Serikali ya Rais Samia Suluhu yaahidi kuimarisha uhusiano wake na Asasi za Kiraia (AZAKI)

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Ni siku 565 tangu Rais Samia Suluhu aingie madaraki, na Serikali yake imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uhusiano wake na asasi za kiraia nchini katika kutambua mchango wa asasi hizo katika ujenzi wa Taifa.

Kupitia Mwenyekiti wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Mwantumu Mahiza, amesema kwamba Tanzania Bara na hadi Visiwani, Marais wote wanaunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mashirika Binafsi.

Tangu Rais Samia Suluhu ameingia madarakani, Serikali imekuwa na mazingira rafiki kwa asasi za kiraia kufanya kazi. Uhuru wa asasi za kiraia umeongezeka na zimekuwa zikifanya kazi kwenye jamii kutoa huduma na elimu mbalimbali, jambo ambalo limepongezwa na Serikali.

Tangu sheria ya asasi za kiraia ianzishwe, asasi za kiraia zimekuwa mwenza mkubwa wa serikali yetu katika kuleta maendeleo nchi na pia kuwapatia vijana wetu ajira.

FVxMHdpXwAAm8l5 (1).jpg
 
Back
Top Bottom