Serikali ya Tanzania yakaribisha tena wafanyabiashara kununua korosho

Ata mimi nataka kilo 100vipi wataniletea?
Kwa ufupi
Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema mfanyabiashara, Brian Mutembei wa kampuni Indo Power Solutions ya Kenya anakamilisha taratibu za kisheria na biashara kwa ajili ya kununua tani 100,000 za korosho

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi efilbert@mwananchi.co.tz
Arusha. Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema mfanyabiashara, Brian Mutembei wa kampuni Indo Power Solutions ya Kenya anakamilisha taratibu za kisheria na biashara kwa ajili ya kununua tani 100,000 za korosho nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 20, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha huku akiwakaribisha wafanyabiashara wengine zaidi kununua korosho kwa kiwango cha chini wanachoweza.

"Hadi jana Februari 19, 2019 Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko chini ya timu ya pamoja ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Kilimo ilikua imekusanya jumla ya tani 221,060 za korosho ghafi kutoka kwa wakulima," amesema Kakunda.

Amesema amepatikana mnunuzi mwingine ambaye ni kampuni ya Bi -Southern ya jijini Dar es Salaam itakayonunua tani 15,000 za korosho baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia mkataba na maelekezo ya kisheria kutekelezwa.

Kakunda ameeleza hayo zikiwa zimepita siku 10 tangu kusambaa kwa taarifa kuwa kampuni ya Indo Power haina uwezo wa kununua tani 100,000 za korosho nchini.

Serikali ikajibu taarifa hiyo kuwa haiangalii mambo mengine, bali uwezo wake wa kutekeleza masharti ya mkataba.

Januari 30, Serikali ilitangaza kumpata mteja atakayenunua tani 100,000 za korosho kwa Dola 180,000 za Marekani (zaidi ya Sh418 bilioni) na wiki mbili tangu kutolewa kwa taarifa hiyo, gazeti la kila wiki la The East African lilichapisha habari kuwa kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka 2016 haina historia ya kufanya miamala mikubwa kiasi hicho.

Katibu mkuu wa wizara ya viwanda na Biashara, Profesa Joseph Buchweishaija alilieleza Mwananchi kuwa historia si hoja ya msingi waliyoipa kipaumbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najalibu kutafakari itakapogika October 1 2019 wakulima watahitaji maghara yao kwa ajiri ya kuhifadhia mazao yao na ili hali bodi ya mazao mchanganyiko itakua korosho zishaoza aijuwi pango watamlipa nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi
Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema mfanyabiashara, Brian Mutembei wa kampuni Indo Power Solutions ya Kenya anakamilisha taratibu za kisheria na biashara kwa ajili ya kununua tani 100,000 za korosho

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi efilbert@mwananchi.co.tz
Arusha. Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema mfanyabiashara, Brian Mutembei wa kampuni Indo Power Solutions ya Kenya anakamilisha taratibu za kisheria na biashara kwa ajili ya kununua tani 100,000 za korosho nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 20, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha huku akiwakaribisha wafanyabiashara wengine zaidi kununua korosho kwa kiwango cha chini wanachoweza.

"Hadi jana Februari 19, 2019 Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko chini ya timu ya pamoja ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Kilimo ilikua imekusanya jumla ya tani 221,060 za korosho ghafi kutoka kwa wakulima," amesema Kakunda.

Amesema amepatikana mnunuzi mwingine ambaye ni kampuni ya Bi -Southern ya jijini Dar es Salaam itakayonunua tani 15,000 za korosho baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia mkataba na maelekezo ya kisheria kutekelezwa.

Kakunda ameeleza hayo zikiwa zimepita siku 10 tangu kusambaa kwa taarifa kuwa kampuni ya Indo Power haina uwezo wa kununua tani 100,000 za korosho nchini.

Serikali ikajibu taarifa hiyo kuwa haiangalii mambo mengine, bali uwezo wake wa kutekeleza masharti ya mkataba.

Januari 30, Serikali ilitangaza kumpata mteja atakayenunua tani 100,000 za korosho kwa Dola 180,000 za Marekani (zaidi ya Sh418 bilioni) na wiki mbili tangu kutolewa kwa taarifa hiyo, gazeti la kila wiki la The East African lilichapisha habari kuwa kampuni hiyo iliyosajiliwa mwaka 2016 haina historia ya kufanya miamala mikubwa kiasi hicho.

Katibu mkuu wa wizara ya viwanda na Biashara, Profesa Joseph Buchweishaija alilieleza Mwananchi kuwa historia si hoja ya msingi waliyoipa kipaumbele.
Hahahahahahahaha
 
Mambo makubwa ka ununuzi wa korosho huwa hayatolewi kwa kukurupuka inatakiwa wataalam wa uchumi wafanye upembuzi yakinifu ndio kauli itoke nafikiri Jiwe amejifunza kitu katika hili
UCHUMI NI SCIENCE SIO SIASA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mr. Stone ni habari nyingine! Hana utayari wala uthubutu wa kujifunza. Yeye ni alfa na omega katika kila jambo. Tumshukuru Mwenyezi Mungu, huenda ikawa amemleta kwa makusudi yake!!!
 
Halafu watu wanakwambia jiwe ananyoosha nchi ,atatufikisha mbali ,korosho tu imemshinda chini ya maamuzi yake mwenyewe, hivi huyu ndo atafanya muujiza gani kuiendeleza nchi .
 
Nasikia jeiwii kuna uhaba wa mabomu ya kubangulia koroshow

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Mshika mawili moja humponyoka je,mshika mengi?Ndege wewe koroshounataka wewe"maana sidhani kama bodiyakorosho iliamuwa hivyo"kuzinduwa wewe,misifa wewe"helazipo nataka hilijambo lifanywe mala moja"milioni hamsini kilakiji wewe,madarakawewe
kwahiyo mshika mengi huulumia
 
Back
Top Bottom