Serikali ya Rais Mkapa ndiyo iliyopitisha sheria inayoruhusu mchanga kusafirishwa nje ya nchi

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Nakumbuka sana jinsi ambavyo rais mstaafu ndugu Benjamin Mkapa alipojinasibu mwaka 2000 kuwa kuna maeneo hatapita kufanya kampeni kwani tayari ameshashinda. Hata yale maeneo machache ambayo Mkapa alienda kupiga kampeni, ilikuwa ni kwa ajili tu ya wagombea wa CCM kwenye ngazi ya ubunge ambao walikuwa na "kaupinzani kiduchu" hivyo walihitaji kanguvu kidogo ka rais ili wamalize mambo.

Katika mkoa wa Kilimanjaro jimbo langu pamoja na jimbo lingine ndiyo majimbo pekee aliyokanyaga Mkapa kumpigia kampeni mgombea wake wa ubunge ambaye hata hivyo hakushinda! Mkapa akarudi zake Dar kuendelea na kazi za kitaifa.

Hatimaye Mkapa akashinda kwa wastani wa asilimia 71 akiongeza asilimia kumi zaidi kulinganisha na uchaguzi uliopita kabla.

Lakini ni takribani miaka miwili tu tangia Mkapa alipojichimbia ikulu akisaini mikataba lukuki asubuhi, saa sita, jioni na usiku wa manane. Mikataba ambayo ilisifiwa sana na wana CCM na ikapewa jina la "mwarobaini wa umasikini" Mikataba hiyo ikasifiwa kila kona ya nchi na wana CCM huku wakimtaja Mkapa kama mkweli na muwazi kuwa amewaambia wana CCM hao kila kitu na mambo ni waaa.

Lakini miaka 20 baadaye anakuja rais mwingine wa chama kilekile akilaumu mambo yaleyale aliyofanya mtangulizi wake na bahati mbaya sana wana CCM wamebadili mkondo na wanasifia kuwa rais wetu amefanya jambo la msingi na kwamba CCM ndiyo inayojali maslahi ya wanyonge.

Akija tena kiongozi mwingine huko mbeleni labda akawa ni wa CCM na kufanya kinyume cha huyu mtangulizi wake (Magufuli) basi upo uwezekano mkubwa wa wana CCM kupiga tena vigelegele na mayowe.

Ni kweli kuwa rais Magufuli anahitaji kuipitia upya mikataba aliyosaini mtangulizi wake. Akae pamoja na wawekezaji waangalie win-win situation. Lakini kamwe wana CCM wasiwafanye wa Tanzania wote kuwa ni wajinga, mazezeta na watu tusio na akili. Haya yamefika hapa kwa matokeo ya wao kupiga vigelegele kwa kila jambo linalofanywa na mkuu wao! Hii ni ishara kuu ya uchizi na ulemavu wa akili walio nao hawa wana CCM!

Wanayofanya wana CCM kila kukicha ni uthibitisho kuwa akili zao zimechoka kiasi cha kutisha. Wanataka kuwavuta wengine nao wachoke akili kama wao. Kina Shaka na Polepole ambao sasa wanasema kuwa rais kafanya kubwa ni kina Shaka na Polepole haohao waliokuwepo enzi ya Mkapa ila wanatofautiana tu ukomavu wa sura, rangi ya sura na maumbile!

Hawa hawajawahi kubadilika na hawatawahi kufanya hivyo.

Nini kifanyike?
Cha kwanza ni sisi wenye akili kuvalia njuga swala hili la mikataba na kutoa mbinyo kwa serikali ya Magufuli ifanye nini. Tutailazimisha ili maslahi ya taifa yawe mbele na siyo mbinja za hawa wana CCM wajinga.

Pili ni lazima tubadili mifumo hii ya kijinga iliyotamalaki nchini. Kinga ya rais iondolewe, katiba iwe na nguvu ndani ya nchi kwa kila kitu, mifumo ya chama dola ife.

Tatu ni lazima tuchoshwe na CCM kwani imekuwa ni kama kinyonga anayebadili rangi kuendana na hali ya maficho. Hili dude ni lazima lizimwe! Lipotee ili nchi yetu izaliwe upya chini ya uwajibikaji imara.

Ni upuuzi mtu kama Polepole leo kutoka na kusema kuwa eti CCM inajifunza na watu wakapiga makofi! Polepole jana alitakiwa kupigwa mawe ili liwe funzo kwa matumizi ya midomo yetu.
 
Magu wanadai ni chaguo la kwa Mungu. Mkuu wa mkoa wa majichumvi wanamwita Mungu wa maji chumvi.

Kunauwezekano rais wa awamu ijayo kama atatoka ccm wanaweza kumuita Mungu wa watanzania.

Kwahiyo naomba tuwavumilie hawa wenzetu kwa ugonjwa huu mbaya wa kupenda hata kufikia kumkufuru Mwenyezi Mungu
 
Ukishateuliwa na Bwana mkubwa pm ataongea nini asikike. Kumbuka katiba nzuri mliikataa mkaja na yenu mmefikia wapi au ndo uoga
 
The truth is wabunge wa ccm waliweka siasa sana kwenye hili suala. wakidhan wanakomoa wapinzani, well side effect imekuja kuonekana leo.
Na vile wote chama kimoja cjui ni nani atamfunga paka kengele
 
mkuu G Sam, kwenye andiko kama hili, huwezi kuwaona mafisi na misukule ya huko Lumumba...

kimsingi nchi yetu inaangamia kwa sababu ya unafiki na uzandiki wa wanaccm...wamekuwa vinyonga kazi yao ni kubadili rangi ili kufit na awam iliyopo madarakani..


Mimi naamini mwarobaini wa haya ni kuiondoa ccm madarakan yote..na si kubadili mtu then tunajisifu kuwa sasa matatizo yetu yatakwisha....la hasha!
 
Back
Top Bottom