Serikali ya Tanzania inatumia ipasavyo Tafiti za Wasomi wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Tanzania inatumia ipasavyo Tafiti za Wasomi wake?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by RayB, Dec 5, 2009.

 1. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF hebu tuangalie naomba suala lazima la utumiaji wa tafiti zetu tunazozifanya hapa Bongo. Katika upeo wangu na mlolongo wangu wa kutafuta elimu nimekumbana na tafiti nyingi sana na mimi mwenyewe nikiwa mmoja wapo wa watu ambao wamebahatika kufanya tafiti mbalimbali ndani na nje ya nchi. Lakini kiukweli mpaka leo sijaona matokeo ya tafiti nyingi ninazozifahamu hapa kwetu.

  Resource nyingi sana huwa zinatumika kufanya tafiti hizo lakini mara zinapopelekwa katika nagzi ya serikali ili kufanya maamuzi huwa hazianyiwi kazi ukizingatia na serikali za wenzetu. Na mimi naamini wenzetu wameendelea sana kutokana na hilo na ndo maana katika bajeti zao tafiti huwa zinapewa kipaumbele sana.

  Ukipita katika maofisi ya Wizara mbali mbali utakuta makabrasha ya data mbali mbali lakini watu bado wanafanya kazi kwa kutumia miongozo iliyojengwa chini ya data zilizopitwa na wakati ndo kusema wanafanya kazi kutokana na mazoea tu.

  Kitu kingine ambacho huwa kinaniumiza kichwa hivi utasikia sijui timu ya wizara ya kilimo ilikuwa Misri kujifunza kilimo cha umwagiliaji lakini wakirudi huku hawafanyii kazi kabisa bali kuonyeshana picha walizopiga katika mabembea huko nchi za watu.

  Nawasilisha
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ha ha ha

  wana muda hata wa kusoma hizo tafiti..ndugu?

  Wako busy nakuomba msaada ..tanzania sijaona nchi ya ajabu kama hii ambayo solutions zote za matatizo yake lazima wa outsource, hakuna local solutions kutoka kwa wasomi wa ndani.na wala hawazitumii...

  utalii mkulu anasema tu-copy huko jamaica na cuba..badala ya kuuliza chuo cha utalii etc etc ni upuuzi mtupu..
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Na sisi wananchi pia tunachangia.....

  Sasa kila mtu anataka furniture za nje,hata kama ubora ni
  wa chini kuliko za kwetu...

  Serikali bogus,wananchi pia.
   
 4. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu pinda alishatoa majibu.Alipoambiwa maendeleo makubwa ya kilimo aliyoshudia indonesia inatokana na wanasayansi aliuliza KWANI HUKU HAKUNA WANASIASA?.Kumbuka ni mkuu wa serikali.Maanayake ni kwamba serikali yake wanasiasa wanasema wataalam wanafuata.Ni aibu lakini ndo Tanzania.May be isemwa na IMF au WB.Vingevyo tafiti za ndani havina nafasi.Hapa ni hakina makamba, Sofia Simba, masha, RA EL na hao wenye degree feki ndo wanaongoza sisi tunafuata hakuna tafiti.
   
 5. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo la waTz ni kwamba wanaoenda kujifunza jambo nje si watendaji/wataalamu bali ni adminstrators! Wakisharudi toka kujifunza makarabrasha wanayaweka kwenye mashelf na hawayatendei kazi! Haya mambo ya kukimbilia posho nje yanatuumiza sana nchi yetu!
   
 6. Madago

  Madago Senior Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni topic nyeti na ya msingi sana. Hua ninasikitika sana ninaposikia wanataaaluma wetu na vyuo vyetu vikipigwa vita humu JF as if hakuna kitu wanachokifanya. Kuna tafiti nyingi mno ambazo tena serikali yenyewe ili commission kwa consultancies wa kwenye hivi vyuo majibu yakatolewa lakini utekelezaji sifuri. Tatizo liko wapi? Kwa uzoefu nilouona ni kwamba nchi yetu na uongozi wake kwanza hakuna mfumo wa kuweka vipaumbele (priority setting mechanisms) na la pili na nafikir ndio kuu ni maamuzi ya kimaendeleo yanaagalia zaidi mwelekeo wa kisiasa unavyoenda. Kama rais katoka sehemu flani au waziri wa eneo fulani, mafungu yanenda kule. Ikifika wakati wa uchaguzi hata kama wasomi watatoa decisions za kunusuru nchi kiafya au kiuchumi priority itaelekezwa kupeleka "maendeleo" kule ambako kura sinaweza kupotea. nk
   
 7. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tuendelee kutafiti na kuzitangaza tafiti zetu. IPO SIKU!!!!
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  This is Tanzania. Hatuna lolote tunalotaka kujifunza. Tunapoteza muda mrefu kuzurura nje, kama watoto tusio na baba. I dont understand kama viongozi wetu wanafikiriaje mustakabali wa Taifa.Naona kama wanafikiri usanii ndo utatuletea tunayoyahitaji.
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  H… Healthy, Hopeful, Humble, Humorous, Hummus eater

  A … Appreciative, Approachable, Activist for global peace & justice

  P … Peaceful, positive, …

  P … Passionate, practical, …

  Y… Youthful, yummy, …
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  tuwe wakweli kidogo by looking at another angle, wengi thesis na projects ni za kudesa, cooking data, na kudownload kutoka kwenye internet. Sasa hizo research zinazofanywa na graduates waliocook data, zinaweza kutumika kivipi ili hali kila mtu anajua aliyefanya hiyo research hajawaji kufanya yoyote reliable hata ya Masters degree ali cook data? graduates mwenye ku-cook data atawezaje kuresearch kitu chenye faida kwa nchi? uzoefu and skill ya kuresearch kaitoa wapi?
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  Ndahani, this country has no leader. Ili kuamsha waTz we need a dikteta hata kwa miaka miwili pale ikulu. kwanza hata Rais wa sasa hajui hata Job Description yake au pengine haipo kabisa ktk katiba na hata mawaziri sidhani kuna mwenye job description.

  This is a great country without leadership, but amazingly people get away with life!
   
 12. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2009
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nchi yeyote ile haiwezi kuendelea bila kufanya tafiti mbalimbali hasa zinazohusu maendeleo ya jamii yake. Tanzania na nchi nyingi za ki-Afrika haziendelei si kwamba hazifanyi tafiti ila misingi ya maendeleo iliyowekwa na viongozi wetu akiwemo Nyerere, Nkrumah, Kenyata na wengineo katika Afirika ilijengwa katika umimi zaidi kuliko maendeleo ya jamii nzima.
  Kwa hiyo kiongozi yeyote yule aliye madarakani atahakikisha tafiti zote iwe kwenye elimu,afya,kilimo nk zinakuwa(cooked) ku-support matakwa ya watawala na wanaomzunguka. Kama hayaendani na matakwa yake atatumia nguvu aliyonayo kama(machinery)Mahakama,Bunge (watu) kama REDET,Tume,wanasiasa,watabiri kina Yahaya kuwa ndio misingi mikuu kwake kwa tafiti zozote zile.
  Kwa maana hiyo wewe kama una utafiti wako halisia itabidi uchujwe kwanza na wanasiasa, wataupindisha, wakishindwa kuuzuia mahakama au bunge litauzuia.
   
 13. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #13
  Dec 27, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Lumbe kula tano,nakubaliana na wewe juu ya ku cook data hata humu jamvini tumo wengi tu.
  Pili hizo research naamini zipo ambazo zinaweza kuanza kufanyiwa implementation katika ngazi walizopo hao wasomi kwa kuanzisha miradi kama demonstration kwa jamii, na jamii au wasomi wengine waka copy na ku paste au wakaendeleza kuanzia pale alipoishia yule aliyeanzisha.
   
 14. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #14
  Dec 27, 2009
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wakuu,
  Hii ni mojawapo kati ya threads nilizozipenda hapa JF! Ni kweli kabisa tafiti zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mataifa mbalimbali. Licha ya kwamba maarifa yanayopatikana kupitia tafiti ndio yamemwendeleza mwanadamu kufikia hapa alipo, nchi moja moja hufaidika kiuchumi kutokana na kazi za watafiti wake.
  Naomba tunapoendelea kuchangia tuzingatie pia kuwa, tafiti si zile tu zinazofanya na wanafunzi 'wanaodesadesa', yamkini wanafanya hivyo kwa ajili ya certification. Hata hivyo hili ni tatizo ambalo vyuo husika havina budi kulidhibiti, kwa sheria dhidi ya plagiarism. Katika vyuo vingi duniani ukibainika umedesa hiyo degree sahau. Aidha, tunao watanzania wengi ambao wamesoma katika vyuo visivyoendekeza kudesa, sidhani kama hata hawa wamejiingiza katika utamaduni wa 'kupika' takwimu. Kama wanafanya hivyo, basi aliyeturoga alikufa.
  Pili, watafiti wengi tulionao (Doctors and Professors) wamekuwa watumishi wa mataifa na mashirika ya nje (wale wenye uwezo wa kutoa research funds) na hapa ni wale waliohama kabisa nchi na/au wale waliobaki nchini. Serikali inao wajibu wa kuwatumia kwa kuwapa maslahi stahili na ku-commission tafiti zao. Bahati mbaya haifanyi hivyo katika kiwango kinachoridhisha. Hapo ndipo taifa linapopata hasara mara mbili, human resource ya nchi inatumika kwa faida ya nchi zingine (Mwalimu alisema, ili nchi iendelee inahitaji watu wake)
  Tatu, nchini Tanzania taasisi za utafiti sio vyuo vikuu tu, zipo nyingi. Tatizo lipo katika matokeo ya tafiti za taasisi hizi kufika katika sekta lengwa. Huu nadhani ni wajibu wa taasisi kwa kiasi kikubwa. Huwa najiuliza, inakuwaje matokeo ya tafiti za REDET yanajulikana nchi nzima, lakini kutoka kwingine husikii kitu; au ni kwa sababu za REDET ni za kisiasa na wanasiasa wako interested?
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tafiti hazifanyiwi kazi kwa sababu tumetawaliwa sana na siasa, kama tafiti hazina masilahi kwa wanasiasa zinaishia kwenye makablasha.
   
 16. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  hii ni mada nzuri sana kwa taifa, lakini mafanikio yake yamekuwa pia hayaonekani kwa kuwa tumetawaliwa sana na siasa. Lakini kama sheria ya plagiaism ipo, kwanini isifanye kazi humu nchini? Nadhani taasisi husika ina jukumu la kufuatilia na kumuajibisha mwenye ku-cook data vilivyo, vinginevyo taasisi hiyo ijulukane kuwa imeshindwa kazi na kufutiwa hata uhalali wake. Ni vema hata kuwa na taasisi moja nchini, lakini yenye sifa dhabiti za kupitisha tafiti kama hizi, kuliko kubaki na nyingi zenye kutumika kama loophole ya kufoji taaluma na ku-cook data.

  Huenda hali hii ndio imepelekea hata wataalam (hasa Doctors and Professors) humu nchini kijiingiza kwenye siasa, badala ya kubaki kama kioo na washauri wa jamii. Hii ni kwa sababu maslahi yameelekezwa kwenye siasa zaidi kuliko kazi zao. Pia ukijaribu kufuatilia mahusiano kati ya wanasiasa (hasa wabunge) na wasomi katika majimbo huenda yasiwe yenye kuonesha maelewano na ushirikiano katika kupambana na janga la umaskini, maradhi na ujinga. Ni kwa kuwa tu kila mmoja anajiona kuelewa kuliko mwingine.

  Ukifuatilia pia bajeti za kila wizara, hakuna hata kifungu cha "researches"! Hii inaonesha ni jinsi gani hata serikali yetu isivyodhamini tafiti, na kama ipo basi wanatumiwa wataalam kutoka nje (outsourcing).

  Sawa, ni vema kufanya traninings mbalimbali kwa watumishi, lakini si kila mtumishi anastahili kwenda kila training. Nadhani kila training inavyotokea inastahili kuwapelekea watu wahusika, mf. mhasibu kwa maswala ya fedha na si kwa maswala ya madini. Hata hivyo kila atakayepelekwa aahidi kuleta matunda mara tu atakaporudi, na asipelekwe tena hadi matunda ya aliyohudhuria nyuma yaonekane kutoka kwake.
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Asante mwanawane, sijasikia thesis, wala dissertation yo yote iliyo kuwa implemented hata na UDSM yenye faida si tu kwa nchi hata kwa chuo chenyewe zaidi ya machine za kufyatua tofali alizokuwa anasimamia Dr. Kawambwa.
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkulu usiiesabu REDET kama taasisi yenye faida kwa nchi, ni uzushi mtupu hawa jamaa huwa hata hawadensi huwa wanacook data kwa malengo ya kupewa vyeo na wanasiasa.

  Pili fikiria kuwa chuo kama mzumbe ambacho wahitimu wake wengi ndio watumishi wa serikali za mitaa na serikali kuu kutokana na historia yake. Maprofessor wake na wahadhiri baadhi wamenunua vyeti, sorry wamedai wamesoma chuo kikuu kinachoitwa Pacific Western University, chuo alichosomea Mh Lyatonga-chuo ambacho ni feki, makao makuu ya chuo ni kibanda kama cha muuza mitumba pale Los Angeles. Hawa wanaweza kweli kumwandaa researcher?
   
 19. nzehe

  nzehe Member

  #19
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Hii thread ni nzuri sana kwa sababu imegusa mojawapo ya sababu ya maendeleo yetu kusuasua.
  Wakati umefika tupunguze tafiti nyingi bali tufanye kazi kwani tafiti nyingi lengo lake kwanza ni kuvuta kasma ya kuitengeneza,makongamano na safari za kitafiti baada ya hapo tunaweka makabrasha makabatini.
  Tanzania tuna watafiti wengi wazuri sana sikatai lakini watendaji wako wapi?na kama wapo wameonyesha model ya tafiti hizo?
   
 20. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hizi ndio siasa zenyewe sasa na si kule kwenye jukwaa la siasa kumejaa ushambenga mtupu. Thanks very much na wachangiaje wote wa hii thread for the eye opening issues.
   
Loading...