Serikali ya Tanzania ina ‘hit squad’ yake au?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,519
Prof. Nicas Mahinda

Prof. Athumani Livigha

Prof. Jwani Mwaikusa

Dr. Sengondo Mvungi

Dr. Steven [Stephen?] Ulimboka

Tundu Lissu

Ben Saanane

Mohammed Dewji

Abdul Nondo

Roma Mkatoliki......

Kwa nini nimewaorodhesha hao watu?

Nimewaorodhesha kwa sababu, wote hao wana ‘common denominator’ katika yaliyowatokea, hususan baada ya [ma]tukio.

Mpaka leo bado hakuna taarifa za uhakika kwa nini Prof. Nicas Mahinda aliuwawa!

Dr. Ulimboka alitekwa na baadaye akaja kukutwa/ kuokotwa huko Mabwepande akiwa hajitambui.

Ben Saanane haijulikani alipo.

Mpaka sasa hatujui ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu pale Dodoma.

Roma Mkatoliki naye alitekwa lakini akaja kuachiwa akiwa mzima.

Majuzi tu hapa bilionea Mo Dewji alitekwa halafu eti akaja kutupwa usiku wa manane kwenye viwanja vya Gymkhana.

Matukio yote hayo ya watu kutekwa, kujaribiwa kuuwawa, na kupotea kabisa, hayana maelezo yaliyokamilika wala kunyooka.

Watu hata hatujui kwa nini Mo alitekwa, achilia mbali alitekwa na nani!

Ni zaidi ya mwaka sasa baada ya Lissu kujaribiwa uhai wake na hakuna hata mshukiwa/ washukiwa.

Sasa mimi nauliza, hivi serikali ya Tanzania ina ‘hit squad’ yake au?

Matukio yote haya ya uhalifu dhidi ya raia, wananchi hatupewi taarifa za kutosha zinazoyahusu.

Kwa nini hasa?

Ukosefu wa taarifa za kutosha na kuridhisha ni moja ya sababu zinazowafanya baadhi ya watu waamini kuwa huko serikalini kuna ‘hit squad’ na kuna watu wanaojua fika kinachoendelea.

Kama hakuna ‘hit squad’, mbona hatupewi taarifa?

Hali inatisha.....
 
Kutakuwa na kikundi kinachojihusisha na mauaji na utakaji!
Kikundi hicho kinategemea orders kufanya kazi!
So tunaweza kuona ni vipi mkulu anaweza akawa israel mtoa roho!
Nakubaliana na wewe. Na mara nnyingi hata rais mwenyewe unaweza kuta hata hakifahamu vyema hicho kikundi. Yeye anajuwa kuwa kinamlinda tu basi. Lakini ugoro wanaofanya na unyama wanaoufanya kwenye hiyo process kwa jina la kumlinda, angetumia akili angekomesha haya mambo.

Mara nyingi ni wapambe nuksi!
 
Nyani ngabu ‘Hit squad’ ni Polisi na serkali …...ukifatilia Kesi ya Abdul Nondo ndo utajua wasio julikana ni ‘hit squad’ ndani ya Polisi na Usalama wa Taifa.Kosa kubwa waliofanya kwa kesi ya Nondo ni kupeleka Mahakamani na kuna uwezekano hawatapeleka kesi nyingine tena
 
Hit squad imeanza siku nyingi sana na imegharimu sana maisha ya wapendwa wetu.

Toka kuuwawa kwa Kassim Hanga mpaka Kolimba, kuuwawa kwa Kombe mpaka Mtikila.

Kupotea kwa Kanali Mahfoudh mpaka Ben Saanane na Mo?

List ni ndefu, hit squad haiwezi kuwa mtaani kama Temeke, Tandale, Buzuruga, Kijenge Juu, Sahare, Isaka au Bububu. Hit Squad iko kwao, wanaimiliki na wanailinda.
 
Hit squad imeanza siku nyingi sana na imegharimu sana maisha ya wapendwa wetu.

Toka kuuwawa kwa Kassim Hanga mpaka Kolimba, kuuwawa kwa Kombe mpaka Mtikila.

Kupotea kwa Kanali Mahfoudh mpaka Ben Saanane na Mo?

List ni ndefu, hit squad haiwezi kuwa mtaani kama Temeke, Tandale, Buzuruga, Kijenge Juu, Sahare, Isaka au Bububu. Hit Squad iko kwao, wanaimiliki na wanailinda.

Inatenda kutokana na maagizo ya nani?
 
Back
Top Bottom