Serikali ya Samia Suluhu Hassan nayo yaanza rasmi kubambikizia watu kesi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,439
50,961
Mwanzo tulidhani rais huyu ni muungwana, mchukia uonevu, mstaarabu kumbe ni walewale. Ukiwa member kwenye timu ya wachawi na wewe ni mchawi tu.

Naona serikali yake imeanza kubambikizia watu kesi. Eti Mbowe gaidi, ugaidi mmeujua tu kwa kuwa kaanza kudai katiba mpya na haki ya vyama vya siasa kufanya siasa?

Kiufupi, hii serikali inajidhalilisha, inafanya mambo ya ajabuajabu mpaka inatia aibu.

Najiuliza kwa nini hii serikali imeanza kuwa reactionary, defensive isiyo jiamini?. Yaani wanashindwa kutenda haki kwa mujibu wa katiba wanaanza kutenda uonevu na dhulma za Wazi

Napenda nimkumbushe Samia, Mwenyezi Mungu aliyetuondolea Magufuli, angali yu hai, Kama na yeye ataendeleza dhulma sisi tutapiga Goti kwa BWANA WA MAJESHI. Tulipiga goti tuliponyanyaswa na Magufuli na tutapiga goti tena mbele yake ukiendeleza udhalimu.

Samia uliapa huku umeshika Qu'ran tukufu, na uliapa kutenda haki. Nakushauri tu acha uonevu, kwa sababu hicho kiapo chako ulicholula ni kizito, kina consequences ukikivunja kwa makusudi

Nimefilisha ujumbe kwako mheshimiwa rais, ukitaka fuata niliyokueleza ukitaka acha. Lakini ukizidi Dhulma tutapiga goti kumshitakia Muumba mbingu na nchi!
 
Nilisema hapa kuwa the so called Mama ni takataka watu wakafikiri kuwa nina husda,the worst is yet to come.CCM haina uwezo wa kutoa kiongozi mwenye akili.Period.

Akimalizana na upinzani anageukia huko CCM, the same kama bwana Chato.Tena huyu atakuwa lethal kuliko bwana Chato.Waliokuwa wanaiita takataka kuwa ni "Mama" shame on you all!

Having a vagina is no proof that one cannot be a tyrant.
 
Nilisema hapa kuwa the so called Mama ni takataka watu wakafikiri kuwa nina husda,the worst is yet to come.

Akimalizana na upinzani anageukia huko CCM, the same kama bwana Chato.Tena huyu atakuwa lethal kuliko bwana Chato.Waliokuwa wanaiita takataka kuwa ni "Mama" shame on you all!

Having a vagina is no proof that one cannot be a tyrant.
She is in panic mode, she can't think rationally anymore!
 
Alituzuga yeye ni msafi kwa kushika kitabu cha dini yake kitakatifu kwamba atailinda na kuitetea Katiba kumbe ndiyo wale wale!!! Ndiyo sababu anaihofia Katiba Mpya kwani haitampa nafasi ya kuidharau akithubutu kutoiheshimu kutakuwa na vipengele ambavyo vitambana na kupigwa faini kubwa, au kwenda jela au adhabu zote mbili kwa wakati mmoja.
 
Mkuu, huyu mwanamke anacheza na kitu kinachoitwa kiapo..
Anamchemzea Mwenyezi MUNGU..
Hajiulizi kwanini mwenzie baada ya kula kiapo alikaa miezi mi 3 tu..!!
MUNGU BABA tunaomba sasa uende ukatende na kutuondolea mtawala huyu dhalimu, anaetesa vyama vya upinzani, anabambikia wapinzani kesi za uongo, anaweka kodi na tozo za kuwadidimiza Wananchi na mabaya yote..
Nenda katende sasa Ee Mungu.
 
Tulikuwa tumezoea waislam kubambikiziwa kesi hizi za ugaidi lakini sasa hivi wameanza kuwabambikia wanasiasa
 
SAMIA unae mwambia ndo anajua kifo cha Magufuli kuliko wewe unae andika hapa.
Bora ukaendelea na mengine tu.
 
Wanadai Mbowe ni gaidi alipanga kuwaua viongozi wa serikali, hiyo kauli imetolewa na msemaji wa polisi akiwa Dodoma kupitia BBC Swahili.
 
Mkuu, huyu mwanamke anacheza na kitu kinachoitwa kiapo..
Anamchemzea Mwenyezi MUNGU..
Hajiulizi kwanini mwenzie baada ya kula kiapo alikaa miezi mi 3 tu..!!
MUNGU BABA tunaomba sasa uende ukatende na kutuondolea mtawala huyu dhalimu, anaetesa vyama vya upinzani, anabambikia wapinzani kesi za uongo, anaweka kodi na tozo za kuwadidimiza Wananchi na mabaya yote..
Nenda katende sasa Ee Mungu.
Acha ramli hizi. How do explain about JK or Mkapa aliyetesa wapinzani na wote wakamaliza muda wao. huyo Magufuli alipoapa na kumaliza first term, Mungu alikuwa hajamuona bado? Sikubaliani kabisa na udhalimu, lakini pia sikubaliani na haya mambo kuwa ukiapa kwa Bible/Quran ukawa dhalimu basi utakufa kabla ya kumaliza muda wako. Mambo ya kifo ni Mungu mwenyewe ndiye anapanga ufe lini.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom