Serikali ya Rwanda imepiga marufuku aina yoyote ya matangazo ya biashara ya dawa za asili

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
872
1,000
_105261188_gettyimages-578324698.jpg

Serikali ya Rwanda imetangaza kupiga marufuku aina yoyote ya matangazo ya biashara ya madawa ya kijadi au asili na kuamuru vyombo vya habari vya nchi hiyo kusitisha vipindi vya waganga wa kijadi kunadi umaarufu wao.

Biashara ya madawa ya kijadi imeshamiri Rwanda na wizara ya afya inasema waganga wengi wa jadi wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kupotosha wananchi.

Kulingana na tangazo la wizara ya afya ya Rwanda ni marufuku kutangaza biashara ya madawa kwa kutumia picha, mabango au pia kutumia vipaaza sauti barabarani kote nchini Rwanda.

Vyombo vya habari pia kama magazeti, mitandao ya kijamii , redio na televisheni vimekatazwa kupitisha vipindi na matangazo yoyote ya biashara kuhusu uganga wa kijadi.

Matangazo au vipindi kuhusu waganga na madawa ya kijadi siku hizi imekuwa biashara kubwa sana kwa karibu vituo vyote vya redio na televisheni za kibinafsi nchini Rwanda.

Waganga wa kijadi wenyewe wakipishana moja kwa moja kila mmoja akitangaza umaarufu wake kutibu magonjwa sugu wanayosema kwamba yamekosa tiba ya kizungu.

Wengine wanakwenda mbali na kutangaza kuwa wanatoa madawa ya Baraka na kutibu umaskini huku wengine wakisema wazi kuwa wachawi.

Tangazo hilo limezua hisia mbali mbali miongoni mwa waganga wa jadi.

Baadhi wamesikitishwa na uamuzi wa wizara ya afya wa kuwakataza kutangaza biashara yao kupitia vipindi vya redio:

''Sijafurahishwa na uamuzi huu kwa sababu ingekuwa vizuri wizara ya afya kwanza ikatuuliza ukweli wa yale tunayozungumzia, halikadhalika ubora na uhalali wa madawa tunayotumia.

Mimi nilikuwa nafanya matangazo mengi ya biashara yangu kupitia vyombo vya habari ili watu wafahamu umaarufu wangu wa kutibu magonjwa, ila ninachosema kama kuna mmoja wetu aliyefanya kosa la kusema kwamba anafanya miujiza, sote hatuwezi kuathirika kutokana na yeye.'' amesema mmoja.

''Kawaida mimi natibu wanawake wenye matatizo ya mimba na watu waliopewa sumu.nilirithi utaalamu huo kutoka kwa wazazi wangu na kamwe sikuwaona wakijipigia debe na kupitisha matangazo kwa redio kwamba wao ni waganga wa ajabu.Naunga mkono wizara kupiga marufuku matangazo ya biashara hii ;kwani ukiwa mtaalamu katika maswala Fulani achieni wale unaowasaidia wakutangaze wenyewe,yaani chema cha jiuza. Ameeleza mwingine.

Mashirika ya waganga wa jadi pia yameunga mkono uamuzi wa wizara ya afya yakisema yatasaidia kuweka utaratibu mzuri na imara wa utendaji kazi wa waganga wa jadi na kuwagundua wanaopotosha umma.

Chanzo: BBC
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom