Serikali ya Rais Samia Kupima na Kumilikisha ardhi

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetenga kiasi cha TZS bilioni 50/= kwaajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini. Pesa hizo zitakopeshwa kwa Halmashauri 55 nchini kutekeleza programu hiyo.

"Kuhusu masuala ya ardhi, namshukuru rais wetu Samia kwa kuipatia wizara shilingi bilioni 50 na kati ya kiasi hicho mkoa wetu wa Mwanza umepata shilingi bilioni 6.91, pesa ambazo zimesaidia sana upimaji viwanja katika halmashauri zetu ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela"- Dk Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi

Programu ya Upimaji na umilikishaji wa ardhi itasaidia jamii kuepuka migogoro ya ardhi, pamoja na hayo Serikali ya Rais Samia iko kazini migogoro ya ardhi inapatiwa ufumbuzi.
 
Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetenga kiasi cha TZS bilioni 50/= kwaajili ya programu ya kupanga...
Kuna wau walipimiwa tangu 2016 2017 wakalipia gharama zilizohitajika na kuahidiwa baada ya miezi mitatu au sita watapewa mrejesho hakuna kitu
 
Mh mbona hii ngumu Kumeza!? Hili swala nila aibu sana hasa kwa wajumbe wetu huku kwetu chamazi. Tupo badhi tumelipa pesa kwa awamu tatu (1)100,000 (2)700,00 (3)300,00

Ambapo awamu hizo zinajumuisha upimaji ardhi na upadikizaji wa mawe ktk mipaka baada ya hapo.
Linakuja swala la kupata hati milik ya ardhi ambacho ghrama yake ni 300,000.

Sasa hili swala kapewa mkandarasi ambae inaonekana ameelekea kuzingua kwan kuna baadhi kama mm nmelipa karbia gharama zote.
Sasa na hili bandiko napagawa sana ngoja nisubir mktano ujao wa mwisho wa mwezi. Kwani wanasema kuna kamat itakuja na majibu.
 
Lukuvi,Kabudi na Kitila waliambiwa wanautaka Urais ambao Mwigulu na January Makamba hawautaki,hivyo wakatemwa rasmi kwenye Baraza la Mawaziri!!
 
Iko siku moja isiyojulikana itakayoiaibisha Serikali hii na kupata aibu kama ile aliyoipata Boris Johnson wa UK. Ardhi wana bajeti kila mwaka, Rais anatenga tena mabilioni ili iweje wakati huo upimaji wa viwanja bado mwananchi unatakiwa kulipia?.

Enzi za Waziri Lukuvi, kuna zoezi la kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi, ambapo makampuni binafsi yalipewa jukumu la kuwapimia wananchi viwanja kwa gharama zao, viwanja vilipimwa na kuwekewa beacon kwa shilling kati ya 150, 000 na 250,000. Hakuna taarifa za hati hadi leo.

Makampuni yaliyofanya kazi hiyo ya kitapeli kutoka ngazi za juu yalikusanya pesa za wananchi na kutokomea kusikojulikana. Ofisi walizofungua Serilkali za mitaa, ziliishafungwa na watendaji wa kata waliotumika kama washenga wamekuwa mabubu, ukiwauliza wanasema suala hilo liko Wizarani!!!...... Sasa anaibuka Mabula na wimbo mpya wa kupanga upya kwa mabilioni?? ... Ufisadi wa kitaasisi huu.
 
Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetenga kiasi cha TZS bilioni 50/= kwaajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini. Pesa hizo zitakopeshwa kwa Halmashauri 55 nchini kutekeleza programu hiyo.

"Kuhusu masuala ya ardhi, namshukuru rais wetu Samia kwa kuipatia wizara shilingi bilioni 50 na kati ya kiasi hicho mkoa wetu wa Mwanza umepata shilingi bilioni 6.91, pesa ambazo zimesaidia sana upimaji viwanja katika halmashauri zetu ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela"- Dk Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi

Programu ya Upimaji na umilikishaji wa ardhi itasaidia jamii kuepuka migogoro ya ardhi, pamoja na hayo Serikali ya Rais Samia iko kazini migogoro ya ardhi inapatiwa ufumbuzi.
Moisemusajiografii
 
Kuna vifaa vya upimaji viwanja vilinunuliwa na serikali kwa pesa nyingi tu, Lukuvi kwa kinywa chake mwenyewe alitangaza kuwa kila Halmashauri ikachukue vifaa hivyo na kuanza rasmi kupima viwanja. Mabilioni yanayotolewa na Hangaya ni ya kupima?, kununua vifaa? au posho za watendaji? 🤔
 
Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imetenga kiasi cha TZS bilioni 50/= kwaajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini. Pesa hizo zitakopeshwa kwa Halmashauri 55 nchini kutekeleza programu hiyo.

"Kuhusu masuala ya ardhi, namshukuru rais wetu Samia kwa kuipatia wizara shilingi bilioni 50 na kati ya kiasi hicho mkoa wetu wa Mwanza umepata shilingi bilioni 6.91, pesa ambazo zimesaidia sana upimaji viwanja katika halmashauri zetu ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela"- Dk Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi

Programu ya Upimaji na umilikishaji wa ardhi itasaidia jamii kuepuka migogoro ya ardhi, pamoja na hayo Serikali ya Rais Samia iko kazini migogoro ya ardhi inapatiwa ufumbuzi.
Soma Tena
 
Hongera sana Serikali ya Awamu ya 6, Hili jambo tumelisubiri kwa muda mrefu sana. Huu ndo muarobaini wa makazi holela Tanzania.
 
Sahizi amekuwa mshenga kwenye harusi za wazee wenzanke!!.
Duh !! Nilisikia kwamba katika siasa haijalishi wewe uko smart kiakili kiasi gani au unajua kuongea kiasi gani hivyo vigezo haviwezi kukusaidia chochote!! Kinachotakiwa kwenye siasa ni kuwa na bahati tu ndio kitu muhimu !! Je ni kweli ??!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom