Serikali ya Tanzania likumbukeni na hili?

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
415
359
Mafuta na gesi ni nishati muhimu sana hapa duniani. Nchi zilizo endelea zina tafuta usiku na mchana mafuta na gesi, ili ziweze kujitegemea na kuwa na utoshelevu wa mafuta na gesi. Wenyewe tumeshuhudia Nchi hizi zikiwekeza matilioni na matilioni ya pesa katika kutafuta na kuzalisha mafuta na gesi. Lengo la hizi nchi ni ili zijitegemee katika mafuta na gesi.

Leo hii ukienda Malaysia na Indonesia wao wanajitahidi hata kubadili mafuta ya michikichi kuwa diseli lengo lao ni ili nao wajitegemee katika nishati hii.

Wenzetu south africa nao wanakimbia mbele, wao walipo gundua kuwa mafuta na gesi ni muhimu, waliamua kujiingiza tangu miaka ya 1950 kwenye mradi wa kubadili makaa mawe kuwa mafuta na gesi (rejea SASOL COAL TO LIQUIDS TECHNOLOGY)

Lakini pia Qatar nchi yenye hifadhi kubwa ya gesi asilia, ilipo gundua kuwa mafuta ni muhimu zaidi kuliko gesi, iliamua nayo kuanzisha mradi wa kubadili gesi asilia kuwa mafuta (rejea QATAR GAS TO LIQUIDS TECHNOLOGY)

Si hivyo tu wenzetu Malaysia na Indonesia hivi sasa nao wanabadili mafuta ya michichiki kuwa diesel (rejea Palm oil to diesel Technology). Hawa wote wanacho kitafuta ni kupunguza utegemezi wa mafuta na gesi kutoka nchi zingine.

Mwalimu Nyerere alitujengea kiwanda cha kusafisha mafuta (TIPPER) lakini tulikiua tena kwa makusudi, mitambo yote ilisha kufa na kuoza imebaki tu sehemu ya kuhifazia mafuta. Na niseme ukweli hicho kiwanda kingekuwepo tungekua tuko mbali sana katika teknolojia ya mafuta na gesi. Ni lini tuta kirudisha tena kiwanda hicho. TIPPER yetu ilikua inasafisha mafuta ghafi (crude oil) na kutupatia petroli, diesel, mafuta ya taa, gesi ya kupikia (LPG), vilainishi vya magari (lubrucants and grease) pamoja na lami). Leo hii tunaagiza kila kitu nje ya nchi hili swala sio zuri. Zipo faida nyingi sana tutakazo zipata tukijitegemea katika nishati ya mafuta na gesi. Leo hii thamani ya pesa yetu ikishuka hapo lazima bei ya mafuta na gesi ndani ya nchi yetu itapanda. Tutauza kwa bei kubwa ili tuweze kufidia ile currency conversion rate na ili tupate faida kwasababu tunaenda kununua mafuta nchi za nje kwa dolla. Lakini tungekua na mafuta yetu wenyewe, wala kushuka kwa thamani ya shilingi kusinge asili bei ya mafuta ndani ya nchi yetu.

Sasa basi ni lini tutajitegemea na kutumia mafuta na gesi ya kwetu wenyewe? Hatuwezi kufikia huko bila kuwa na wataalam walio fundishwa na kuiva kivitendo. Taaluma ya mafuta na gesi ni taaluma ambayo huwez linganisha na taaluma nyingine yeyote hapa duniani, jaribu kufikiri mtu anaenda kutafuta mafuta na gesi baharini, panahitaji maarifa na, ujuzi wa hali ya juu. Sasa huo ujuzi wataupatia wapi, mmewasomesha sawa lakini mmewaacha mtaani wataalam wa mafuta na gesi. Alafu mkitangaza kazi mnataka (uzoefu) experience ya miaka sita (rejea NAFASI ZA KAZI EWURA). Vijana wengine wameenda kusoma CHINA, UK lakini wapo tu mtaani hawana la kufanya. Vijana waliosomea UDSM na UDOM nao wapo tu mtaani wanafanya kazi za kuuza madawa ya famasi kwa wahindi, wengine wanafanya kazi za uhasibu, wengine wanafanya kazi kwenye viwanda vya soda. Lakini niweke tu wazi taaluma ya mafuta na gesi inahitaji maarifa na ujuzi wa hali ya juu ili iweze kutumika kivitendo katika mazingira. Huwezi tafuta uzoefu wa kuchimba gesi baharini au kuchakata gesi kwenye kiwanda cha kutengeneza nguo, rangi au soda hapo unaua taaluma.
Serikali tunawaombeni wasaidieni wataalam wa mafuta na gesi, wapate ujuzi.

Mafuta na gesi vina umhimu mkubwa katika jamii yetu,

moja mafuta yanatumika kuendeshea magari, mashine, ndege na treni.

Lakini pia mafuta yanatumika kama vilainishi kwenye sehemu za injini za magari, ndege, treni na mitambo ili kuzuia msuguano.

Mafuta yanatumika kuzalishia mbolea mbalimbali (rejea NAPTHA TO FERTILIZER TECHNOLOGY). Hivi sisi tangu kipindi cha ukoloni mpaka leo tunaagiza mbolea kutoka nje ya nchi, tujitahidi, kwakweli kwendana na wakati, dhama hizi sio za utegemezi.

Mafuta yanatumika kutengenezea lami (Bitumen)

Lakini pia mafuta yanatumika kutengezea kemikali (petrochemicals),

Gesi inatukima kutengnezea mbolea, plastics zote unazo zijua, matairi ya magari, pikipiki na matrekita, na chemikali mbalimbali (petrochemicals).

Gesi ni nishati nzuri sana kwa kupikia,

Nawaombeni viongozi wetu tusiwatupe hawa wataalam wa mafuta na gesi, badala yake tuwatafute tuwakusanye tuwaendeleze katika fani yao hiyo hiyo, nchi yetu hii itafika mbali sana kwani mafuta na gesi ni chachu kubwa ya maendeleo ya taifa lolote duniani, kwani bila mafuta na gesi hakuna usafiri duniani, bila mafuta na gesi hakuna bidha za plastiki duniani, bila mafuta na gesi hakuna mbolea bora, bila mafuta na gesi hakuna gesi kwaajili ya kupikia. Kweli hata gesi ya kupikia tunaagiza nje ya nchi?

Nakuacha na swali la kujiuliza,
Wewe unahisi nini kitatokea endapo kama mafuta na gesi na makaa ya mawe vikaisha ghafura hapa duniani?

Mwingine atanijibu kuwa kuna nishati mbadala kama jua, upepo, nyukilia n.k

Na mimi namwuuliza VILAINSHI VYA INJINI NA MITAMBO TUTAVIPATA WAPI?
PLASTIK TUTAZIPATA WAPI?

Ahsanteni sana
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ifanikishe.
 
Haviwezi kuisha maana vinakaribuni miaka 2000 vi natumika

Na kama vikiisha dunia itakuwa imeaamia kwenye matumizi mingine
 
Mafuta na gesi ni jambo linalotakiwa kupewa nafasi kubwa kwa manufaa ya sasa na baadae!

Mafuta na gesi ni rasilimali inayoweza kuinua pato la taifa kwa hali ya juu sana, kwa bahati nzuri hapa Tanzania kuna maeneo mengi yenye uwezekano wa kuwa na mafuta ( petroleum deposits) hasa maeneo ya mwambao wa pwani ya bahari ya hindi na morogoro.

Nashangaa sana kwanini msisitizo wa serikali yetu kwenye utafiti wa mafuta umepungua sana, au ni kweli sekta ya gesi na petroleum ilishauzwa kwa kuwekwa bond kipindi cha mzee jk? hata Magufuli na ubabe wake hagusi huko, kwanini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usichokijua mleta uzi kwa sasa tuna mambo mengi mno tunayoyafanya kiasi cha kusahau hata mengine ya msingi kama hilo la mafuta na gesi .

Labda nikuweke wazi tu kuwa sasa tumejikita zaidi kwenye sekta ya udukuz wa mawasiliano ili tuweze kupambana na mawakala wa mabeberu mnaotukwamisha kuelekea kwenye Tanzania ya kijani na njano
 
Sasa wewe pamoja na ng'ombe wako kama unatengeneza kiatu kwa gharama ya laki 1 na kiatu cha mchina kinafika sokoni kwa sh 25,000 nani ataangaika na hilo likiatu lako lisilo na shepu, Sori ya mugambo! viwanda vingi vimekufa kwa sababu hiyo.
 
Chief umeandika mengi na ya msingi lakn kubwa ni KILIO CHA AJIRA KWA WAHITIMU FANI TAJWA HAPO JUU kwa serikal hii ya chichiem sahau kabisa nikikumbuka enz za mzee wa msoga tulivyoaminishwa kuwa hakutakuwa na tatzo LA umeme kwan mkomboz GESI toka NTWARA maajabu awamu hii tunaambiwa gesi imeshikwa na mabeberu n hao hao waliokuwa mawaziri wabunge na watendaji wakuu serikalin ndio waliopitisha uji ga huo kuwapa hao mabeberu najiuliza cjui mabeberu waliingia bungen na MTUTU kuwashurutisha waheshimiwa wasaini huo mkataba hata hii STIGGLER'S baada ya miaka 8 ijayo tutaambiwa tayar mabeberu wamejimilikisha. Swali langu HV hawa mabeberu ni watu au hawa mbuzi dume tunawafuga huku mallee I SONGEA vijjn maana sielewi kabisa tafsir ya beberu wajuz nijuzeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuacha na swali la kujiuliza,
Wewe unahisi nini kitatokea endapo kama mafuta na gesi na makaa ya mawe vikaisha ghafura hapa duniani?

Nimekusoma mkuu.

Sijui ni nini hasa kinachokupa msukumo mkubwa wa kuviona mafuta na gesi kuwa muhimu zaidi kuliko mengineyo. Pengine wewe bado unatazama umuhimu wa muda mfupi, miaka miwili hadi mitano ijayo; na hata muda wa kati, labda miaka saba hadi kumi hivi ijayo. Muono wako huu haukukupa fikra za kuangalia nje ya boksi na kuona fursa nyingine zinazojitokeza kwa kasi sasa.

Ya nini ukahangaike na kutengeneza diesel wakati unalo jua mwaka mzima, na upepo unaovuma kila siku.
Hukukumbuka kabisa juhudi kubwa zinazofanywa katika teknologia za 'energy storage'. ili hata wakati jua haliwaki pawe na njia ya kuiweka stoo nguvu iliyokusanywa wakati jua lilipokuwa likiwaka ili itumike wakati halipo. Hivyo hivyo na upepo. Pawe na betri za kuweka nguvu hiyo itumike inapohitajika.

Pamoja na kukubaliana nawe katika umuhimu wa vyanzo hivyo vya nguvu, lakini mimi nisingevipa kipaumbele kwa sasa. Ningewawezesha vijana pale Chuo kikuu wabobee kikwelikweli katika ujuzi wa teknolojia hii mpya inayoibukia sasa hivi katika kutumia re-newable energy sources na jinsi ya kuistore.
Tesla na wengine tayari wanayo magari yasiyohitaji petroli na diesel. Ni kiasi cha muda tu - miaka michache ijayo hii ndio itakuwa njia kuu ya kupata mahitaji ya 'energy sources' kuendesha shughuli nyingi za kiuchumi wa nchi nyingi..
 
Mafuta na gesi ni nishati muhimu sana hapa duniani. Nchi zilizo endelea zina tafuta usiku na mchana mafuta na gesi, ili ziweze kujitegemea na kuwa na utoshelevu wa mafuta na gesi. Wenyewe tumeshuhudia Nchi hizi zikiwekeza matilioni na matilioni ya pesa katika kutafuta na kuzalisha mafuta na gesi. Lengo la hizi nchi ni ili zijitegemee katika mafuta na gesi.

Leo hii ukienda Malaysia na Indonesia wao wanajitahidi hata kubadili mafuta ya michikichi kuwa diseli lengo lao ni ili nao wajitegemee katika nishati hii.

Wenzetu south africa nao wanakimbia mbele, wao walipo gundua kuwa mafuta na gesi ni muhimu, waliamua kujiingiza tangu miaka ya 1950 kwenye mradi wa kubadili makaa mawe kuwa mafuta na gesi (rejea SASOL COAL TO LIQUIDS TECHNOLOGY)

Lakini pia Qatar nchi yenye hifadhi kubwa ya gesi asilia, ilipo gundua kuwa mafuta ni muhimu zaidi kuliko gesi, iliamua nayo kuanzisha mradi wa kubadili gesi asilia kuwa mafuta (rejea QATAR GAS TO LIQUIDS TECHNOLOGY)

Si hivyo tu wenzetu Malaysia na Indonesia hivi sasa nao wanabadili mafuta ya michichiki kuwa diesel (rejea Palm oil to diesel Technology). Hawa wote wanacho kitafuta ni kupunguza utegemezi wa mafuta na gesi kutoka nchi zingine.

Mwalimu Nyerere alitujengea kiwanda cha kusafisha mafuta (TIPPER) lakini tulikiua tena kwa makusudi, mitambo yote ilisha kufa na kuoza imebaki tu sehemu ya kuhifazia mafuta. Na niseme ukweli hicho kiwanda kingekuwepo tungekua tuko mbali sana katika teknolojia ya mafuta na gesi. Ni lini tuta kirudisha tena kiwanda hicho. TIPPER yetu ilikua inasafisha mafuta ghafi (crude oil) na kutupatia petroli, diesel, mafuta ya taa, gesi ya kupikia (LPG), vilainishi vya magari (lubrucants and grease) pamoja na lami). Leo hii tunaagiza kila kitu nje ya nchi hili swala sio zuri. Zipo faida nyingi sana tutakazo zipata tukijitegemea katika nishati ya mafuta na gesi. Leo hii thamani ya pesa yetu ikishuka hapo lazima bei ya mafuta na gesi ndani ya nchi yetu itapanda. Tutauza kwa bei kubwa ili tuweze kufidia ile currency conversion rate na ili tupate faida kwasababu tunaenda kununua mafuta nchi za nje kwa dolla. Lakini tungekua na mafuta yetu wenyewe, wala kushuka kwa thamani ya shilingi kusinge asili bei ya mafuta ndani ya nchi yetu.

Sasa basi ni lini tutajitegemea na kutumia mafuta na gesi ya kwetu wenyewe? Hatuwezi kufikia huko bila kuwa na wataalam walio fundishwa na kuiva kivitendo. Taaluma ya mafuta na gesi ni taaluma ambayo huwez linganisha na taaluma nyingine yeyote hapa duniani, jaribu kufikiri mtu anaenda kutafuta mafuta na gesi baharini, panahitaji maarifa na, ujuzi wa hali ya juu. Sasa huo ujuzi wataupatia wapi, mmewasomesha sawa lakini mmewaacha mtaani wataalam wa mafuta na gesi. Alafu mkitangaza kazi mnataka (uzoefu) experience ya miaka sita (rejea NAFASI ZA KAZI EWURA). Vijana wengine wameenda kusoma CHINA, UK lakini wapo tu mtaani hawana la kufanya. Vijana waliosomea UDSM na UDOM nao wapo tu mtaani wanafanya kazi za kuuza madawa ya famasi kwa wahindi, wengine wanafanya kazi za uhasibu, wengine wanafanya kazi kwenye viwanda vya soda. Lakini niweke tu wazi taaluma ya mafuta na gesi inahitaji maarifa na ujuzi wa hali ya juu ili iweze kutumika kivitendo katika mazingira. Huwezi tafuta uzoefu wa kuchimba gesi baharini au kuchakata gesi kwenye kiwanda cha kutengeneza nguo, rangi au soda hapo unaua taaluma.
Serikali tunawaombeni wasaidieni wataalam wa mafuta na gesi, wapate ujuzi.

Mafuta na gesi vina umhimu mkubwa katika jamii yetu,

moja mafuta yanatumika kuendeshea magari, mashine, ndege na treni.

Lakini pia mafuta yanatumika kama vilainishi kwenye sehemu za injini za magari, ndege, treni na mitambo ili kuzuia msuguano.

Mafuta yanatumika kuzalishia mbolea mbalimbali (rejea NAPTHA TO FERTILIZER TECHNOLOGY). Hivi sisi tangu kipindi cha ukoloni mpaka leo tunaagiza mbolea kutoka nje ya nchi, tujitahidi, kwakweli kwendana na wakati, dhama hizi sio za utegemezi.

Mafuta yanatumika kutengenezea lami (Bitumen)

Lakini pia mafuta yanatumika kutengezea kemikali (petrochemicals),

Gesi inatukima kutengnezea mbolea, plastics zote unazo zijua, matairi ya magari, pikipiki na matrekita, na chemikali mbalimbali (petrochemicals).

Gesi ni nishati nzuri sana kwa kupikia,

Nawaombeni viongozi wetu tusiwatupe hawa wataalam wa mafuta na gesi, badala yake tuwatafute tuwakusanye tuwaendeleze katika fani yao hiyo hiyo, nchi yetu hii itafika mbali sana kwani mafuta na gesi ni chachu kubwa ya maendeleo ya taifa lolote duniani, kwani bila mafuta na gesi hakuna usafiri duniani, bila mafuta na gesi hakuna bidha za plastiki duniani, bila mafuta na gesi hakuna mbolea bora, bila mafuta na gesi hakuna gesi kwaajili ya kupikia. Kweli hata gesi ya kupikia tunaagiza nje ya nchi?

Nakuacha na swali la kujiuliza,
Wewe unahisi nini kitatokea endapo kama mafuta na gesi na makaa ya mawe vikaisha ghafura hapa duniani?

Mwingine atanijibu kuwa kuna nishati mbadala kama jua, upepo, nyukilia n.k

Na mimi namwuuliza VILAINSHI VYA INJINI NA MITAMBO TUTAVIPATA WAPI?
PLASTIK TUTAZIPATA WAPI?

Ahsanteni sana
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ifanikishe.

Mleta mada na wanabodi,
Hii mada ni nzuri ila ina mambo mengi ya kuchangia. Nitachangia moja la elimu na uzoefu katika sekta ya mafuta na gesi. Nakushukuru mtoa mada kwa kutujulisha kumbe kuna vijana wengi wamesomea fani hii huko nje ila wako mitaaani hawana kazi au wanafanya kazi zisizoendana na fani walizosomea na hadhi yake. Hili linatokana na sababu nyingi zitokanazo na utekelezaji wa sera zetu mbali mbali za nchi yetu. Mbali na elimu ni kweli fani hii inahitaji uzoefu. Hii ni kwenye Upstream na Down Stream. Up Stream ni katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na Down Stream ni uuzaji na usambazaji wa mafuta, gesi na bidhaa zitokanazo na mafuta na gesi. Elimu na uzoefu vinahitajika katika maeneo yote hayo mawili. Tatizo linaloikumba nchi yetu ni kwa baadhi ya taasisi kutokuthubutu kwa maksudi kabisa kuthamini michango ya watanzania katika kujitafutia maendeleo mmoja mmoja na au kwa makundi kwa watanzania WAZAWA. Najua hili litawakwaza wengi lakini ndiyo ukweli. Narudia. Kama taifa lazima tulenge kuthubutu ku-support WAZAWA potelea mbali nikieleweka vibaya. Ukishajua umuhimu wa hili na kulikubali utakuwa umepiga hatua moja muhimu ya kuelekea kwenye kuwasaidia watu wako kushiriki katika kujiletea maendeleo wao wenyewe. Hii ni pamoja na ajira na kujiajiri. Serikali na taasisi zake inatakiwa kuweka miundo mbinu imara na kuendelea kuiboresha kwa kadri ya matakwa ya uchumi na biashara ya leo ili watanzania waweze kuthubutu kujiletea maendeleo wao wenyewe na familia zao. Kama hili likitiliwa mkazo utakuta kuna makampuni ya WAZAWA mengi na biashara zao nyingi zinasubiri kuwaajiri vijana kama hao katika mnyororo mrefu wa Up Stream and Down Stream Petroleum Business in our country. Hapa watapata uzoefu na kupiga hatua moja mbali ya kujiletea maendeleo wao, familia zao na career development zao.

National Economic Empowerment Council must take lead in this and other developmental agendas badala ya kusubiri kuendeleza walima nyanya na vitunguu kule Iringa na kwingineko. Serikali ya sasa inathubutu. Tunaona. Wabeja sana. Mapungufu lazima yawepo ili tuweze kujirekebisha tuweze tusonge mbele, siyo? Je taasisi zake zinai-support vipi? Hilo inaliona? Inachukua hatua za haraka? Ukianza kuingiza siasa kwenye udhaifu wa wazi kwenye jambo kubwa kama hili nchi lazima ipata shida kidogo.
Kwenye Down Stream business EWURA ina support vipi WAZAWA? Mbona masharti ya kusajiri kampuni ya kuagiza, kusambaza na kuuza mafuta na bidhaa zitokanazo na mafuta zinafanana kwa WAZAWA na wasio WAZAWA? Je wanajua kwamba possibility ni kubwa kwa WAZAWA kuwekeza tena faida itakayopatikana kwenye hii biashara badala ya asiye MZAWA ambaye possibility ni kubwa kwamba ataipeleka na kuwekeza kwao au nchi nyingine? Na ajira je? MZAWA ataajiri wazungumza Kiswahili wengi kwa sababu wanaelewana lakini asiye MZAWA atafanya hivyo??!! Najua matakwa ya TIC kwenye ajira za wageni. Haya kweli hayakufundishwa shuleni kiasi kwamba EWURA hawayajui? Sasa tunawafundisha maana elimu haina mwisho, siyo.
 
Back
Top Bottom