Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali

kuna kaugonjwa ka kukIla umakini kwenye uandikaji wa barua au taarifa za serekali, as epitomized by zile za Msigwa wa ikulu ambazo zinakuwa na so many silly mistakes.

hata hii nayo ni hivyo hivyo... kama huja notice at least one shortcoming kwenye hii barua basi nawe ni wale wale tu!
Unapotaka mtu ajifunze mweleze una kasoro hii au ile sasa unamkosoa bila kumweleza kwa uwazi akajua tatizo nawe pia unakuwa walewale.
 
Mimi nimefanya kazi kampuni binafsi ambapo tulikuwa tunaingia kazini saa 8:30 asubuhi na kutoka saa 11:30 jioni.

Kabla ya 8:30 asubuhi, mitandao yote inapatikana kwenye internet ya ofisini. Ikifika muda wa kazi, hizo social media kama facebook, blogs na vitu visivyoendana na kazi hazifunguki tena mpaka saa 11:30.

Ukitaka kutumia either wahi asubuhi au chelewa kutoka jioni, laa sivyo tumia bundle lako la simu ila piga kazi. Wakiona kutwa unashinda unachezea simu lazima wakuhoji unafanya nini.

Ukibisha sana kujifanya mjanja, mtajuana kwenye review ya kuongezewa mshahara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili linawezekana ila ni gumu

1. Watu wanaweza kuunplug hizo RJ 45 kwenye computer zao badala yake wakatumia simu zao kwa kufanya tethering( Simu inaweza kutumika kama Modem) watu wakaingia kwenye Internet kama kawaida

2.. Kimsingi ni wazo zuri lakini kulitekeleza kutahitaji mambo mengi sana , kwanza gharama ya tools za kuenforce hiyo policy (routers, firewalls etc) ni expensive kuziinstall nchi nzima.

3. Kanuni kali za discipline maofisini ukikutwa unatumia mitandao husika mida ya kazi (lakini hili litaleta mgawanyiko maana huwezi kupita unachunguza chunguza computer za watu hususan mabosi) .

4. labda waweke policy ya mtu kutokuingia na smartphone muda wa kazi, na badala yake waingie na simu za torch, lakini hii nayo ni ngumu maana kuna torch nyingine nazo zinaaccess internet
 
Kwa watumishi wa ACACIA naamini huu uzi mmeuelewa. Huwa si rahisi kutumia mtandao wa kampuni ku access vitu vingine visivyokuwa vya kikazi! Na hii huwafanya watu kuwa busy full time! kama ukitaka ku-access mitandao ya kijamii basi inabidi utumie smart phone yako (kama unayo ruhusa ya kuwa na simu kazini). Kwa maana nyingine hili silo jambo geni!
 
Wanaolinganisha makampuni ya watu binafsi na serikali kwenye hili suala wanashindwa kuelewa kuwa Makampuni ni entity limited in scope. Wanaweza kuspend kiasi cha hela kuwezesha hilo wakaafford. Lakini Serikali ambayo ina maofisi kila kona ya nchi watainvest shilingi ngapi kwenye software na hardware kulifanikisha hilo?

Kuzuia siyo ishu, Ishu ni kuinvest mpunga wa kutosha kufanikisha hilo! JE BAJETI IPO?
 
Hoja yangu ni wewe kusema uko na serikali, wewe ni nani mpaka ujifanye uko na serikali ?.
Wewe ni mkenya?

Tz ukisema upo na kitu unamaanisha unakubaliana na kitu husika.

Hivyo nakubaliana na uamuzi wa kumtaka mtumishi asitumie mtandao na vifaa vya serikali kusurf vitu binafsi muda wa kazi.
 
JF kuna members mnapenda kupotosha sana, me nilivyoelewa usitumie internent ya Serikali kwa matumizi yako hasa hayo ya social Networks.
 
kwa madai:

"yanaathiri kasi ya mtandao wa intaneti ya serikali."

hiyo ndio sababu muhimu wameiona hadi kuzuia hiyo tabia makazini!!!!.....kazi kweli kweli.
Mkuu kama umewahi kusimamia mtandao kwenye kampuni au shirika lolote utawaelewa sana hawa serikali.
Nipo sekta binafsi kuna kipindi inatulazimu kuzuia youtube na facebook, kwenye firewall ili kazi flani ziende.

Unakuta mwingine kageuza Tv kabisa anasikiliza Gospel, mwingine bongo flava, mwingine shilawadu, mwingine Zari na mabeto, alafu kuna mwingine unataka kutuma file muhimu kwa email kama attachment, Au unafanya backup muhimu online lakini inachukua masaa au inafail kabisa.
Watu wanakula bandwidth yote na kusababisha resource contention ya hali ya juu.

Tatizo lingine ni matumizi mabaya ya muda.
 
Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali wakati wa kazi, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.

Inaonekana serikali haijatambua 80% ya biashara za kisasa zinafanyikia mtandaoni,huko insta na facebook watu wanamobile electronic shops.

Wameshazoea kudraw pesa za mshahara kila mwisho wa mwezi wamesahau kuna vingine vinavyowapa wenzao kula kama biashara kupitia mitandao.

Wanadhani mitandao ni sehemu ya kutafutia mademu na kujionyesha La hasha hizi ni ofisi kama zilivyo zakwao.

Kama ukiweza kumanage biashara kiganjani kwako wewe ni bora kuliko mwenye fremu kibao anaeka kusubiri wanaopita.

Mimi nadhani ni muda wa serikali kutambua mitandao ya kijamii ni ofisi za watu.

Kama wanataka kufungia wadisconnect network katika majengo yao ya serikali tu.
View attachment 849176View attachment 849175View attachment 849174View attachment 849173

======

Serikali ya Tanzania imezuia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma wakati wa kazi kwa madai yanaathiri kasi ya mtandao wa intaneti ya Serikali.

Pia, imedai watumishi wengi wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kutekeleza majukumu yao.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro kwa taasisi zote za umma, imeonya juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ya Serikali na kwamba, hatua hiyo imelenga kudhibiti matumizi ya mitandao.

“Kasi ya mtandao wa Serikali inapungua kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii hususan inayopakua video, mfano “YouTube” na hivyo kusababisha watumishi wengine wanaotumia mtandao wa intaneti wa Serikali katika kutekeleza majukumu yao kuathirika,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Aidha, taarifa hiyo inaeleza juu ya upakuaji wa nyaraka zenye hatimiliki bila idhini ya wamiliki kwa kutumia Intaneti ya Serikali kinyume na utaratibu.

“Mitandao ya kijamii haitapatikana kwenye intaneti ya Serikali wakati wa muda wa kazi kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri,” inaeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, Menejimenti ya Utumishi imezitaka taasisi zenye mahitaji maalumu ya matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa saa za kazi, kuwasilisha maombi yao kwa katibu mkuu wa utumishi yakiambatana na sababu za maombi hayo.

“Watumishi wa umma hawataweza kupakua nyaraka, picha na video zenye hatimiliki kwenye intaneti ya Serikali bila idhini ya wamiliki.”

Kwa mara kadhaa, Serikali imekuwa ikitoa miongozo ya matumizi ya Tehama kwa taasisi za Serikali ikiwamo kukataza matumizi ya mitandao kupitia intaneti ya Serikali saa za kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii tulishazuilwa Tayari ilibakia kutangaziwa tu kwenu Raia... Ni Social Media pekee vingine vinapatikana kawa Kawa...
 
Mkuu kama umewahi kusimamia mtandao kwenye kampuni au shirika lolote utawaelewa sana hawa serikali.
Nipo sekta binafsi kuna kipindi inatulazimu kuzuia youtube na facebook, kwenye firewall ili kazi flani ziende.

Unakuta mwingine kageuza Tv kabisa anasikiliza Gospel, mwingine bongo flava, mwingine shilawadu, mwingine Zari na mabeto, alafu kuna mwingine unataka kutuma file muhimu kwa email kama attachment, Au unafanya backup muhimu online lakini inachukua masaa au inafail kabisa.
Watu wanakula bandwidth yote na kusababisha resource contention ya hali ya juu.

Tatizo lingine ni matumizi mabaya ya muda.
sawa sijakataa, nakubaliana na wewe chief,
nashangaa ni kwanini waseme inaathiri kasi ya intaneti ya ofisi....inamaana isingekuwa inaathili kasi ya intaneti hao watumishi wanaruhusiwa kuingia kwenye mitandao ya kijamii wakati wa kazi?
 
hawauwezi mziki wa internet watafungia mitandao ipi maana kuna mitandao mingine watu hawajawahi kuiskia majina ipo kabla ya hata fb na insta kuanzishwa. so ukifungia huu tunahamia kwingine
 
Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana, unalalamikia uruhusiwe kutumia Internet ya serikali bure, tena wakati wa kazi, kuperuzi insta, fb, what'sapp, twita, jf, nk? Hivi huyo aliyeturoga ni nani?
Nyie watu wengine mnauzi sana. Wakati wa kazi, fanya kazi; wakati wa break peruzi hiyo mitandao, tena utumie bando lako. Unataka kodi zetu ndo utumie kuchat insta? Damn .....!
Sawa tumekuelewa,ila huo wakati wa break kazini ni saa ngapi mkuu ? au ulikuwa unamaanisha ni baada ya muda wa kazi..?
 
Watu ni wagumu kuelewa jamani,iyo ishu inahusu wale wanaotumia rasilimali gvt ikiwemo internet kwa matumizi binafsi wakati serikali inalipia.Ukihitaji mitandao ya kijamii+kudownload movies tumia rasilimali zako binafsi.mfano mzuri wakati tuko college kuna net ya bure ambayo wanafunzi tunaitumia vibaya ikiwemo kudownload movies,ngono kinyume na utaratibu.

Wazee wa kukurupuka yaani hawasomi wao wameangalia kichwa cha habar tu na kurukia kukomenti. Mbona imeeleweka kabisa kwamba wanazuia matumiz ya internet kwny ofis za serikali. Inamaana wewe mfanyakazi kama unataka internet tumia kwny simu yako, bando lako ebo!
 
Back
Top Bottom