Serikali ya Tanzania ikishutumiwa kufanya upendeleo kwa vyombo vya Habari itaonewa?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mada inahusika.

Kumekuwa na wimbi shutuma la kuminywa kwa habari kwa vyombo mbali mbali lakini vile vile kumeonekana upendeleo wa wazi.

Kuna haya magazeti likwemo la "TIMES OBSERVER" "JAMVI LA HABARI", "LA JIJI" na mengineyo yamekuwa yakikiuka taratibu za uandishi na hatujaona hatua za wazi kuchukuliwa dhidi yao.

Magazeti haya sio tu kuwa hayafanyi " Balancing" ya stori zao kuwahusu wapinzani Tanzania, wala kutoa taarifa sawa na kuwapa nafasi, lakini wanavunjia heshima viongozi wa kitaifa wa vyama bila kuulizwa wala kuguswa.

Kwa mfano. Magazeti ya Jana tarehe 12 Agosti, 2020, magazeti hayo ya "Times Observer" na " Jamvi la Habari" yaliendeleza KASHFA kwa Maalim Seif ambaye si tu kuwa kiongozi mkubwa wa chama, lakini Mstaafu wa nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Waziri Kiongozi mstaafu.

Kwa hali hio hivi Serikali haioni upotoshaji huo na haioni uvunjifu wa amani unaokaribishwa na magazeti haya? Hivi Serikali yetu ikilaumiwa kwa upendeleo itakuwa inaonewa?

Iko wapi TCRA? iko wapi HABARI MAELEZO? Yuko wapi Waziri wa Habari?



Kishada.

Screenshot_20200813-114030.png
Screenshot_20200813-114056.png
 
Hata wewe kwa mwanao, huwezi mfanyia unyama ukamuacha mtoto wa mbali..!
 
Back
Top Bottom