Serikali ya Tanzania inawachukulia vipi watanzania ambao wana dharura kama kufiwa wanapotokea nje ya Tanzania?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,876
20,285
Suala la dharura mara nyingi huwa halikwepeki na hutokea wakati wowote ule.

Ndo maana hata katika nchi ambazo zimedhurika kabisa na athari za ugonjwa wa Covid-19 zimechukua hatua kadhaa ambazo wananchi wanapaswa kuzifuata ili kujikinga na madhila ya gonjwa hili hatari linalosababishwa na kirusi cha corona.

Nchini kwenye nchi za Italia, Uingereza, Ufaransa na Hispania mikusanyiko imepigwa marufuku kabisa na ukionekana unazurura kwenye viambaza au pembezoni mwa barabara basi polisi wanachukua hatua ya kukupa onyo au kukupatia faini kabisa.

Nchini Ufaransa unatakiwa kujaza fomu kabisa mtandaoni ya kukuruhusu kutoka nje kwa sababu maalum kama kununua dawa au mahitaji muhimu kama chakula.

Pia nchi nyingi zimefunga anga zao yaani hakuna ndege kutua au kuruka isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini.

Isipokuwa tu shughuli za msiba ndizo zimeruhusiwa na zikihusisha wanafamilia pekee ambapo watafanya shughuli hizo kwa ukimya na wanamaliza kisha wanaruddi majumbani mwao kuendeleza msiba.

Lakini Tanzania bado ndege zaendelea kutua na kwa uchunguzi wangu nimegundua kuwa hata usiku huu ndege kama Ethiopia Airlines inatarajiwa kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London kuelekea Addis Ababa kupitia uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere nchini Tanzania.

Kama mmoja wa abiria wa ndege hiyo ni mfiwa na anatarajia akitua kesho mchana uwanja wa ndege wa JNIA atoe sababu kwamba ana msiba hivyo asiweze kupelekwa au kujipeleka karantini ambako atakaa kwa siku 14?

Je, kama msiba umetokea leo mchana na abiria huyo amejulishwa baadae mchana huu na akakata tiketi ya ndege ya kwenda Tanzania, uataratibu wa kuwapokea wageni ambao ni wafiwa umekaa vipi?

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwa hali ilivyo nchi kama USA.. UK.. Italy hata kama mtu akifiwa na wazazi wake akae tu huko maana anaweza kuja kuzika akaambukiza watu 100 ukawa msiba mkubwa kwa nchi
 
Akili za Kiafrika nazo zinatukwamisha sana. Yaani msiba nao ni dharura?

Marehemu akishakufa dharura zote zimeisha, dharura ni wakati anatibiwa. Kiherehere cha kuzika kinaambatana na kuua watu wapya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom