Hashimu lwenje
JF-Expert Member
- Oct 2, 2017
- 415
- 359
Mafuta na gesi ni nishati muhimu sana hapa duniani. Nchi zilizo endelea zina tafuta usiku na mchana mafuta na gesi, ili ziweze kujitegemea na kuwa na utoshelevu wa mafuta na gesi. Wenyewe tumeshuhudia Nchi hizi zikiwekeza matilioni na matilioni ya pesa katika kutafuta na kuzalisha mafuta na gesi. Lengo la hizi nchi ni ili zijitegemee katika mafuta na gesi.
Leo hii ukienda Malaysia na Indonesia wao wanajitahidi hata kubadili mafuta ya michikichi kuwa diseli lengo lao ni ili nao wajitegemee katika nishati hii.
Wenzetu south africa nao wanakimbia mbele, wao walipo gundua kuwa mafuta na gesi ni muhimu, waliamua kujiingiza tangu miaka ya 1950 kwenye mradi wa kubadili makaa mawe kuwa mafuta na gesi (rejea SASOL COAL TO LIQUIDS TECHNOLOGY)
Lakini pia Qatar nchi yenye hifadhi kubwa ya gesi asilia, ilipo gundua kuwa mafuta ni muhimu zaidi kuliko gesi, iliamua nayo kuanzisha mradi wa kubadili gesi asilia kuwa mafuta (rejea QATAR GAS TO LIQUIDS TECHNOLOGY)
Si hivyo tu wenzetu Malaysia na Indonesia hivi sasa nao wanabadili mafuta ya michichiki kuwa diesel (rejea Palm oil to diesel Technology). Hawa wote wanacho kitafuta ni kupunguza utegemezi wa mafuta na gesi kutoka nchi zingine.
Mwalimu Nyerere alitujengea kiwanda cha kusafisha mafuta (TIPPER) lakini tulikiua tena kwa makusudi, mitambo yote ilisha kufa na kuoza imebaki tu sehemu ya kuhifazia mafuta. Na niseme ukweli hicho kiwanda kingekuwepo tungekua tuko mbali sana katika teknolojia ya mafuta na gesi. Ni lini tuta kirudisha tena kiwanda hicho. TIPPER yetu ilikua inasafisha mafuta ghafi (crude oil) na kutupatia petroli, diesel, mafuta ya taa, gesi ya kupikia (LPG), vilainishi vya magari (lubrucants and grease) pamoja na lami). Leo hii tunaagiza kila kitu nje ya nchi hili swala sio zuri. Zipo faida nyingi sana tutakazo zipata tukijitegemea katika nishati ya mafuta na gesi. Leo hii thamani ya pesa yetu ikishuka hapo lazima bei ya mafuta na gesi ndani ya nchi yetu itapanda. Tutauza kwa bei kubwa ili tuweze kufidia ile currency conversion rate na ili tupate faida kwasababu tunaenda kununua mafuta nchi za nje kwa dolla. Lakini tungekua na mafuta yetu wenyewe, wala kushuka kwa thamani ya shilingi kusinge asili bei ya mafuta ndani ya nchi yetu.
Sasa basi ni lini tutajitegemea na kutumia mafuta na gesi ya kwetu wenyewe? Hatuwezi kufikia huko bila kuwa na wataalam walio fundishwa na kuiva kivitendo. Taaluma ya mafuta na gesi ni taaluma ambayo huwez linganisha na taaluma nyingine yeyote hapa duniani, jaribu kufikiri mtu anaenda kutafuta mafuta na gesi baharini, panahitaji maarifa na, ujuzi wa hali ya juu. Sasa huo ujuzi wataupatia wapi, mmewasomesha sawa lakini mmewaacha mtaani wataalam wa mafuta na gesi. Alafu mkitangaza kazi mnataka (uzoefu) experience ya miaka sita (rejea NAFASI ZA KAZI EWURA). Vijana wengine wameenda kusoma CHINA, UK lakini wapo tu mtaani hawana la kufanya. Vijana waliosomea UDSM na UDOM nao wapo tu mtaani wanafanya kazi za kuuza madawa ya famasi kwa wahindi, wengine wanafanya kazi za uhasibu, wengine wanafanya kazi kwenye viwanda vya soda. Lakini niweke tu wazi taaluma ya mafuta na gesi inahitaji maarifa na ujuzi wa hali ya juu ili iweze kutumika kivitendo katika mazingira. Huwezi tafuta uzoefu wa kuchimba gesi baharini au kuchakata gesi kwenye kiwanda cha kutengeneza nguo, rangi au soda hapo unaua taaluma.
Serikali tunawaombeni wasaidieni wataalam wa mafuta na gesi, wapate ujuzi.
Mafuta na gesi vina umhimu mkubwa katika jamii yetu,
moja mafuta yanatumika kuendeshea magari, mashine, ndege na treni.
Lakini pia mafuta yanatumika kama vilainishi kwenye sehemu za injini za magari, ndege, treni na mitambo ili kuzuia msuguano.
Mafuta yanatumika kuzalishia mbolea mbalimbali (rejea NAPTHA TO FERTILIZER TECHNOLOGY). Hivi sisi tangu kipindi cha ukoloni mpaka leo tunaagiza mbolea kutoka nje ya nchi, tujitahidi, kwakweli kwendana na wakati, dhama hizi sio za utegemezi.
Mafuta yanatumika kutengenezea lami (Bitumen)
Lakini pia mafuta yanatumika kutengezea kemikali (petrochemicals),
Gesi inatukima kutengnezea mbolea, plastics zote unazo zijua, matairi ya magari, pikipiki na matrekita, na chemikali mbalimbali (petrochemicals).
Gesi ni nishati nzuri sana kwa kupikia,
Nawaombeni viongozi wetu tusiwatupe hawa wataalam wa mafuta na gesi, badala yake tuwatafute tuwakusanye tuwaendeleze katika fani yao hiyo hiyo, nchi yetu hii itafika mbali sana kwani mafuta na gesi ni chachu kubwa ya maendeleo ya taifa lolote duniani, kwani bila mafuta na gesi hakuna usafiri duniani, bila mafuta na gesi hakuna bidha za plastiki duniani, bila mafuta na gesi hakuna mbolea bora, bila mafuta na gesi hakuna gesi kwaajili ya kupikia. Kweli hata gesi ya kupikia tunaagiza nje ya nchi?
Nakuacha na swali la kujiuliza,
Wewe unahisi nini kitatokea endapo kama mafuta na gesi na makaa ya mawe vikaisha ghafura hapa duniani?
Mwingine atanijibu kuwa kuna nishati mbadala kama jua, upepo, nyukilia n.k
Na mimi namwuuliza VILAINSHI VYA INJINI NA MITAMBO TUTAVIPATA WAPI?
PLASTIK TUTAZIPATA WAPI?
Ahsanteni sana
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ifanikishe.