Upo sahihi kwa kiwango kikubwa ila katika ufaulu wa haya masomo ya dini ikiwa wanafunzi wa dini ya walalamishi hata wote wapate A na B halafu wale wanafunzi wa dini ya wasio walalamishi wapate wote D na F sidhani kama kutakuwa na tatizo sana ukifananisha na ikitokea kinyume chake. Ufike wakati serikali ijitoe katika hizi lawama zisizo na ulazima na iache haya masomo ya dini yafundishwe huko huko kwenye nyumba za ibada za imani husika, kwa kufanya hivyo utegemezi na kulia lia serikalini kutapungua kwa kiasi kikubwa maana sasa hivi imefikia imani nyingine kila kitu wanataka serikali iwafanyie, watataka hata watoto wao nyumbani walelewe na serikali halafu wenyewe washinde kucheza bao na kunywa kahawa vijiweni. Kama kila kitu ni haki yao kudai serikali iwasaidie, wawapeleke na wake zao serikalini ili serikali iwasaidie yale mambo, tena akina Mwigulu na Malima watafurahi sana lol!!Binafsi naunga mkono tupeane mitihani ya kidini misikitini, kanisani,nk hii haitakuwa na kelele hata zikiwepo zitaishia huko huko misikitini na makanisani..maana lililopo sasa waislamu wakiangilia matokeo ya bible knowledge wakaona A,B za kumwaga wakaangalia islamic wakaona C,D,F au kinyume chake wakristo waone bible knowledge ni C,D,F wakati islamic A,B kuna anza kuwa na mawazo kwamba wenzetu wanabebwa,bila kujali kwamba waliosahihisha ni imani moja nao au la na bila kujali mtihani ulikuwaje..