Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 44,096 na kupandisha madaraja watumishi 92, 619

Binafsi sikubaliani na huu mfumo wa ajira wa sasa wa kutegemea ajira za serikali tu.

Serikali iboreshe mazingira watu wengi waajiriwe na sekta binafsi.

Serikali itaajiri hadi lini? Kwa presha ya sasa itabidi kila mwaka serikali ilazimike kuajiri ili kuwaziba watu midomo lakini hii sio njia nzuri ya kutatua tatizo.

Kwa mtindo huu wa kutegemea ajira za serikali na serikali ikawa inaajiri kila mwaka itafika wakati mapato yote na makusanyo yanaishia kwenye kulipana mishahara tu.

Serikali kwanza irekebishe mifumo, isambaze pesa sekta binafsi. Pili ipitie upya muundo wa watumishi wake. Unaenda shule za mjini waalimu 80, shule za vijijini waalimu 2.

Kabla ya kufikiria kuajiri, kwanza pitia miundo upya, boresha mazingira ya hao watumishi waliopo watafanya kazi kwa morali, mfano mwalimu leo analipwa 720,000. Unataka utajiri mwalimu mwingine, wakati hiyo hela ya mwalimu mpya ukiboresha mazingira kwa mwalimu aliepo ukamlipa 1M ama 1.1M, huyu atakua moralized sana na atafanya kazi hata ya waalimu 2.

Tuboreshe sekta binafsi kwanza, pili tuboreshe maslahi ya watumishi tulionao kabla ya kufikiria kuajiri wapya.
Safi
 
ingeacha kuajiri kwanza au iajiri wastani ili kujenga uwezo wa kuwaboreshea masilahi waliopo.

lkn pia ni wakati sasa serikali ikaajiri kwa MIKATABA YA Muda sio KUDUMU.

MKATABA WA MIAKA 3 ikimpendeza mwajiri anaongeza. vinginevyo anasitisha mkataba, hii itasaidia sana kuongeza ufanisi kazini, na pia wataheshimu kazi.
 
Hiki unachokisema kinatumika nchi gani??.

Suala la watu kutoheshimu kazi ni hulka tu ya mbongo. Porojo nyingi kazi ni sifuri.
 
Back
Top Bottom