Serikali ya Rais Samia iachane na Uhandisi Jamii unoendelea kwani unamharibia taswira yake kwa kiwango kikubwa

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,876
20,284
Soko la Karume limechomwa lote na hakikusalia kitu hata kimoja na wamachinga wapo hoi bin taaban yaani "they are devastated big time".

Soko la Kariakoo nalo liliunguzwa na sasa lipo kwenye matengenezo.

Yapo masoko mengine ambayo yamechomwa moto yote na kutekeketea kama lile soko maarufu ya Mwanjelwa mjini Mbeya.

Suala ambalo huibuka ni kwamba moto huanza usiku wa manane na huenda hadi alfajiri ambapo moto huwa umekwishateketeza karibu asilimia 90 ya vibanda vyote na mali zilizomo humo.

Lakini nini lengo la wachoma moto au "the so called self proclaimed special Arsonists on the lose"?

Ukiangalia nia au "motive" kwa makini utagundua kuwa kuchoma moto maeneo ya wamachinga kutapelekea kurahisisha zoezi la ujenzi wa soko jipya na kisha kuwarudisha wamachinga na kuwatoza ada ya vizimba vitakavyojengwa humo ndani ya soko jipya.

Kabla ya kuchomwa moto eneo hilo la Karume wamachinga wamekuwepo hapo wakifanya biashara zao na hivyo serikali imeona fursa hiyo ya kuchukua eneo hilo na kuligeuza kuwa kitega uchumi kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa na "wahuni mbalimbali".

Ninawasema wachomaji hawa kuwa ni "wahuni" kwasababu hawajali maisha ya watanzania maskini na hawana njia sahihi au uwezo wa kubuni njia sahihi ya kutatua suala la wamachinga. Pia kwa kitendo hichi walokifanya hawa wahuni chaonyesha kiwango cha juu cha kutostaarabika kwa sisi watanzania ndani ya miaka 60 ya uhuru tulousheheka mweiz mmoja ulopita.

Isitoshe, kitendo hicho chaonyesha kiwango cha juu ya udhaifu katika kufikiri na kutoelimika kwa kila mmoja ambae ahusika na kadhia, dhuluma, dhahama na ubaradhuli huu.

Pia Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya husika wanaonyesha kuwa wanafahamu au hawafahamu kampeni hii mbaya sana inofanywa na hili kundi la wahuni ambao lengo lao ni kumilikishwa eneo hilo na kulitumia kujipatia faida lakini kwa kuwaumiza wananchi maskini.

Nasema hivyo kwasababu kauli yao ni kwamba "tutaunda tume" kuchunguza chanzo cha moto huo na baadae hakutakuwa na taarifa rasmi.

Moto huchunguzwa na watu wa zimamoto wachunguzi maalum "fire Investigators" (ambao hatuna au tunao lakini ni mafisadi) ambao wakifanya kazi yao kwa ueledi watatuambia chanzo cha moto hata kama kumebakia chembechembe na majivu.

Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya kote nchini wana wajibu wa kuwashugulikia wananchi wake khasa wale wenye maisha ya chini kwa kuthamini "utu" wao. Kwa kitendo hichi cha kunyamazia vitendo vya kihuni vya kuwachomea moto miundombinu, mali, vifaa na vitu vyao wamachinga hawa wakiwemo mama ntilie ni kinyume cha haki za binadamu na chakiuka mojawapo ya misingi mikuu ambayo yamo ndani ya katiba yao wenyewe ya CCM kwamba binadamu wote ni sawa.

Vitendo vya kihuni kwa sasa vyaonekana kuibuka na kushamiri vikiwemo vitendo vya watu kuvunjiwa nyumba zao na kuibiwa mali zao kama vifaa vya magari na vitendo vingine ambavyo vyafuzu kabisa kuitwa ni vitendo vya kigaidi, yaani kwamba nchi sasa imeshikwa na magaidi na wahuni ambao wanaleta hofu na vitisho ndani ya jamii yaani "the thugs they are terrorising the society".

Lakini kwa upande mwingine ni kwamba serikali bila kujitambua yafanya kitu chaitwa uhandisi jamii ambao siku za usoni utaja kuleta mpasuko mkubwa na kuishi kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Uhandisi jamii ni jaribio lilop[angwa kutokea kwa watawala la kutawala mabadiliko ya kijamii na kubadili au kusimamia mabadiliko hayo pamoja na tabia ya jamii hiyo.

Yaani kwa kiingereza yasema, " the use of centralised planning in attempt to manage social change and regulate the future development and behaviour of the society". Hivyo basi, serikali kwa kutumia au kuidhinisha au kuhalalisha matumizi ya nguvu (kwa kufahamu au kutofahamu) dhidi ya wananchi wa hali ya chini (working class) ili kuwabadilisha mawazo na kuwadhalilisha kifikra na kuwafanya kuwa wategemezi wao.

Tayari serikali imeweka tozo mbalimbali kwenye miamala ya simu, tozo katika malipo mbalimbali na pia kwa kupitia ongezeko la thamani bei ya bidhaa zimeruka maelfu ya maili kwenda angani (sky rocketing) na kusababisha ugumu wa maisha. Leo hii ukimchomea moto kibanda mjasiriliamali wategemea ataishi vipi?

Kama lengo ni kuuza maeneo hayo kwa wawekezaji kwanini taratibu zisifuatwe au kutafuta maeneo mengine rasmi ambayo yalingana na mvuto wa biashara kwa wamachinga hao?

Serikali iachane na uhandisi jamii, na ijikite katika kudhibiti mfumuko wa bei, na iangalie uhalali wa bei za bidhaa mbalimbali na uhaba wa vinywaji na wasababishwa na kitu gani.

Nchi yetu kwa sasa ipo katika kipindi cha mpito baada ya janga la Covid-19 kuelekea kupoa na maisha kuendelea na baadhi ya nchi ambazo huko nyuma zilikuwa zikiisakama Tanzania sasa hivi nazo zimepunguza siku za kujitenga (isolation) kuwa siku 5 tu. Hii yamaanisha kwamba ugonjwa huu wa Covid-19 kwa sasa utachukuliwa kuwa ni ugonjwa kama magonjwa mengine na wananchi wazingatie tu kutumia vitakasa maji na kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko.

Nahitimisha kwa kusema kwamba uhandisi jamii ni mbaya na hauleti matokeo chanya katika jamii kwani utaishia kuwa na kundi kubwa la watu ambao hawana ajira hata zile za ujasiriamali.

Serikali iachane na uhandisi jamii kwani waiharibia taswira yake "big time" na macho mengi ndani ya nje ya Tanzania yazidi kuangazia.
 
Kama walikuwa na lengo la kuwaondoa machinga kijanja naona lengo lao halitatimia, machinga wameshaweka alama ya maeneo yao wakisubiri hizo siku 7 za tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto.

Kwa kuwa majibu ya tune huwa hayatolewi, nawashauri machinga baada ya hizo siku saba wajiongeze kwa kuendelea na ujenzi wa vibanda vyao, wasiingizwe kwenye mtego wa kusubiri majibu ya tume ya kijanja iliyoundwa ili kuwazubaisha.
 
Jangwani baada ya kufanya upembuzi yakinifu imeshindikana kwahiyo mbadala wake ni karume tu
Kama Jangwani hapafaai kuwanyiwa "land reclamation" akapewa mwekezaji?

Maana hii nchi kuuza ardhi kwa miaka 99 si mbaya kama kuna uwekezaji wenye tija.

Huo utaleta ajira, mapato kwa nchi na unadhifu kimazingira.

Zipo sehemu kadhaa duniani ambapo wamefanya maeneo kama Jangwani kuwa sehemu za biashara na burudani.
 
Kama walikuwa na lengo la kuwaondoa machinga kijanja naona lengo lao halitatimia, machinga wameshaweka alama ya maeneo yao wakisubiri hizo siku 7 za tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto.

Kwa kuwa majibu ya tune huwa hayatolewi, nawashauri machinga baada ya hizo siku saba wajiongeze kwa kuendelea na ujenzi wa vibanda vyao, wasiingizwe kwenye mtego wa kusubiri majibu ya tume ya kijanja iliyoundwa ili kuwazubaisha.
Lengo ni hilo kuchoma tena usiku na estimate ya damage 3 am -Morning tayari ilifanywa, huu ni uhuni na haukubaliki katika nchi yetu.

Hii ni nchi yetu sote kwanini watu wachache ndo wawe na hakimiliki ya kuwaumiza wachache masikini kwa uroho wa mali?
 
Soko la Karume limechomwa lote na hakikusalia kitu hata kimoja na wamachinga wapo hoi bin taaban yaani "they are devastated big time".

Soko la Kariakoo nalo liliunguzwa na sasa lipo kwenye matengenezo...
"Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya kote nchini wana wajibu wa kuwashugulikia wananchi wake khasa wale wenye maisha ya chini kwa kuthamini "utu" wao"

Hii para (para ya 10) imesababisha mambo yote uliyoyaandika niyatoe maana.

Serikali ina wajibu wa kuwashughulikia watu wote bila ubaguzi Wa hali, mali, jinsia, dini, kabila au ukanda. Ni upuuzi na ujinga mkubwa kuishauri serikali kujinasibisha na watu Wa hali ya chini. Hii ni dhana ya kimasikini kwa kudhani kuwa, watu wenye unafuu au wenye maisha ya juu wamepata hizo hali kwa kuwadhulumu wengine.

Kuna watu ni masikini kwa kuwa ni wavivu, ingawa pia wapo watu wenye bidii ya kazi ila bado hawajabahatika. Na kuna matajiri, wamepata utajiri wao baada ya kusota kweli kweli na hawakuiba cha mtu na kinyume chake
 
"Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya kote nchini wana wajibu wa kuwashugulikia wananchi wake khasa wale wenye maisha ya chini kwa kuthamini "utu" wao"

Hii para (para ya 10) imesababisha mambo yote uliyoyaandika niyatoe maana...
Nimelenga kusema wananchi wake na nikasisitiza khasa wale wenye maisha ya chini.

Ukiwa wasoma kitu soma mstari kwa mstari.
 
Soko la Karume limechomwa lote na hakikusalia kitu hata kimoja na wamachinga wapo hoi bin taaban yaani "they are devastated big time".

Soko la Kariakoo nalo liliunguzwa na sasa lipo kwenye matengenezo...
CCM mbele kwa mbele.
 
Kama walikuwa na lengo la kuwaondoa machinga kijanja naona lengo lao halitatimia, machinga wameshaweka alama ya maeneo yao wakisubiri hizo siku 7 za tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto...
Kwani Ardhi ni ya serikali au ya Machinga?
 
Kwani Ardhi ni ya serikali au ya Machinga?
Ukienda short namna hii utawapa serikali sababu ya kuendeleza uhuni wao kwa machinga, hata kama mwenye mamlaka ya mwisho ya umiliki ardhi ni Rais, lazima sheria nyingine zifuatwe kuwaondoa eneo husika, sio kuwchomea moto maeneo yao usiku wa manane.

Wanaunda tume kuchunguza kila siku, majibu ya hizo tume yako wapi? huu uhuni sio wa kufumbia macho kisa mwenye dhamana ya ardhi ni Rais, kwa namna hii Rais anaweza kuitumikia hiyo dhamana yake vibaya kuwaumiza walalahoi kwa manufaa ya matajiri wachache halafu nyie mridhike tu, think.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom