Serikali ya Tanzania ilipora Maelfu ya mifugo ya nchi nyingine iliyokamatwa kwenye mapori ya mpakani. Wahanga walipwe fidia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,485
215,327
Unyama wa serikali ya awamu ya 5 ulijumuisha hadi wizi wa mifugo ya nchi jirani kwa kisingizio cha kuvuka mpaka.

Mifugo kutoka Rwanda na Uganda ilitaifishwa baada ya kuvuka mpaka na kuingia kwenye mapori ya Tanzania, badala ya kurejeshwa zilikotoka viongozi wa Tanzania wakaamua kuzipora na bila shaka waligawana, maana mifugo ile haionekani popote.

Natoa wito kwa viongozi wa Tanzania wa sasa kuwalipa fidia wale wote walioporwa mifugo yao kutoka Uganda na Rwanda ili kurejesha mshikamano uliovurugwa na jiwe.
 
Hili andiko umepotoka mkuu. Jifunze kitoinenea mabaya nchi yako. Mnaweza kuwa tofauti kivyama lakini nchi kwanza vyama baadae
 
Yaani kusema kweli mtoa post anaandika kwa mihemko! Wakati mwingine ni hawa hawa wanakuja hapa kusema mwendazake alikuwa mhutu! Ingetokea aliwalipa fidia wangekuja na ngonjera za kuwa kwa vile ni wahutu wenzie kawapa fidia!

Kusema kweli nchi hii mtu anaweza kuwalisha hata vinyesi kwa vile ni jirani au mwekezaji mnacheka tu! Sie tunaotembea nchi jirani wenzetu wakao serious na nchi zao tena niwashenzi kweli kweli! Pata tatizo ndo utawajua!
 
Cha ajabu, cha kushangaza na kuchekesha ni kwamba CCM walioshangilia kipindi kile ndo hao hao wanaoshangilia kipindi hiki....chama kile kile kilichobariki huo ujinga ndio hicho hicho
 
Una hakika hizo nchi nyingine hazipori mali za wengine fanya utafiti kwanza kabla ya kusukumwa na mihemko!
 
Wazee wa EAC mpaka wa leo takriban miaka 45 hawajalipwa,dua zao zinaendelea kututafuna
 
Yaan walipwe fidia kwa ku kuingiza mifugo kwenye mapori ya Tanzania? Nani kavunja sheria hapo?

Think twice kabla hujaandika chochote
 
Tanzania ilipora ng'ombe 4,000 toka Kenya. Ikawaweka mahabusu wafugaji wa Kenya, kisha kuwaachia wafugaji mikono mitupu.

Wiki mbili baadaye, Kenya ikakamata ng'ombe 9,000 wa Tanzania walioingia ardhi ya Kenya. Wakawashikilia ng'ombe kwa siku 7, kisha wakawarudishia wafugaji wa Tanzania.

Wakati wa kukabidhi ng'ombe wale kwa Watanzania, gavana wa Kenya alisema, "Utawala wa Magufuli ni aibu kwa Afrika. Watanzania inalia, Wakenya inalia. Wamasai ya Tanzania hawana shida. Wamasai ya Kenya hawana shida. Shida ni Magufuli.

Sisi tumeamua kuirudishia wafugaji ya Tanzania ng'ombe yao. Uhuru Kenyata ameamua wale wafugaji ya Kenya walionyang'anywa ng'ombe yao na Magufuli, serikali ya Kenya itawalipa. Mfugaji itaamua ilipwe pesa au ipewe ng'ombe"
 
Yaani kusema kweli mtoa post anaandika kwa mihemko! Wakati mwingine ni hawa hawa wanakuja hapa kusema mwendazake alikuwa mhutu! Ingetokea aliwalipa fidia wangekuja na ngonjera za kuwa kwa vile ni wahutu wenzie kawapa fidia!

Kusema kweli nchi hii mtu anaweza kuwalisha hata vinyesi kwa vile ni jirani au mwekezaji mnacheka tu! Sie tunaotembea nchi jirani wenzetu wakao serious na nchi zao tena niwashenzi kweli kweli! Pata tatizo ndo utawajua!
Mngeweza kuwarejeshea mifugo yao na kuwaambia wasiilete tena, ikiwa kama yaliyofanyika yalikuwa haki kwanini Hangaya anaomba radhi kwa kuchomwa vifaranga vya kenya?
 
Tanzania ilipora ng'ombe 4,000 toka Kenya. Ikawaweka mahabusu wafugaji wa Kenya, kisha kuwaachia wafugaji mikono mitupu.

Wiki mbili baadaye, Kenya ikakamata ng'ombe 9,000 wa Tanzania walioingia ardhi ya Kenya. Wakawashikilia ng'ombe kwa siku 7, kisha wakawarudishia wafugaji wa Tanzania.

Wakati wa kukabidhi ng'ombe wale kwa Watanzania, gavana wa Kenya alisema, "Utawala wa Magufuli ni aibu kwa Afrika. Watanzania inalia, Wakenya inalia. Wamasai ya Tanzania hawana shida. Wamasai ya Kenya hawana shida. Shida ni Magufuli.

Sisi tumeamua kuirudishia wafugaji ya Tanzania ng'ombe yao. Uhuru Kenyata ameamua wale wafugaji ya Kenya walionyang'anywa ng'ombe yao na Magufuli, serikali ya Kenya itawalipa. Mfugaji itaamua ilipwe pesa au ipewe ng'ombe"
Mungu ibariki Kenya
 
Kama Walivuka mipaka ni sahihi kufanyiwa Ivo ingekuwa sisi ndio tuliwafata kwao basi ingekuwa vita ukiona kimya ujue hakuna sheria iliovunjwa
 
Ni kuwapora na sio kuzipora
Unyama wa serikali ya awamu ya 5 ulijumuisha hadi wizi wa mifugo ya nchi jirani kwa kisingizio cha kuvuka mpaka.

Mifugo kutoka Rwanda na Uganda ilitaifishwa baada ya kuvuka mpaka na kuingia kwenye mapori ya Tanzania, badala ya kurejeshwa zilikotoka viongozi wa Tanzania wakaamua kuzipora na bila shaka waligawana, maana mifugo ile haionekani popote.

Natoa wito kwa viongozi wa Tanzania wa sasa kuwalipa fidia wale wote walioporwa mifugo yao kutoka Uganda na Rwanda ili kurejesha mshikamano uliovurugwa na jiwe.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom