Serikali ya Tanzania ishushe mafuta - sekta ya usafirishaji inategemea mafuta

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,382
1,247
UCHAMBUZI WA MAKATO NA MAPENDEKEZO MAPYA KWA KILA LITA MOJA YA MAFUTA YA PETROLEUM NCHINI TANZANIA 2022

Zimejitokeza mikanganyiko mbalimbali kutokana na bei za mafuta kuwa juu sana.

Baada ya sintofahamu hii juu ya mafuta, ni vyema Serikali ikaondoa au kupunguza baadhi ya kodi ambazo zinamnyonya mwananchi. Kodi hizo zinazoshauriwa kupunguzwa au kuondolewa zimeainishwa kwa alama ❌ nazo ni kama zifuatavyo:-

MAPENDEKEZO YA KUPUNGUZA BEI

1.Bei ktk Dar port (CIF) = 1,162

2. Wharfage 20.5 ❌ (ibaki tshs 5);
3. Railway dev levy 19.4 ❌ (ibaki tshs 5);
5. Customs processing fee 6.0❌ (ibaki tshs 1.0);
5. Weights & measures fee 5.66.0❌ (ibaki tshs 1 .5 _maana ni uhakiki tu);
6. TBS charge 10.0❌ (ibaki tshs 2.0);
7. TASAC fee 8.7❌ (iondolewe yote)
8. EWURA fee 9.0❌ How wapate kwenye Marketing Fee na Executive agent fee
9. Fuel marking 16.0 ❌ (ibaki tshs 10)
10. Demurrage costs 8.0 ❌ (Why on fuel iondolewe);
11. Surveyors cost 8.00 ❌ (What are they surveying - iondolewe);
12. Financial cost 17.0❌ (What Finance ??? - iondolewe);
13. Evaporation losses 6.5 ❌ (ibaki tshs 1.0);
14. Fuel levy 513.00 ❌ (ibaki tshs 313.00);
15. Excise duty 479.0❌ (ibaki tshs 279);
16. Petroleum fee 180.0❌ (inatofauti gani na fuel levy - iondolewe);
17. Oil marketing companies 163.0✔️
18. Charges to executive agencies 6.0 ✔️
19. Servce levy to LGA 6.7✔️
20. Retailers margin (profit) 210.5✔️
21. Transport charges (local) 50.5✔️

Jumla ya Ushuru ni 1,054.1
Jumlisha CIF ni 1,162

Jumla Bei ya kuuzia = 2,216.1

Serikali ondoeni hii Tsh 1,743.4 Kodi yote, yaani kodi ni kubwa kuliko bei ya mafuta na imefanya watanzania wabebe mzigo mkubwa bila sababu.

Aidha, katika kipindi hiki kigumu, serikali itafute vyanzo mbadala vya kukusanya mapato yake ili kuendesha shughuli zake.

Vilevile ihakikishe ukusanywaji wa mapato katika kila Idara unasimamiwa vyema sana (EFD ihusike sana), hakika itakusanya fedha nyingi sana huko.

Ili kuhakikisha maisha ya Mtanzania yanakuwa nafuu na mazuri, ni vyema sana bidhaa ya mafuta isizidi tshs 2500/- kwa lita Moja.

Lakini ipo haja ya kubana matumizi yanayosababishwa na safari za viongozi - kwa kuwa kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nchini ina mfumo wa vikao na mikutano uitwao E-conference ambazo zilijengwa kwa kodi za watanzania.

Ningeandika mengi lkn niishie hapa ingawa iwapo Mamlaka za Serikali zikipenda kushauriwa basi nafasi iko wazi na zinitafute kwa simu hizi:-

Msakila M Kabende
Economist &
C.E.O - Smart Agrobusiness Company
0747-718-545
 
Ushauri mzuri japo tunapaswa kuangalia pia uwiano majirani zetu, Bei zetu zikishuka pakswa na tofauti significant tatizo jipya.

Marking fee, haina maana awali waliweka zama za kuchakachua mafuta ya taa, bado ikawa ngumu, suluhu wakapandisha Kodi mafuta ya taa kwanini marking fee ilibaki??
 
Back
Top Bottom