Serikali ya Tanzania ovyo sana

idumu

Member
Jun 5, 2009
44
1
Jamani nasikitika kwa kusema nchi yetu haina uongozi coz umejaa rushwa na ubinafsi, Kwa nini nasema hivyo:

1. Hivi uliona nchi gani shirika limebinafishwa lakini linapewa pesa na serikali, Mfano TRL(Shirka la Reli) ina management(Uongozi) wahindi 14 na hamna wanachokifanya then mnawapa Bil 45 za nini?? Wizi tu hapa na me nasema ipo siku, Huyu JK ameshindwa NCHI ajihuzulu

2. Pili TICTS inatuingizia hasara, Kwa nini wanaikumbatia?? Kuna nini hapo???

Sasa Rwanda, Burundi na Congo wamehamia bandari ya Mombasa ajili ya UPUMBAVU WA VIONGOZI WETU, Huyu Rais wetu yupo makini kweli au amelishwa nini??

3. Nchi hii na wabunge wote wa CCM kutoa wachache tu ni makini mengine yako bungeni kupokea posho tu, WATZ TUAMKENI, we kama unakatwa kodi kwenye mshahara wako, unalipia shule za kata, unachangia uchafu nyumbani kwako, Unalipia bill ya UMEME, unalipia MAJI, unalipia kodi ya GARI LAKO, unalipia kodi ya DUKA LAKO AU OFFICE YAKO, Je kuna umhmu wa wa wewe au mimi kuendelea kutetea hawa viongozi hawana huruma, HUYU JK HANA WASHAURI WA UCHUMI, Tafakari

4. TAASISI DINI nani kasema zinarushwa?? Serikali, Kwa nini wasikamatwe?? Hiyo DECI miaka 3 nchini ipo WALIKUWA WAPI kama viongozi???
Je hospitali ngapi ni za taasisi za dini kusini, kanda ya ziwa, Kaskazini na sehemu zingine. Mfano Kaskazini huduma nyingi za afya ni za mashirika ya DINI.

Je hili mnalionaje ?? I am hating kuwa na viongozi hawana upeo wa akili na maamuzi yenye kuleta Tija na maendeleo nchini.

TOA MAONI YAKO
 
Mkuu hayo uliyoyasema hapo juu....ndo kila siku tunayapigia kelele hapa JF na kwingineko kuliko na wanaharakati!

Lakini hiyo title yako ungeedit kidogo iwe ...''Serikali ya Tanzania hovyo sana'' na si Tanzania nchi hovyo Tanzania kama Tanzania to me hakuna mfano wako....imeja kila aina ya neema na upendeleo wa kila aina toka kwa Mungu! Ina mito mingi sana, maziwa mengi, bahari, milima, mbuga za wanyama, ardhi yenye rutuba, madini ya kila aina etc!

Tatizzo letu nchi hii iliyojaaa asali na maziwa imekosa serikali madhubuti ya kusimamia vyema rasilimali hizo na kuiziconvert into lulu ya kuwaondolea umasikini watanzania! Viongozi wetu kila moja kwa nafasi yake anajitahidi kutumia kanafasi hako kumaximize personal wealth kwa njia yoyote ile hata iwe kwa kuangamiza rasilimali hizo! Viongozi wetu ni wabinafsi, wamekosa moyo wa kizalendo kabisa wanatetea matumbo yao tu!

Hivyo ni watu hasa viongozi ndio waliosababisha Tanzania iwe hivi ilivyo sasa....hawa ndio hovyo!
 
Tanzania kama Tanzania to me hakuna mfano wako....imeja kila aina ya neema na upendeleo wa kila aina toka kwa Mungu! Ina mito mingi sana, maziwa mengi, bahari, milima, mbuga za wanyama, ardhi yenye rutuba, madini ya kila aina etc!

This is my country.....
Hivi vipaji vyote vimetusaidia vipi?
Nani wa kulaumiwa?
 
Idumu, unajua hii nchi imefika mahali viongozi wanaona WaTZ kama watoto wadogo wasioelewa kitu. Ukiangalia hiyo TRL ilikuwa ni mpango maalum wa viongozi walijua kwamba watu wanaowaleta hawana uwezo lakini kwa kuwa walishafanya mahesabu yao, wao hawamfikirii Mtanzania mradi matumbo yao yamenenepa basi. Lakini Kama alivyosema Mbunge mmoja Bungeni kwamba wawe wanasoma na Maandiko ya Mungu. wakumbuke kwamba hapa duniani ni wapitaji na kwamba wanaweza kuja kupata vifo vya mahangaiko sana pamoja na MIPESA yao.
 
Kwa kweli uozo ni mwingi sana katika serikali yetu - na uozo huu kwa vile unaumiza mwananchi wa kawaida na kuwafanikisha wachache tu mafisadi - ambao wamesahau kuwa kuna Mungu - sijui hiyo MIPESA WATAENDA NAYO WAPI - WANADHANI WATAISHI MILELE DUNIANI - kwa kweli WATZ tuamkeni - mimi nina shida moja - sioni nani atatukwamua, hebu tushauriane hatua za kuchukua - unafanya kazi kwa nguvu zako zote na unachopata kidogo - bado wanakichukua kwenye MA-TAX kibao walizoweka - nini kitatufungua tutoke kwenye shida hii?? au itakuwa hivi milele?? LAITI WAANDISHI WA HABARI WANGEKUWA WANAANDIKA MAMBO YOTE YA KIFISADI YANAYOTOKEA KWA UWAZI - ILI KILA MTANZANIA AELEWE KINACHOENDELEA - wengine hawajui - wanasikia tu RELI, BANDARI ETC. inatakiwa hata wale walio vijijini waelewe ili tuungane tulio tuchukue hatua - na nani kiongozi wetu - oh my God I have so many questions in my mind - someone help me get answers!!!!!
 
Mimi kusema ukweli nalia na wasomi wa nchi hii hasa walio katika vyuo vyetu vikuu maana hao ndio chachu ya mapinduzi ya kweli sehemu yoyote duniani lakini hapa kwetu wasomi wetu wanakubali kupelekwa kama gari bovu.
Kuna nchi nyingi ambazo mapinduzi (yaani mabadiliko ya kiuchumi,kijamii,kiutamaduni na kisiasa) yamefanikiwa kwa uongozi wa wasomi wao walio vyuoni, sasa hapa kwetu jambo hilo linaonekana gumu.WASOMI MPOOOO!!!!?????
 
1. Hivi uliona nchi gani shirika limebinafishwa lakini linapewa pesa na serikali, Mfano TRL(Shirka la Reli) ina management(Uongozi) wahindi 14 na hamna wanachokifanya then mnawapa Bil 45 za nini?? Wizi tu hapa na me nasema ipo siku, Huyu JK ameshindwa NCHI ajihuzulu

Idumu,

Mambo mengi umerudia yaliyokwisha jadiliwa ila nisemee moja tu!... Tanzania Railway Limited ni kampuni inayomilikiwa kati ya Governement of Tanzania na RITE (shirika la reli la india, strategic investor according to walamali).

Sasa ndugu unatakiwa kuelewa yafuatayo... huenda billion 45 zimekopwa... na TRL, hivyo ni hela zinaenda kuingia kwenye vitabu vya TRL... nadhani serikali inatoa dhamana tu...

Pili namna nyingine ya ku-bail out ni serikali kuongeza hisa zake TRL na baadaye huenda TRL kurudi kuwa mali ya serikali.

Nilidhani niweke hiyo wazi kidogo kwa faida yetu wote.
 
Jamani nasikitika kwa kusema nchi yetu haina uongozi coz umejaa rushwa na ubinafsi, Kwa nini nasema hivyo:

1. Hivi uliona nchi gani shirika limebinafishwa lakini linapewa pesa na serikali, Mfano TRL(Shirka la Reli) ina management(Uongozi) wahindi 14 na hamna wanachokifanya then mnawapa Bil 45 za nini?? Wizi tu hapa na me nasema ipo siku, Huyu JK ameshindwa NCHI ajihuzulu

2. Pili TICTS inatuingizia hasara, Kwa nini wanaikumbatia?? Kuna nini hapo???

Sasa Rwanda, Burundi na Congo wamehamia bandari ya Mombasa ajili ya UPUMBAVU WA VIONGOZI WETU, Huyu Rais wetu yupo makini kweli au amelishwa nini??

3. Nchi hii na wabunge wote wa CCM kutoa wachache tu ni makini mengine yako bungeni kupokea posho tu, WATZ TUAMKENI, we kama unakatwa kodi kwenye mshahara wako, unalipia shule za kata, unachangia uchafu nyumbani kwako, Unalipia bill ya UMEME, unalipia MAJI, unalipia kodi ya GARI LAKO, unalipia kodi ya DUKA LAKO AU OFFICE YAKO, Je kuna umhmu wa wa wewe au mimi kuendelea kutetea hawa viongozi hawana huruma, HUYU JK HANA WASHAURI WA UCHUMI, Tafakari

4. TAASISI DINI nani kasema zinarushwa?? Serikali, Kwa nini wasikamatwe?? Hiyo DECI miaka 3 nchini ipo WALIKUWA WAPI kama viongozi???
Je hospitali ngapi ni za taasisi za dini kusini, kanda ya ziwa, Kaskazini na sehemu zingine. Mfano Kaskazini huduma nyingi za afya ni za mashirika ya DINI.

Je hili mnalionaje ?? I am hating kuwa na viongozi hawana upeo wa akili na maamuzi yenye kuleta Tija na maendeleo nchini.

TOA MAONI YAKO

Mkuu,
Nadhani jazba sasa imeshapungua.
Kwa vile hayo uliyoyaweka hapo juu si mageni hapa jamvini, basi si vibaya sasa ukatupa alternatives au ukasema constructively nini kifanyike.
 
Si mlisema serikali yote hii ni chaguo la Mungu mkawapa vichwa na sifa wasizostahili???na bado waliotoa pesa zao wanarudisha pesa zao na kupata faida hadi 2015 ndio watakuwa wameshamalizana wanasubiri bogus mwingine ajipendekeze kuomba pesa zao......maana uraisi unaenda kuomba kwao...mafisadi na wafanya biashara wakubwa.....wengine wote mil karibu 39.5 ni wasindikizaji tuu...wa tabaka dogo sana la wanaojifanya wameteuliwa....kuwa viongozi.
 
Jamani nasikitika kwa kusema nchi yetu haina uongozi coz umejaa rushwa na ubinafsi, Kwa nini nasema hivyo:

1. Hivi uliona nchi gani shirika limebinafishwa lakini linapewa pesa na serikali, Mfano TRL(Shirka la Reli) ina management(Uongozi) wahindi 14 na hamna wanachokifanya then mnawapa Bil 45 za nini?? Wizi tu hapa na me nasema ipo siku, Huyu JK ameshindwa NCHI ajihuzulu

2. Pili TICTS inatuingizia hasara, Kwa nini wanaikumbatia?? Kuna nini hapo???

Sasa Rwanda, Burundi na Congo wamehamia bandari ya Mombasa ajili ya UPUMBAVU WA VIONGOZI WETU, Huyu Rais wetu yupo makini kweli au amelishwa nini??

3. Nchi hii na wabunge wote wa CCM kutoa wachache tu ni makini mengine yako bungeni kupokea posho tu, WATZ TUAMKENI, we kama unakatwa kodi kwenye mshahara wako, unalipia shule za kata, unachangia uchafu nyumbani kwako, Unalipia bill ya UMEME, unalipia MAJI, unalipia kodi ya GARI LAKO, unalipia kodi ya DUKA LAKO AU OFFICE YAKO, Je kuna umhmu wa wa wewe au mimi kuendelea kutetea hawa viongozi hawana huruma, HUYU JK HANA WASHAURI WA UCHUMI, Tafakari

4. TAASISI DINI nani kasema zinarushwa?? Serikali, Kwa nini wasikamatwe?? Hiyo DECI miaka 3 nchini ipo WALIKUWA WAPI kama viongozi???
Je hospitali ngapi ni za taasisi za dini kusini, kanda ya ziwa, Kaskazini na sehemu zingine. Mfano Kaskazini huduma nyingi za afya ni za mashirika ya DINI.

Je hili mnalionaje ?? I am hating kuwa na viongozi hawana upeo wa akili na maamuzi yenye kuleta Tija na maendeleo nchini.

TOA MAONI YAKO

Bwanamkubwa uliyoyasema ni kweli tupu!
Ila kitu kimoja nikusahihishe kwa mtazamo wangu, nchi yetu sio ovyo! Viongozi wetu hawa walitafuta uongozi kwa kuhonga, hawa kina JK hawa, ndiyo hovyo kabisa...kama alivyosema Selelii wanatafuta laana hawa, tusamehewe hapa lakini ni kweli wanastahili laana hawa!
 
Huwa nasikia tu eti tuna kikosi cha makomandoo pale ngerengere na mwenge mlalakua pia zanzibar je, wanangoja nini wasichukue nchi tukachagua rais wa mpito?
 
This is my country.....

Yes you are WOS......but......see my comments below!

Hivi vipaji vyote vimetusaidia vipi?

As of now nothing... WOS...!

Ila naweza sema huu utajiri umetusaidia kuamsha harakati za ukombozi wa kweli ili hatimaye urithi huo tuliopewa na Mungu utusaidia kututoa tutoka katika dimbwi kubwa la umaskini to The Next Level!''The heaven of Africa''

Kwa sasa ni watu wachache sana tena wengine hata si watanzania ndio haswa wanaofaidika na mema ya nchi yetu......inaniuma sana!

Nani wa kulaumiwa?

Ha!ha!....Wos Good question!

Wakwanza najilaumu mimi mwenyewe..... kwa sababu najiona kabisa sijaifanyia nchi hii lolote la maana.....japokuwa na mimi bi mojawapo nilofaidika na pesa za walipa kodi kule University! Angalia now, harakati zangu naziendesha hapa JF tena nyuma ya screen nikiopwa sijiui kuonwa vile....true kabisa najiona kabisa wakulaumiwa! Ningetamani niwe kama njiwa vile nikaruka mpaka pale mitaa ya Jangwani,Lumbila, Inio, Kidegembye, Busanda, KG etc nikusanye raia na kuwashushia nondo hizi juu ya HAKI YA MTANZANIA KWENYE RASIRIMALI ZA TANZANIA.....! bt I can't for now kwa sababu nyingi sana!

Pili nawalaumu watanzania wote wanapata fursa ya kufanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbalimbali kushindwa kutumia fursa hizo vizuri either kwa kuto shiriki uchaguzi au kwa kukubali kupokea rushwa ya nyama, pombe, t shirt etc ambavyo kny utajiri wa nchi hii ni kama a molecule baharini!

Tatu nawalaumu wale wachache walipata kuaminiwa na watanzania wachache kushika nyadhifa mbalimbali, wakawasaliti na kugeuza nyadhifa hizo mitaji ya biashara na ofisi za umma kugeuzwa mahala pa kufanyia biashara.....''Wamegeuza nyumba ya baba yangu mahala pa biashara......Jesus''. Nawalaumu sana!
 
Mimi kusema ukweli nalia na wasomi wa nchi hii hasa walio katika vyuo vyetu vikuu maana hao ndio chachu ya mapinduzi ya kweli sehemu yoyote duniani lakini hapa kwetu wasomi wetu wanakubali kupelekwa kama gari bovu.
Kuna nchi nyingi ambazo mapinduzi (yaani mabadiliko ya kiuchumi,kijamii,kiutamaduni na kisiasa) yamefanikiwa kwa uongozi wa wasomi wao walio vyuoni, sasa hapa kwetu jambo hilo linaonekana gumu.WASOMI MPOOOO!!!!?????

Hili ndilo tatizo sugu ,japo tunajaribu kulizunguka kwa sababu linatungusa wengi kama sote.
Uki hint point Tatizo la Tanzania ni tatizo la kisomi zaidi, yani UELEWA.Hii ndilo tatizo kuu na uozo wote umejikita hapa,Wasomi wamesoma,tumesoma lakini hatujaelimika hakika hili ndilo tatizo hakuna tatizo jingine.
 
Last edited:
Inaonekana unaupeo mpana ndugu. unaonane nawewe mwakani uchukue fomu za Ubunge au udiwani ili uingie kwenye system urekebishe uozo huo?
Tafakali!!
 
Mageuzi/mapinduzi yoyote huletwa na wananchi/raia/tabaka la chini kabisa baada ya kuchoshwa na vitimbi vya watawala. yaani muda ukifika utaona kila mtu anachukua hatua. Haihitaji wasomo wengi. Angali mapinduzi ya Ufaransa, Uingereza, Marekani na Urusi.
 
Idumu,

Mambo mengi umerudia yaliyokwisha jadiliwa ila nisemee moja tu!... Tanzania Railway Limited ni kampuni inayomilikiwa kati ya Governement of Tanzania na RITE (shirika la reli la india, strategic investor according to walamali).

Sasa ndugu unatakiwa kuelewa yafuatayo... huenda billion 45 zimekopwa... na TRL, hivyo ni hela zinaenda kuingia kwenye vitabu vya TRL... nadhani serikali inatoa dhamana tu...

Pili namna nyingine ya ku-bail out ni serikali kuongeza hisa zake TRL na baadaye huenda TRL kurudi kuwa mali ya serikali.

Nilidhani niweke hiyo wazi kidogo kwa faida yetu wote.
Lakini ukumbuke serikali ilivyo sema inaleta strategic investor ilisema haina hela na haiwe kuendelea kuwekeza kwenye mfuko uliotoboka, yyani wanawekeza lakini hakuna tija, sasa hizo fedha za kukopesha au kuwekeza kwa wahindi zimetoka wapi? ni yale yale ya ATC na SAA, Ya Alliance Air nk
 
Mimi kusema ukweli nalia na wasomi wa nchi hii hasa walio katika vyuo vyetu vikuu maana hao ndio chachu ya mapinduzi ya kweli sehemu yoyote duniani lakini hapa kwetu wasomi wetu wanakubali kupelekwa kama gari bovu.

Joe mimi nadhani kuwalaumu wasomi ni kuwaonea bure wao hawana hiyo nguvu kwani nchi inaongozwa na watu hopeless kabisa. Hapa wa kuwalaumu ni WATANZANIA WENYEWE. Haiingii akilini hii mijitu mijinga toka uhuru inaongoza hakuna mabadiliko ya maana still kila baada ya miaka mitano inakuja kutudanganya na uongo mwingine then tunaipa kura tena? Kwanini tusiwabadilishe? So hali hii ngumu ipo sana nchini infact itaongezeka maana wajinga wataongoza sana hii nchi sioni dalili zozote za watanzania kuelewa nguvu waliyonayo ya kuibadili hii nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom