Serikali ya Tanzania yadaiwa kunakili katiba ya Kenya

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi,James Mbatia,amesema katiba iliyo andaliwa na serikali inayotarajiwa kufikishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa imenakiliwa kutoka katiba ya kenya.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam,kwa niaba ya wanachama wake mwenyekiti wa chama hicho alisema muswada wa katiba unaotarajiwa kuletwa na serikali ni marejeo ya katiba namba tisa(9)ya mwaka 2008Alisema kilichofanyika katika katiba mpya iliyo andaliwa ni uigaji na hata kunakili moja kwa moja sheria ya nchi nyingine hali ambayo itasababisha hatari ya kuingiza sheria isiyoandamana na mila,desturi,siasa na hata utamaduni wa wananchi.
 
:tape:

Serikali ya vilaza, kama kawa copy and paste vichwa vyeupe

Kama elimu za kupewa na kuhongwa unatarajia nini?.........

Hata mikataba yenyewe huwa wanaenda kuomba nje ambayo imekwisha andaliwa na kazi ya ku-edit bila hata kuipitia kwa undani na ndio maana inakuwa na clause unazojiliza hawa watu walificha akili makalioni wakati wa kutengenez hiyo mikataba au?

Btw tunataka katiba inayoandikwa kutoka kwenye makundi ya jamii na kisha jamii nzima....wachukue ya wale jamaa wakina Kiwanga wanayoandaa wasituletee adabrakadabra zao
 
Kwani mmeshasahau hata risala za mbele ya mgeni rasmi kwenye sherehe yoyote in vivyo hivyo!
 
Suala si copy n' paste, je, inatufaa? Mbatia alitakiwa aseme ni kitu gani kibaya kilichopo kwenye hiyo sheria ili kijadiliwe!
 
Hamna tutakachotunga kije kuwa kipya ulimwenguni kote, ila tuseme kwa mfano mapungufu ya katiba ya kenya ni haya, na hatuyahitaji.

Sio kuja kukurupuka tu,eti mila na desturi ni tofauti! Kwani wakenya wana tofauti kubwa ipi na sisi? Kuna wajaluo,wamasai,wakurya kama ilivo tz. Hii sio hoja kabisa.
 
Mbatia anajitafutia umaarufu wa bure, nchi zote duniani uandika sheria zake kwa kutumia sheria za nchi nyingine baada ya kuzifanyia marekebisho stahiki. Kwetu hapa sheria nyingi zilizotungwa zimenakiliwa kutoka India. Kama mh.Mbatia ndipo hivi sasa analijua jambo hili amechelewa sana, naomba atupishe hasije akatupotezea muda kwa kujadili mambo yasiyokuwa ya msingi.
 
:tape:

Serikali ya vilaza, kama kawa copy and paste vichwa vyeupe

Kama elimu za kupewa na kuhongwa unatarajia nini?.........

Hata mikataba yenyewe huwa wanaenda kuomba nje ambayo imekwisha andaliwa na kazi ya ku-edit bila hata kuipitia kwa undani na ndio maana inakuwa na clause unazojiliza hawa watu walificha akili makalioni wakati wa kutengenez hiyo mikataba au?

Btw tunataka katiba inayoandikwa kutoka kwenye makundi ya jamii na kisha jamii nzima....wachukue ya wale jamaa wakina Kiwanga wanayoandaa wasituletee adabrakadabra zao

Kuna wakati walifanya the same kwenye loan forms kule loan board na wanafunzi wakawa wanashindwa kujaza baadhi ya vipengele kwani vilikuwa irrelevant kwao. Angalia policies za mawizara zinavyofanana ndo utaona kazi ya copy and paste ilivyopata walaji Tanzania na hii dhambi inaanzia kule shuleni mambo ya kukariri maswali ya mitihani thru tuitions, wakija chuoni desa na wakienda kazini the same practice maana tayari imekuwa part of training!
 
Habari zaidi tusomeni hapa chini

Saturday, 02 April 2011 09:27
Fidelis Butahe
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimeuponda muswada wa marejesho ya Katiba ya Tanzania wa mwaka 2011 kwa kuwa unampa mamlaka makubwa Rais, yakiwamo mamlaka ya kuunda Tume ya Kutunga Katiba. Pia chama hicho kimesema muswada huo ambao utajadiliwa Bungeni Juni mwaka huu, hauna lolote kwa kuwa umenakiliwa ‘neno kwa neno' kutoka Sheria ya Kenya ya Marejeo ya Katiba namba 9 ya mwaka 2008.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alisema maudhui ya muswada huo yanaonyesha wazi serikali imekamia kuunda Tume ya kutunga katiba ambayo itateuliwa na Rais. "Pendekezo hilo linamaanisha kuwa Rais ndiye mdau katika mchakato wa kutunga katiba mpya, vifungu vya 5,6(1) na (2) katika muswada huu, vinampa mamlaka makubwa Rais.
"Viko vifungu vingi vinavyompa mamlaka rais ni kifungu cha 8(1), 13(2), 13(4), 14(2), 16(2), 16(3), 21(1), 21(3), 23(3), 23(4) na 25(2)," ,"alisema Mbatia. Mbatia alisema kazi ya kutungwa kwa katiba lazima liwashirikishe Watanzania kwa kuwa katiba ni kauli ya umma kuhusu utawala wa nchi na jinsi wanavyotaka kuishi.
"Rais ni mtumishi namba moja wa taifa lake, hana nafasi au mamlaka ya kulitungia taifa lake katiba,"alisema Mbatia. Alisema rais anapaswa kuviachia vyombo huru vya umma ili vianze mchakato wa kutunga katiba mpya.

"Kwa kuwa hatuko katika nafasi sifuri, yaani bila taifa wala dola, ni vyema kiutaratibu kupeleka bungeni muswada wa marekebisho ya ibara ya 98 ili iruhusu bunge kutunga sheria ya baraza la kutunga katiba na sheria ya kura za maoni,"alisema Mbatia.

Alisema hatua ya pili ni kupelekwa bungeni muswada wa sheria ya baraza la kutunga katiba na sheria ya kura za maoni na kusisitiza kuwa mambo hayo mawili yanaweza kufanywa wakati mmoja katika kikao kijacho cha bunge. Baraza la kutunga Katiba
Mbatia alifafanua itungwe sheria ya baraza la kutunga katiba na wabunge wa bunge la Jamhuri wawe wajumbe wa baraza hilo huku likiwa na wajumbe wengine.
"Wajumbe wengine wawe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano na la Serikali ya Zanzibar, mwakilishi wa chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa, mwakilishi wa asasi ya kitaifa ya kijamii, makamu wakuu wa vyuo vikuu, wawakilishi wa vyama vya siasa.
"Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, majaji wa mahakama za rufani, marais wastaafu, mawaziri wakuu, wawakilishi wa madhehebu ya dini, watu 10 mashuhuri watakaopendekezwa na bunge pamoja na wakuu wa vituo vya sheria," alisema. Alisema baraza hilo linapaswa kuwa na mamlaka ya kuteua Tume ya Kutunga Katiba.
Serikali imenakili sheria ya Kenya

Mbatia alisema muswada wa marejeo ya katiba wa mwaka 2011 umenakiliwa kutoka sheria ya Kenya ya Marejeo ya Katiba namba 9 ya mwaka 2008 na kufafanua kuwa sheria hiyo iliridhiwa na Rais wa Kenya, Desemba 11, 2008 na kuanza kutumika, Desemba 22, 2008.
"Kuiga au kunakili moja wa moja sheria ya nchi nyingine si jambo la ajabu, lakini lazima ujihadhari na mambo ambayo hayaihusu nchi yako na hasa hatari ya kuiga sheria isiyoandamana na mila, desturi, siasa, utamaduni na mahitaji ya wakati huo," alisema Mbatia.

Alisema kama mazingira ya Kenya yalihitaji marejeo ya Katiba, mazingira ya Tanzania hayahitaji suluhisho kama hilo bali yanahitaji katiba mpya na kuhoji kwamba iweje muswada huo unakiliwe neno kwa neno wakati Tanzania kuna wataalamu wengi wa masuala ya katiba na sheria.
"Kenya ni nchi yenye muundo rahisi kikatiba ‘simple state', wakati Tanzania ni nchi yenye muundo mgumu ‘complex state' , Tanzania ni Jamhuri ya Muungano, Kenya wao ni Jamhuri tu, sasa wapi na wapi," alisema Mbatia.
Naye Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa chama hicho, Dk Sengondo Mvungi alifafanua kwamba hawana lengo la kufungua kesi mahakamani kupinga muswada huo bali watawatumia wabunge wa chama hicho kuomba mabadiliko ya muswada huo bungeni.

"Inawezekana kabisa wataalamu wa Rais wakawa wamempotosha kuhusu hili la muswada, Rais hasipelekwe kabisa katika hili, maana hapa kwetu Zanzibar tayari nchi, Tanganyika je, ni mkoa au, wananchi wanatakiwa kulitambua hili," alihoji Mvungi.
Mwananchi newspape
 
Hapo kwenye blue ndio pananitatanisha tunashindwa kuelewa kabisa,hivi mfumo gani huu tuliona,hatuwezi kuiga kenya sisi kwa sabau tuna serikali mbili ambazo zilizoungana na tukapata mfumo wa muungano,halafu nchi moja kufuta utaifa wake hivi ni mfumo gani huu,kweli wa kuwaiga wakevya sisi ?

Kwa irudishwe tanganyika ikisha ndio tujadili katiba,au muungano.
 
Back
Top Bottom