Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kulipa walimu na madaktari bila kubadilisha muundo wa serikali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kulipa walimu na madaktari bila kubadilisha muundo wa serikali!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Feb 8, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tanzania haina uwezo wa kupandisha mishahara ya walimu, madaktari, askari polisi na jeshi bila kubadilisha muundo wa serikali. Nilishasema hapa kwamba Watanzania inabidi waamue serikali ifanye nini; yaani ni vitu gani vifanywe na serikali na vitugani vifanywe na biashara/kibinafsi. Bila kujibu swali hili serikali haitaweza kukithi mahitaji yote.

  Mfano: Serikali inawapa pesa ATC kampuni ambayo haina ulazima na haitoi hudumu ya kotosha lakini ni pesa hizo hizo zingeweza kutumika sehemu nyingine. Sasa Watanzania hawawezi kuruhusu vitu kama ATC halafu wakati huhu huo wanataka mishahara ipande. Kibaya zaidi ndugu zangu ni kwamba kwasababu serikali ni kubwa hakuna umakini unaofanywa kwenye mashirika hivyo hayo mashirika yanatumika kuingia mikataba mibovu kama ATC na Tanesco. Serikali isingekuwa na mkono wake hii mikataba isinge ingiwa.

  Kama Watanzania wangeamua serikali ifanye vitu tu ambavyo wananchi hawawezi kufanya wenyewe serikali ingekuwa ndogo ambayo inashughulikia mambo muhimu tu kama Afya, Elimu, Ulinzi, Barabara,Maji, na utekelezaji wa sheria mbalimbali za bunge basi. Mambo mengine yote yafanywe na watu binafsi.

  Watanzania tusiwe watu wa kulalamikia serikali wakati ukweli ni kwamba dunia imebadilika na kama hatutakuwa na muundo wa kibepari ambao una serikali ndogo basi itabidi tuwe na muundo wa kidicteta kama china. Hatuwezi kuwa na vyote.
   
 2. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  huenda unafahamu ulichokuwa unataka kukiandika. lakini amini nakwambia ulichokiandika siyo ulichotaka kukisema hapa. kaa tulia, soma uliyoandika lingalisha na uliyotaka kuandika , kisha rekebisha maandiko yako yafanane na una ulichotaka kuwafikishia wana JF, hapo ujumbe utakuwa umefika.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kindimbajuu inawezekana hujaielewa hayo maneno na maana yake iko deep sana kimawazo. Kwa wale wanaopenda topic za ushabiki itakua ngumu kuilewa lakini itafikia wakati watu wataielewa hii topic vizuri. Watu bado hawajafunguka vizuri kwenye chanzo cha matatizo ya maendeleo Tanzania.
   
Loading...