Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Serikali ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD) imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani wa euro milioni 50 hadi milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini
Hayo yamesemwa na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Malika Berak, Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa katika uandaaji wa kongamano la uwekezaji litakalofanyika jijini Dar es salaam mwezi Aprili mwaka huu
Berak amesema mkopo huo utaiwezesha na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi wa mazingira na miradi ya umeme
Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Serikali ya Ufaransa kupitia kwa balozi wake hapa nchini kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano dhidi ya umaskini nchini
Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa nchini kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote mbili za Tanzania na Ufaransa
Makamu wa Rais amemweleza Balozi wa Ufaransa hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yoyote katika kuandaa kongamano hilo amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua kusaidia mchakato huo kutokana na umuhimu wa kongamano hilo hasa wakati huu ambapo Tanzania inataka kujenga uchumi wa viwanda.