Serikali ya Rais Samia yatenga tsh. Bil 83.4/- kuinua wachimbaji wadogo nchi zima

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko chini ya Rais Samia Suluhu imetangaza neema kubwa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima. Neema ambayo inakwenda kuwakomboa kabisa kimaisha. Hatua hii imekuja baada ya kuonekana kwamba wachimbaji wadogo na sekta nzima ya madini imekuwa na mchango mkubwa sana katika kuchangia pato la Taifa.

Maelekezo ya Rais Samia Suluhu ni kutaka kuona wachimbaji wadogo wanahitimu na kuwa wachimbaji wa kati na kisha wachimbaji wa kati wanahitimu na kuwa wachimbaji wakubwa.

Hilo litafanyika vipi?
  1. Kwanza wataweka katika maeneo yaliyopimwa vizuri na serikali na watapewa leseni za uchimbaji wa madini.
  2. Kisha Serikali itachukua hatua za kuwapa mafunzo na elimu juu ya shughuli wafanyayo ili kuweza kuzalisha kwa tija zaidi.
  3. Kupitia bajeti ya 2022/23 ya Wizara ya Madini, Serikali ya Rais Samia Suluhu imetenga kiasi cha shilingi Bil. 83.4/- kwa ajili kuinua wachimbaji hao nchi nzima.
Chini ya Rais Samia Suluhu sekta ya madini inachangia 7.3% kwenye pato la Taifa, tofuati na 2020 ambapo ilichangia 6.5%. Lengo la Serikali ya Rais Samia ni sekta ya madini kuchangia 10% kwenye pato la Taifa ifikapo 2025.

Katika mwaka huu wa fedha 2022/23 Serikali ya Rais Samia Suluhu inatarajia kukusanya kiasi cha Tsh 894bn/- kutoka kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, ambapo 2021/22 serikali ilikusanya Tsh Bil 696.4bn/-. Ongezeko la makusanya liliolengwa na serikali ya Rais Samia Suluhu ni 22.2%.
 
Naomba nitajie mishahara ya RAIS,MAKAMU,MAJIWA na Baraza lote halafu tuweke uhusiano wa wachimbaji wadogo na hiyo hela
 
Back
Top Bottom