Serikali ya Tanzania iruhusu Watanzania kumiliki utajiri wa dunia kwa kuruhusu ununuzi na uuzaji hisa masoko makubwa ya hisa duniani

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,560
2,000
Kupata Watanzania wengi matajiri sio rahisi tusiporuhusu watu kununua hisa na kuuza kwenye masoko makubwa ya hisa Duniani yaliyoko Ulaya, Marekani na Japan. Huko ndiko matajiri wa dunia huzalishwa kwenye hayo masoko

Pia Kuwezesha nchi kuwa na pesa nyingi za kigeni badala tu ya kutegemea mauzo ya mazao ya korosho sijui dengu na mazao mengine ya mashambani yanayotegemea Hali ya hewa

Kwenye hayo masoko ndiko kwenye mikampuni mikubwa Duniani inayoongoza kupata faida ambayo huuza hisa na kununua

Bila Tanzania kuwa active kwa Watanzania kushiriki biashara ya hisa ya kimataifa umaskini utaendelea

Soko la ndani la hisa Ni dogo na maskini ndio maana unakuta hata kampuni Kama Vodacom hisa zimedoda sokoni.

Soko maskini halizalishi matajiri.Ndio maana impact ya soko la hisa la Tanzania haionekani kwa Mwananchi wa kawaida kubadili maisha yake akinunua hisa!!!

Kuna masoko zamani madogo lofa yalikuwa yakiitwa soko mjinga.Ukipata meza Hapo ya kuuza ujue utaondoka kapa Kama Ni nyanya zitakuozea kwenye meza
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
7,623
2,000
Kweli kabisa ni moja ya mbinu ya kuwawezesha raia, ila kama dola iko serious yako mengi mno...
Kama kuangalia maswala ya riba za mikopo, mifumo ya kodi, mazingira bora ya kufanya biz hasa kwa SME's n.k n.k.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,560
2,000
Kweli kabisa ni moja ya mbinu ya kuwawezesha raia, ila kama dola iko serious yako mengi mno...
Kama kuangalia maswala ya riba za mikopo, mifumo ya kodi, mazingira bora ya kufanya biz hasa kwa SME's n.k n.k.
Uchumi wa marekani wa ndani asilimia kubwa unategemea SME na wako serious hasa kuisaidia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom