Serikali ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa mimba (IVF)

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Huduma hiyo inaanza ikiwa ni miaka miwili sasa imepita tangu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuanza maandalizi ya utoaji wa huduma hiyo ikiwemo kusomesha wataalamu na kuandaa jengo litakalotumika kutolea huduma hiyo.

Akizungumza bungeni leo Jumanne Mei 11, 2021 wakati akiwasilisha bajeti kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2021/22 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri Dk Dorothy Gwajima amesema katika kipindi cha mwaka 2021/22 Muhimbili itatekeleza mambo makuu manne.

“Kupandikiza uloto (bone marrow transplant) kwa wagonjwa wenye kansa ya damu, kuanza kutoa huduma za upandikizaji wa mimba (IVF), kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa binafsi (private wards) lenye vitanda 200.”

“Tutaendeleza huduma zote za kibingwa kama vile upasuaji kwa kutumia tundu dogo, upasuaji wa kichwa, shingo na koo,” amesema Waziri Gwajima.

Miaka miwili tangu kuanza kwa maandalizi ya upandikizaji mimba MNH, yameibuka matatizo matano ya wanaume ambayo ndiyo chanzo cha ugumba, huku asilimia 50 ya wagumba wakiwa ni jinsi hiyo.

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutokuwa kabisa na mbegu, kuwa nazo zenye ubora hafifu na zisizo na mbio, mbegu chache na zinazorudi kinyumenyume au kufanya tendo mara kwa mara na hivyo kuathiri uzalishaji mbegu bora.

Kupandikiza PCC
Hata hivyo mwaka 2019 wakati wanatambulisha uwepo wa huduma hiyo, kitengo cha magonjwa ya kinamama kilisema gharama zitakuwa ni kati ya Sh2 milioni mpaka 10 milioni, kulingana na ukubwa wa tatizo.

Taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa hospitali kadhaa zinazopandikiza mimba nchini na nje ya nchi hutoza kati ya Sh8 milioni mpaka Sh25 milioni.

Mwananchi
 
Hapa mmekaa kibiashara zaidi, mngeweza kutumia gharama kama hiyohiyo kufanya utafiti nini kinasababaisha hizo mbegu kuenenda hivyo, kuwapa elimu hao wanaume namna ya kuboresha lishe ili mbegu zisiende kinyumenyume zikimbie kwenda mbele. Ila nahisi kwakuwa waziri ni mwanamke anajaribu kukwepa jukumu la mwanamke kwenye ndoa.
 
Nitakua nashida ndio ya mtoto na ntalipia hiyo mikioni labda 10 je huyo mtoto hatokufa?maana gharama ni kubwa mngeangalia ina maana mwenye hali ya chini hawezi kupata suluhisho.
 
Hapa mmekaa kibiashara zaidi, mngeweza kutumia gharama kama hiyohiyo kufanya utafiti nini kinasababaisha hizo mbegu kuenenda hivyo, kuwapa elimu hao wanaume namna ya kuboresha lishe ili mbegu zisiende kinyumenyume zikimbie kwenda mbele. Ila nahisi kwakuwa waziri ni mwanamke anajaribu kukwepa jukumu la mwanamke kwenye ndoa
Ingekuwa ni rahisi ivo eti elimu na lishe hata nchi za nje wasingekuwa na iyo huduma mkuu
 
Ingekuwa ni rahisi ivo eti elimu na lishe hata nchi za nje wasingekuwa na iyo huduma mkuu
Tuanzie hapa, nini chanzo cha hii changamoto kuongezeka kwa kasi namna hii
Je ni hewa tunayovuta?
Je ni maji tunayokunywa?
Je ni kasi ya teknolojia?
 
Kufanya tendo mara kwa mara huadhiri vip kuwa na mbegu bora? Mwenye ujuzi kwa hili afafanue tafadhali.
 
Back
Top Bottom