Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 44,096 na kupandisha madaraja watumishi 92, 619

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Kada ya elimu wataajiri watumishi wapya 10,297, afya 11,215, kilimo 1,383, mifugo 1,250, uvuvi 733, Jeshi la Polisi 1,782, Magereza 843, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji 512 na watumishi wapya wa hospitali za mashirika ya kidini na hiari 1,240.

Serikali ya Tanzania imesema katika mwaka wa fedha 2021/22 inatarajia kuajiri watumishi wa umma wapya 44,096.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 22, 2021 Waziri wa Nchi Ofisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa wakati akiwasilishwa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Amesema kada ya elimu wataajiri watumishi wapya 10,297, afya 11,215, kilimo 1,383, mifugo 1,250, uvuvi 733, Jeshi la Polisi 1,782, Magereza 843, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji 512 na watumishi wapya wa hospitali za mashirika ya kidini na hiari 1,240.

Amesema Serikali itaajiri watumishi 14,841 wa kada mbalimbali ikiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu vyote vya umma nchini pamoja na kada nyingine ambazo haziko kwenye sekta zilizoainishwa awali.

Hata hivyo, amesema watumishi 92,619 wa kada mbalimbali watapandishwa vyeo na watumishi 2,360 watabadilishwa kada katika utumishi.

Amebainisha kuwa maelekezo yatakayotolewa wakati huo ni kuchambua na kuhakiki madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma 17,699 yenye thamani ya Sh37.47 bilioni na kuchukua hatua ipasavyo.

Aprili 15, 2021 Serikali ya Tanzania ilieleza matarajio yake ya kuajiri watumishi wapya 44,811 katika mwaka wa fedha 2020/21.

Hayo yalielezwa na aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka huo wa fedha.

Alitaja ajira hizo mpya kuwa ni kada ya elimu (13,529), afya (10,467), kilimo, mifugo na uvuvi (2,145) Jeshi la Polisi (2,725), magereza (685), Jeshi la Zimamoto (501), uhamiaji (495) na hospitali za mashirika ya kidini na hiyari (1,262).

Chanzo: MWANANCHI
 
Binafsi sikubaliani na huu mfumo wa ajira wa sasa wa kutegemea ajira za serikali tu.

Serikali iboreshe mazingira watu wengi waajiriwe na sekta binafsi.

Serikali itaajiri hadi lini? Kwa presha ya sasa itabidi kila mwaka serikali ilazimike kuajiri ili kuwaziba watu midomo lakini hii sio njia nzuri ya kutatua tatizo.

Kwa mtindo huu wa kutegemea ajira za serikali na serikali ikawa inaajiri kila mwaka itafika wakati mapato yote na makusanyo yanaishia kwenye kulipana mishahara tu.

Serikali kwanza irekebishe mifumo, isambaze pesa sekta binafsi. Pili ipitie upya muundo wa watumishi wake. Unaenda shule za mjini waalimu 80, shule za vijijini waalimu 2.

Kabla ya kufikiria kuajiri, kwanza pitia miundo upya, boresha mazingira ya hao watumishi waliopo watafanya kazi kwa morali, mfano mwalimu leo analipwa 720,000. Unataka utajiri mwalimu mwingine, wakati hiyo hela ya mwalimu mpya ukiboresha mazingira kwa mwalimu aliepo ukamlipa 1M ama 1.1M, huyu atakua moralized sana na atafanya kazi hata ya waalimu 2.

Tuboreshe sekta binafsi kwanza, pili tuboreshe maslahi ya watumishi tulionao kabla ya kufikiria kuajiri wapya.
 
Wewe huko kwenye theory ya Quality vs Quantity ila kwa Tanzania yetu tulisha changua Quantity kuliko Quality..... angalia mashule yenyewe ma hosipitali mabarabara nk... acha watu wapate ajira Quality badaye jomba.
 
Back
Top Bottom