga mipango ya kimaendeleo kwa sababu watu walikuwa wanaoana bila vyeti vya kuzaliwa!

Najiuliza kimoyo moyo.
 
Wana jf naimani hii hbr ya waziri wa sheria na katiba mh mwakyembe ya kutaka wanaofunga ndoa wote kuanzia mei mosi mwaka kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Kimsingi binafsi nafaham umuhim wa kuwa na cheti cha kuzaliwa hasa katk mambo kama ya kutafuta ajira kuhitajika kwenye taasis za elimu. Sasa sijaelewa uhusiano uliopo kati ya kuoa/kuolewa na ulazima wa kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa nni wasiseme tu kwamba kila mtanzania ni lazima awe na cheti cha kuzaliwa? Wenye ufahamu tafadhali mtusaidie
Wanasiasa wanapayuka wanazuoni wanaandika
Siku hizi kila anayepata upenyo kwa kusema lake anaongea
 
Hivi tupo serious na matamko tunayoyatoa? Mkuu alianza kwa kutuaminisha kwamba hakuna mtu atakayepona kwa kutumia vyeti feki, tumeona watu wengi waliolitumikia taifa tangu awamu ya mzee Mkapa hadi mzee Kikwete wakifukuzwa kazi kwa tuhuma ya kuwa na vyeti feki, hatukusikia watu wakiwatetea kama alivyofanya Mrisho kumtetea jamaa kuwa vyeti siyo tija mradi utendaji wa kutukuka. Ukijiuliza swali rahisi, hivi hao waliofukuzwa na kukosa stahiki zao za kustaafu hawakuwa wanafanya kazi vizuri?

Leo Mwakyembe amejitokeza hadharani akipiga marufuku kufunga ndoa hadi uwe na cheti cha kuzaliwa, amesahau kuwa mtu yeyote anayo haki ya kuolewa na mtu wa taifa lolote mradi tu wamependana na kukubaliana. Pila amesahau kuwa rita hutoa cheti cha kuzaliwa kwa kila mtoto anayezaliwa nchini hata kama siyo raia wa Tanzania.

Lipo tatizo kubwa katika utawala huu
 
Ni jambo jema sana kuwa na cheti cha kuzaliwa mnapofunga ndoa. Lakini je ni njia gani itatumika kuwezesha hicho cheti cha kuzaliwa kipatikane kwa kila mwananchi anayekihitaji? Huduma ya kutoa hivi vyeti imekuwa dhaifu sana hivyo upatikanaji wake umekuwa wa kusuasua na wenye kuudhi. Hivyo ni jukumu sasa la Mh Waziri kuhakikisha upatikani wa cheti unakuwa wa rahisi kwa kila eneo.
 
Wanazuoni njoo mtuelimishe kama kuna ammendment imeshafanyika kwenye marrieage act au mtaalam keshadondosha hicho kipengele kwenye GN.Navyojua mm ndoa ni muunganiko wa watu wawili wa jinsia tofauti ambao kwa hiari yao wanaamua kuishi pamoja kama mke na mme.Yeyote anayekataa wasiuangane watu hawa nje ya vipengele vilivyoainishwa kisheria anakuwa amekwenda kinyume na kifungu hiki na adhabu iko pale.
B Sijaona kipenele cha kukataa ndoa isifanyike kwa kukosa vyeti vya kizaliwa.Mm nashauri sheria itungwe ya kutaka kila mtanzania awe na cheti cha kuzaliwa wananchi tutamuelwa waziri wetu ila hii ya ndoa ni kubwa yake.
 
Wakati mwingine wanasiasa wananishangaza.
Huwa wamekaa huko juu na kusahau kabisa waliko toka.
Tamko hili la Waziri wa Sheria na Katiba Dr Harrison Mwakyembe, kuwa watu wasifunge ndoa hadi waonyeshe vyeti vya ndoa, kwa kweli limetia fora.

Tukimvhukua Mwakyembe alikotoka, Kyela, nina uhakika yeye mwenyewe ana ndugu ambao licha ya kutojua haswa tarehe ya kuzaliwa , hawana kabisa vyeti vya kuzaliwa.

Sababu kubwa kama ilivyo kwa wananchi wengi wa vijijini, ni kuzalishwa na wakunga wa jadi.
Na hao wakunga hawatoi vyeti vya kuzaliwa!

Kazi kwako !
I sadi it!
Asante Mh Dr JPJ Magufuli kwa kuliona tatizo na kufuta agixo la Mwakyembe.
 
Kwani yeye Ni Bunge, kutoa orders Kama hizo zina violate principal law, "Law of Marriage Act" maana yake kutakuwa hakuna "presumption of marriage"

Lakini pia, Ni kwenda kinyume Na Mungu ambaye yeye ndiye aliyeanzisha ndoa, so binadamu hawezi kuzuia watu wasioane, huku Napo Ni kuingilia uhuru WA watu kikatiba.

Bila shaka, hili haliwezi kufanikiwa
 
tapatalk_1489737545100.jpeg
[ATTAC
tapatalk_1489737545100.jpeg
 
Back
Top Bottom