Serikali ya Tanzania haina fedha, ahadi za Kikwete kuota mbawa

Miradi ya maendeleo, ahadi za JK zakwama

na Betty Kangonga

SERIKALI inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha uliotokana na matumizi mabaya yasiyo na tija pamoja na misamaha holela ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa katika mkutano wa wahisani na watendaji wa serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, umebaini kuwa serikali ina upungufu wa sh bilioni 600 kutoka kwenye bajeti ya sh trilioni 11, iliyopitishwa na Bunge.

Kati ya sh trilioni 11, sh trilioni 6 zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.

Sababu kubwa ya kupungua kwa fedha hizo, imeelezwa kuwa ni kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika miezi miwili iliyopita.

Duru za kisiasa zinabainisha kuwa ukiachia kiasi cha sh bilioni 60 kilichotengwa na serikali kwa ajili ya kugharimia uchaguzi, serikali imetumia fedha zaidi ikiwemo uchapishaji wa mabango ya kampeni.

Matumizi mengine yanayotajwa kuathiri bajeti ya mwaka 2010/11 ni ya anasa kama vile mikutano na safari za nje na ndani ya nchi ambazo hazikuwa na tija kwa taifa na kushuka kwa makusanyo ya kodi kutokana na misamaha holela.

Mathalani katika kipindi cha Julai na Septemba makusanyo ya vyanzo vya mapato vya ndani na kutoka kwa wafadhili, yalikuwa sh trilioni 1.3 wakati matumizi ya serikali yalifikia sh trilioni 1.9, sawa na tofauti ya sh bilioni 600.

"Kwa hiyo ukiangalia hapa utabaini kuwa matumizi ya serikali kati ya Julai na Septemba, yalikuwa makubwa zaidi kuliko makusanyo ya kodi na fedha za wafadhili na hadi sasa hali bado ni mbaya kwani TRA inakusanya chini ya lengo," alisema kiongozi mmoja wa serikali kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi.

Upungufu huo wa fedha, umeibua hofu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo na ahadi nyingine za Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni kama zile za ujenzi wa barabara za juu, huenda zikakwama.

Habari zaidi zinasema kuwa fedha za wizara mbalimbali zilikuwa zikisubiri uteuzi wa mawaziri, zimepunguzwa ili kukabiliana na punguzo hilo la makusanyo ya mapato.

"Sisi tumetangaziwa kabisa kwamba sasa hakuna semina, safari za ndani na nje ni zile za lazima sana, vinginevyo hakuna," alisema mmoja wa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Hata hivyo, mambo mawili yanaweza kufanyika ili kuokoa hali hiyo, mosi ni kuwa na bajeti ndogo au kukopa kutoka benki.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, amewatoa hofu Watanzania akisema kwamba serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.

Alisema serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa.

Hii ni mara ya pili kwa TRA kushindwa kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi kama ilivyopangwa.

Katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/10, serikali ilitarajiwa kukusanya sh trilioni 5.096, lakini iliishia kukusanya sh trilioni 4.662.

Source: Tanzania Daima (15 December, 2010)

:yuck:
Kutoka Maktaba ya Ufipa.
 
Kipindi hiki Serikali ya JK ilikuwa inakusanya Trilion 1.3 kwa miezi 3 robo mwaka yaani miezi mitatu..!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom