Serikali ya Tanzania isyoaminika na watanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Tanzania isyoaminika na watanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by msani, Mar 13, 2012.

 1. msani

  msani JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ni jambo la hatari sana kufikia hatua wananchi wanashindwa kuiamini serikali iliyopo madarakani,na hii sasa inaonesha kuzoeleka katika nchi ya Tanzania ambapo sio vyepesi kuamini kinachoelezwa kwa umaa kama taarifa.

  Tukio la N/W Malima kuibiwa vifaa huko morogoro huku akiwa ameenda kuangalia tv sebuleni(sijui chumbani hakukuwa na tv na gharama yote hiyo ya chumba) alieleza mwenyewe akihojiwa na waandishi wa hbr juu ya wizi huo.

  Malima:
  "wameiba laptop 2 na pesa na baadhi ya vitu kwenye begi. lakini cha kushangaza hawa wezi hawakuchukua bastola na bunduki yangu yangu yangu ya smg ambapo ingekuwa mtaji mzuri sana huko mitaani"

  hiyo hapo ilikuwa ni taarifa ya aliyeibiwa na ambaye ndiye mmiliki wa hivyo vitu na ndiye anayevijua vizuri vitu vyake,lakini taarifa ya kamanda wa polisi ni hii hapa

  "KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

  Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu."........

  sasa nani mkweli hapo au malima alikurupuka kuongea na sasa anajaribu kusafishwa kama ilivyo kawaida?
  Kuamini unachoambiwa hapa Tanzania inakubidi uwe mwendawazimu
   
 2. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Siamini kama hii ni habari ya kisiasa lakini uliyosema ni sahihi. Aliyeibiwa anasema SMG yake haikuchukuliwa halafu kiongozi wa polisi anasema aliyeibiwa hakuwa na silaha ya namna hiyo. Bado ninashangazwa na thamani ya vitu alivoibiwa Waziri. Mtu anaambatana na vitu vyenye thamani ya mil 23.25???

  Ukweli kwa viongozi wetu si moja ya mambo ya kufanya!!
   
 3. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,734
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Tatizo la taarifa hizi kutofautinana ni kwasababu bwana mkubwa alikuwa na kicheche kikamkoleza mzee akaota yuko kwenye nchi ya ahadi maziwa na asali... watu wakachukua mtaji sasa huu mzunguko wote wa nini tunapotezeana mda wa kuongea mambo mengine muhimu. cha msingi kama angetaka watu wasijue angekufa na tai shingoni kimya kimya na askari wake. wote sisi ni watu wazima tusichezeane akili.... ole wao wautumia usiku vibaya
   
 4. P

  Pelege Senior Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni serikali legelege na dhaifu ya CCM isiyoaminika hata kidogo.
   
 5. msani

  msani JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  tamthilia kila kukicha!!!!!!
   
Loading...