Serikali ya Rais Samia haina ufanisi katika matumizi yake, mfano ni hiki anachotarajia kufanya makamu wake

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,205
13,709
Hivi karibuni tumeambiwa kuwa serikali imeunda jopo la wataalam waliopewa jukumu la kuandika VISION 2050. Katika vision hiyo mambo mengi yameanishwa na jinsi ya kufikia malengo hayo. Ukiangalia kwa makini malengo katika vision hiyo sio tofauti sana na malengo yaliyokuwa kwenye vision ya nchi za Asia mashariki ya mbili wakati wanatafuta Maendeleo ya nchi zao; mfano mzuri ni SINGAPORE.

Nchi hizi zinazojulikana kama ASIAN TIGERS hazijafanya siri mikakati waliotumia kufika hapo walipofikia katika maendeleo yao. Everything they didi is well documented, it is just a question reading their treatises and you will know what strategies were used to enable them to reach their level of development. Sasa Makamu wa Rais Mpango unataka kutumia mabillion ya toto zetu kuwapeleka wataalam uliowateua kuandika hiyo vision 2050 kwenda kutalii huko mashariki ya mbali , kwenda kujifunza mbinu za maendeleo yatakayoiwezesha hiyo vision kufanikiwa.

Mimi ningeshauri kuwa badala ya kutumia mabillioni ya tozo zetu kuwapeleka hawa watu kwenda kutalii, hawa wasomi wa Mpango wanunuliwe vitabu vilivyoandikwa juu ya miracles of development za Nchi hizi za mashariki ya mbali bila kukosekana kitabu kiitwacho" From third world to First; The Singapore Story by LEE KUAN YEW". Kama Mpango kweli anataka hawa watu waelewe mbinu walizotumia wenzetu, ahakikishe kila mmoja wao anasoma kitabu hiki na kuona kama strategies walizotumia kule Singapore viongozi wetu akiwemo yeye Mpango wana what it takes to implement them!

Hakuna faida kuwaumiza wananchi kwa tozo halafu mnatumia hizo tozo kwenda kuwapeleka watu wenu kutalii mkijua wazi nyie viongozi hamna utashi/ubavu wa kuchukua maamuzi magumu. Wenzenu Singapore walikuwa hawana mchezo na RUSHWA ; waziri aliyepatikana kuwa alihongwa safari ya mapumziko na tajiri mmoja alijikuta yuko jela baada ya kurudi toka hiyo likizo!!! Je nyinyi mnaweza kuchukua hatua kama hizo wakati mawaziri wenu kila leo wako DUBAI wakiongozana na wafanya biashara na wengine mpaka wanafanya birthday parties huko New York?

Mpango tafadahari acha mara moja kufuja kodi zetu watu wako wanaweza kujua haya ya mashariki ya mbali wakiwa hapa nyumbani na lap tops zao bila kwenda kutalii.
 
Wewe naona hujaijua vizuri nchi ya tanzania....hapo kama hujafahamu unatengenezwa mwanya wa kuipiga pesa...
 
Kuna wakati Huwa nawaza kwann hawa TISS wasitudukulie hata nchi hizo za Tiger speed economy Wana soma Nini ( syllabus) kwenye shule zao!?
Kwann kusiwena intelligence na namna hiyii!? Sisi tung'ang'ania kusoma out dated topics!!!
 
Back
Top Bottom