Serikali ya Tanzania haina fedha, ahadi za Kikwete kuota mbawa

nyamagaro

JF-Expert Member
Feb 25, 2010
394
101
Miradi ya maendeleo, ahadi za JK zakwama

na Betty Kangonga

SERIKALI inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha uliotokana na matumizi mabaya yasiyo na tija pamoja na misamaha holela ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa katika mkutano wa wahisani na watendaji wa serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, umebaini kuwa serikali ina upungufu wa sh bilioni 600 kutoka kwenye bajeti ya sh trilioni 11, iliyopitishwa na Bunge.

Kati ya sh trilioni 11, sh trilioni 6 zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.

Sababu kubwa ya kupungua kwa fedha hizo, imeelezwa kuwa ni kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika miezi miwili iliyopita.

Duru za kisiasa zinabainisha kuwa ukiachia kiasi cha sh bilioni 60 kilichotengwa na serikali kwa ajili ya kugharimia uchaguzi, serikali imetumia fedha zaidi ikiwemo uchapishaji wa mabango ya kampeni.

Matumizi mengine yanayotajwa kuathiri bajeti ya mwaka 2010/11 ni ya anasa kama vile mikutano na safari za nje na ndani ya nchi ambazo hazikuwa na tija kwa taifa na kushuka kwa makusanyo ya kodi kutokana na misamaha holela.

Mathalani katika kipindi cha Julai na Septemba makusanyo ya vyanzo vya mapato vya ndani na kutoka kwa wafadhili, yalikuwa sh trilioni 1.3 wakati matumizi ya serikali yalifikia sh trilioni 1.9, sawa na tofauti ya sh bilioni 600.

"Kwa hiyo ukiangalia hapa utabaini kuwa matumizi ya serikali kati ya Julai na Septemba, yalikuwa makubwa zaidi kuliko makusanyo ya kodi na fedha za wafadhili na hadi sasa hali bado ni mbaya kwani TRA inakusanya chini ya lengo," alisema kiongozi mmoja wa serikali kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi.

Upungufu huo wa fedha, umeibua hofu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo na ahadi nyingine za Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni kama zile za ujenzi wa barabara za juu, huenda zikakwama.

Habari zaidi zinasema kuwa fedha za wizara mbalimbali zilikuwa zikisubiri uteuzi wa mawaziri, zimepunguzwa ili kukabiliana na punguzo hilo la makusanyo ya mapato.

"Sisi tumetangaziwa kabisa kwamba sasa hakuna semina, safari za ndani na nje ni zile za lazima sana, vinginevyo hakuna," alisema mmoja wa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Hata hivyo, mambo mawili yanaweza kufanyika ili kuokoa hali hiyo, mosi ni kuwa na bajeti ndogo au kukopa kutoka benki.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, amewatoa hofu Watanzania akisema kwamba serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.

Alisema serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa.

Hii ni mara ya pili kwa TRA kushindwa kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi kama ilivyopangwa.

Katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/10, serikali ilitarajiwa kukusanya sh trilioni 5.096, lakini iliishia kukusanya sh trilioni 4.662.

Source: Tanzania Daima (15 December, 2010)

:yuck:
 
If this is True then JK should be hold accountable for this mess.
They guy has been traveling more that Christopher Columbus.
He really need to step down.
Kukubali kushindwa nao pia ni uanaume...

Let some one come in and fix the mes.
Ass the matter of fact inaonekana uchaguzi alishindwa anyway...

I hope ataingia kwenye Historia ya Tanzania kama "the worst president"

==**********JK HUFAI KUWA RAIS************====
 
Miradi ya maendeleo, ahadi za JK zakwama

na Betty Kangonga

amka2.gif
SERIKALI inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha uliotokana na matumizi mabaya yasiyo na tija pamoja na misamaha holela ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa katika mkutano wa wahisani na watendaji wa serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, umebaini kuwa serikali ina upungufu wa sh bilioni 600 kutoka kwenye bajeti ya sh trilioni 11, iliyopitishwa na Bunge.
Kati ya sh trilioni 11, sh trilioni 6 zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.
Sababu kubwa ya kupungua kwa fedha hizo, imeelezwa kuwa ni kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika miezi miwili iliyopita.
Duru za kisiasa zinabainisha kuwa ukiachia kiasi cha sh bilioni 60 kilichotengwa na serikali kwa ajili ya kugharimia uchaguzi, serikali imetumia fedha zaidi ikiwemo uchapishaji wa mabango ya kampeni.
Matumizi mengine yanayotajwa kuathiri bajeti ya mwaka 2010/11 ni ya anasa kama vile mikutano na safari za nje na ndani ya nchi ambazo hazikuwa na tija kwa taifa na kushuka kwa makusanyo ya kodi kutokana na misamaha holela.
Mathalani katika kipindi cha Julai na Septemba makusanyo ya vyanzo vya mapato vya ndani na kutoka kwa wafadhili, yalikuwa sh trilioni 1.3 wakati matumizi ya serikali yalifikia sh trilioni 1.9, sawa na tofauti ya sh bilioni 600.
“Kwa hiyo ukiangalia hapa utabaini kuwa matumizi ya serikali kati ya Julai na Septemba, yalikuwa makubwa zaidi kuliko makusanyo ya kodi na fedha za wafadhili na hadi sasa hali bado ni mbaya kwani TRA inakusanya chini ya lengo,” alisema kiongozi mmoja wa serikali kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi.
Upungufu huo wa fedha, umeibua hofu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo na ahadi nyingine za Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni kama zile za ujenzi wa barabara za juu, huenda zikakwama.
Habari zaidi zinasema kuwa fedha za wizara mbalimbali zilikuwa zikisubiri uteuzi wa mawaziri, zimepunguzwa ili kukabiliana na punguzo hilo la makusanyo ya mapato.
“Sisi tumetangaziwa kabisa kwamba sasa hakuna semina, safari za ndani na nje ni zile za lazima sana, vinginevyo hakuna,” alisema mmoja wa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Hata hivyo, mambo mawili yanaweza kufanyika ili kuokoa hali hiyo, mosi ni kuwa na bajeti ndogo au kukopa kutoka benki.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, amewatoa hofu Watanzania akisema kwamba serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.
Alisema serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa.
Hii ni mara ya pili kwa TRA kushindwa kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi kama ilivyopangwa.
Katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/10, serikali ilitarajiwa kukusanya sh trilioni 5.096, lakini iliishia kukusanya sh trilioni 4.662.
Source: Tanzania Daima (15 December, 2010):yuck:

Kuna mtu aliwahigi kuweka thread hapa jamvini kuwa Hazina Imefulia. Haina mpunga.

Kidogo kidogo tutaujua ukweli.
 
hatari sana mkuu.yani ukifuatilia kwa undani matumizi ya serikali yetu unaweza ukawa mwendawazimu.na sababu kubwa ni udhaifu wa uongozi wa juu kushindwa kupriotize mambo kwa vitendo.wanabaki kupiga porojo mbele za watu ili wapigiwe makofi then in reality wanafanya madudu yaliyokithiri.
 
it is very sad inakuwaje fedha ya serikali inatumika kwenye kampeni, Jamani Watanzania lini tutaamka kupigania haki zetu na watoto wetu,
mpaka lini tutawaachia hawa wezi wachache ( ccm) waendeleee kunyonya damu zetu, mpaka lini eeeeeeeeh, ngoja nijiunge chadema . ni wapi ntapata kadi ya uanachama?
 
...tumezoea kuibiwa.....tena kweupe......!!!!
watanzania tunadhani kupigia kelele na kuchukulia hatua wizi na matumizi mabaya ya rasilimali zetu za taifa ni kazi ya Kubenea, Slaa (PhD) et al, kumbe ni kazi ya watanzania wote. ishu ya kutetea rasilimali ya Taifa inachukuliwa kichama zaidi.
 
it is very sad inakuwaje fedha ya serikali inatumika kwenye kampeni, Jamani Watanzania lini tutaamka kupigania haki zetu na watoto wetu,
mpaka lini tutawaachia hawa wezi wachache ( ccm) waendeleee kunyonya damu zetu, mpaka lini eeeeeeeeh, ngoja nijiunge chadema . ni wapi ntapata kadi ya uanachama?

Uwe unasoma na kuelewa, kampeni zinazo zungumzwa hapa na mabango ni yale yanayo husiana na Tume ya uchaguzi sio vyama vya siasa. Vyama vya siasa wao waligharamia kampeni na mabango kwa hela yao .
 
If this is True then JK should be hold accountable for this mess.
They guy has been traveling more that Christopher Columbus.
He really need to step down.
Kukubali kushindwa nao pia ni uanaume...

Let some one come in and fix the mes.
Ass the matter of fact inaonekana uchaguzi alishindwa anyway...

I hope ataingia kwenye Historia ya Tanzania kama "the worst president"

==**********JK HUFAI KUWA RAIS************====

Point taken mkuu,the way jk anavyoongoza nchi watoto,wajukuu na vitukuu nk watakuwa wanafanya kazi ya kumlipia deni lake what a country where leaders dont care for their citizens?2tafika kweli?
 
Uwe unasoma na kuelewa, kampeni zinazo zungumzwa hapa na mabango ni yale yanayo husiana na Tume ya uchaguzi sio vyama vya siasa. Vyama vya siasa wao waligharamia kampeni na mabango kwa hela yao .

Acha uongo wewe! Au na wewe ni mmoja wao nini? Gharama nyingi za tume zililipwa na wafadhili na hiyo bil. 60 sijui ilitumikaje kwenye kampeni! Siku zote wa-TZ tutaendelea kulialia tu lakini hakuna cha maana tutakachoambulia zaidi ya kuibiwa! inawezekana hizo gharama zilitumiwa na CCM "who knows?"

Jamani mkiambiwa tupigaie haki zetu hamtaki sasa mmebaki kujililia tu hapa JF - Kwishnei!! Mwanza walionyesha nia mbona wengine mlilala?
 
where is he now?

Yuko Zambia sasahv,nafikiri kabla ya mwaka kuisha atakuwa ameenda either UK au US.Sidhani kama mwaka utaisha bila kuzuru hizo nchi mbili! Yetu macho na masikio!

Nchi hii inahitaji discipline kubwa sana katika matumizi ya fedha za umma kuliko wakati mwingine wowote wa historia ya nchi hii ili kutimiza ahadi za mh.rais wakati wa kampeni lakini pia kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha za ndani.

Ni muhimu kwa serikali kuangalia upya gharama zake hasa katika recurrent expenditure na kuhakikisha kwamba maslahi ya taifa yanatangulizwa katika kutoa kipaumbele kwa matumizi ya muhimu tu na siyo yale ya Anasa.

Inawezekana Mh.Pinda kuna kundi kubwa la watu ndani ya serikali halikubaliani naye katika namna ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima katika mambo ya anasa na inawezekana kabisa hakuna support ya Mh. Rais mwenyewe ndiyo maana suala la kupunguza matumizi linakuwa ni gumu.
 
Uwe unasoma na kuelewa, kampeni zinazo zungumzwa hapa na mabango ni yale yanayo husiana na Tume ya uchaguzi sio vyama vya siasa. Vyama vya siasa wao waligharamia kampeni na mabango kwa hela yao .

Is that so? UNDP wao waligharamia nini?
 
• Miradi ya maendeleo, ahadi za JK zakwama

na Betty Kangonga
SERIKALI inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha uliotokana na matumizi mabaya yasiyo na tija pamoja na misamaha holela ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa katika mkutano wa wahisani na watendaji wa serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, umebaini kuwa serikali ina upungufu wa sh bilioni 600 kutoka kwenye bajeti ya sh trilioni 11, iliyopitishwa na Bunge.

Kati ya sh trilioni 11, sh trilioni 6 zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.
Sababu kubwa ya kupungua kwa fedha hizo, imeelezwa kuwa ni kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika miezi miwili iliyopita.

Duru za kisiasa zinabainisha kuwa ukiachia kiasi cha sh bilioni 60 kilichotengwa na serikali kwa ajili ya kugharimia uchaguzi, serikali imetumia fedha zaidi ikiwemo uchapishaji wa mabango ya kampeni.
Matumizi mengine yanayotajwa kuathiri bajeti ya mwaka 2010/11 ni ya anasa kama vile mikutano na safari za nje na ndani ya nchi ambazo hazikuwa na tija kwa taifa na kushuka kwa makusanyo ya kodi kutokana na misamaha holela.

Mathalani katika kipindi cha Julai na Septemba makusanyo ya vyanzo vya mapato vya ndani na kutoka kwa wafadhili, yalikuwa sh trilioni 1.3 wakati matumizi ya serikali yalifikia sh trilioni 1.9, sawa na tofauti ya sh bilioni 600.
"Kwa hiyo ukiangalia hapa utabaini kuwa matumizi ya serikali kati ya Julai na Septemba, yalikuwa makubwa zaidi kuliko makusanyo ya kodi na fedha za wafadhili na hadi sasa hali bado ni mbaya kwani TRA inakusanya chini ya lengo," alisema kiongozi mmoja wa serikali kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi.

Upungufu huo wa fedha, umeibua hofu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo na ahadi nyingine za Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni kama zile za ujenzi wa barabara za juu, huenda zikakwama.
Habari zaidi zinasema kuwa fedha za wizara mbalimbali zilikuwa zikisubiri uteuzi wa mawaziri, zimepunguzwa ili kukabiliana na punguzo hilo la makusanyo ya mapato.
"Sisi tumetangaziwa kabisa kwamba sasa hakuna semina, safari za ndani na nje ni zile za lazima sana, vinginevyo hakuna," alisema mmoja wa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Hata hivyo, mambo mawili yanaweza kufanyika ili kuokoa hali hiyo, mosi ni kuwa na bajeti ndogo au kukopa kutoka benki.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, amewatoa hofu Watanzania akisema kwamba serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.
Alisema serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa.

Hii ni mara ya pili kwa TRA kushindwa kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi kama ilivyopangwa.
Katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/10, serikali ilitarajiwa kukusanya sh trilioni 5.096, lakini iliishia kukusanya sh trilioni 4.662.
 
Wakuu ,

Tofautisheni kampeni na hali halisi. Kampeni ni sawa na michezo ya sarakasi kwa bongo.

Ile miradi ya kugeuza mikoa kuwa califonia, Hong kong ilikuwa ni kuwafurahisha wenyeji wa mikoa hiyo tu. Sidhani kuwa kuna aliyeamini kuwa itatekelezwa. Ikiwa umeme tu ni mgao,sasa utakuwa na Califonia kwenye Giza?

Halafu kama wanasema hela hakuna maana yake wanatudanganya.Siku anahutubia Bunge Mkuu wa Nchi alisema sasa wanakusanya mahela mengi, something like 450 bilion kwa mwezi, ukilinganisha na makusanyo siku za nyuma ni kuwa sasa wanawakamuwa kichizi waTZ. Sasa kama wanasema hakuna hayo mahela, yawe yameyayukia wapi?

Ukweli ni kuwa waliofilisika ni waTZ sio serikali.Wenyewe ndio hao VX , mishahara minono, posho za kila aina. Viyoyozi maofisini. Makongomano, semina elekezi, warsha…ahh mlolongo mrefu.

Wanatutia kamba tu ili wazikamuwe vizuri. TZ haiwezi kufilisika ila wakuu ndio wanatufilisi sisi. Ukiniambia watanzania wa kawaida wamefilisika ,hapo nitakuelewa.
 
Majuzi waziri wa maliasili, ezekiel maige, alipiga marufuku safari za nje za watendaji wakuu wa wizara yake. Jk anaonesha mfano gani kwa watendaji wake? Nani atampiga jk stop ya kupiga misele?
 
Uwe unasoma na kuelewa, kampeni zinazo zungumzwa hapa na mabango ni yale yanayo husiana na Tume ya uchaguzi sio vyama vya siasa. Vyama vya siasa wao waligharamia kampeni na mabango kwa hela yao .

You must be silly person jocking. Dont you remember when Dr Slaa nailed Ikulu of funding Mabango ya CCM which were printed in Canada? From which code did that sum come from. This is no joke neither is a play, the Government is bankrupt now after having divided and spent all the revenue collected by TRA in the CCM's campaigns and only to find that amid UCHAKACHAJI, THE GAY BEING DECLARED A WINNER BY A SMALL MARGIN. The deviation was far from their expectations pamoja na wizi huo wote.
 
Back
Top Bottom