barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,331
- 29,576
SafiKatika muendelezo uleule wa kudanganyadanganya wananchi serikali ya Samia imeanza kupiga chenga juu ya kupunguza tozo kubwa sana za miamala ya fedha.
Baada ya kelele kubwa na kukasirishwa kwa wananchi juu ya tozo kubwa za miamala ya fedha, serikali ya Samia ilijifanya kupoza kelele hizo kwa kuahidi kulifanyia kazi suala hilo. Lakini inaonekana hiyo ilikuwa ni tekniki ya kupoza hali huku wakiendelea kuwakamua wananchi pesa zao.
Hata Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa anasema tozo hizo haziwezi kuondolewa kwa sababu eti ziko kisheria.
Hoja hiyo ni hoja Muflisi kwa sababu hata Kikokotowo kilikuwepo kisheria lakini kiliahirishwa kutumika.
Tunaitaka serikali iitishe kikao cha dharura cha bunge ili bunge lipunguze hizo tozo mara moja.
Watanzania hatuwezi kuishi kwa kudanganywadanganywa
View attachment 1876301