zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,628
- 3,154
Kulalamika kwa kampuni fulani kwamba huduma zao zimeanza kuzorota sio excuse ya maana. Wao wenyewe VODA gharama zao za huduma zinalalamikiwa kuwa ni aghali kuliko mitandao mingine mbona wamekomaa na gharama zao zile zile? Jibu ni simpo, wamefanya analysis wakaona hiyo ndiyo business model yao itakayowaletea faida. Wasioweza kutumia voda wahamie mitandao mingine.VODA wameshalalamika biashara yao ya huduma za kifedha kushuka hasa maeneo ya vijijini, kuna hatari makampuni yakaanza kuhamisha mitaji na kuathiri maendeleo kwenye sekta nzima ya mawasiliano.....tutarudi enzi za kupanda juu ya miti ili uweze kupata network.
Kwa nini serikali ndiyo icompromise mambo yake? Labda kama hawana shabaha ya wanataka nini na watafikaje hapo, vinginevyo ni kazi ya serikali kujenga hoja na kuijenga kwa vitendo, kwamba kabla ya tozo hizi tulikuwa hatuwezi kufanya haya lakini baada ya hizi tozo tumefanya hivi.