MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Kwa muda wote Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira hawakugundua kuwa vyombo vya usalama vinawachunguza na wako mbioni kukamatwa na kupelekwa mahakamani.
Vyombo vya usalama wa Taifa vilikuwa vinafuatilia nyendo zao kwa karibu wakati wao hawakufahamu pamoja na kuwa wana mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.
Harbinder Singh Sethi hakufahamu kuna makachero walikuwa wanamfuata nyuma mpaka Airport na alipotaka kupanda ndege ndipo wakamkamata.
Vyombo vya habari havikunusa habari ya Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira kukamatwa mpaka siku ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alipotangaza kuwa wako mbioni kuwafikisha mahakamani. Hiyo ilikuwa ni siku ya tatu wakiwa mahabusu baada ya kukamatwa. Walikatamatwa Jumamosi Juni 17 na kufikishwa mahakamani Jumatatu Juni 19.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL/PAP, Habinder Seth Sigh akiwa na mkewe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, alikamatwa wakiwa safarini kwenda Afrika Kusini ambako ndiko yaliko makazi yao.
Usiri wa sasa wa serikali ya Rais Magufuli unawafanya vigogo wenye kashfa mbali mbali kupatwa na wasiwasi kwa sababu hawafahamu kinachoendelea kuhusu hatima zao kisiasa na kibiashara.
Zama za siri za serikali kuvuja kwa urahisi zimeanza kutoweka na hii ni ishara nzuri kwa ustawi wa taifa hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo kiwango cha utajiri wako wa pesa au kisiasa ndio kinakuwezesha usiguswe na mkono wa dola.
Unapowaona wafanyabiashara wakubwa kama Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira wanapigishwa magoti kwa amri ya Warder/wardress wa Magereza lazima utajiuliza maswali magumu kuhusu hatima ya ufisadi nchini.
Mwingereza Leslie Bricusse ambaye ni mtunzi aliwahi kusema, “It's a new dawn, it's a new day, it's a new life, and I'm feeling good”.