VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mwanzoni mwa Serikali ya Awamu ya tano,chini ya Rais Magufuli,kulikuwa na matumaini makubwa. Matumaini ya kuona na kusikia mambo tofauti. Matumaini ya kuachana na mazoea yasiyopendeza.
Matumaini ya kupunguza walalamikaji na kuongeza wawajibikaji. Kuanzia kwa wafanyakazi,viongozi hadi wanafunzi,matumaini ya mabadiliko ya kweli yalijaa. Matumaini ya kuondolewa kero na karo na kusonga kama Taifa.
Sasa,mambo yanarudi nyuma. Yanarudi yale. Tunarudi kale. Kule. Wafanyakazi wa NIDA wanasaka haki zao za kuachishwa kazi. Wabunge wa upinzani wanaadhibiwa kwa hoja ya kitaifa. Wananyamazishwa. Wanafunzi wa vyuo wanagoma na wengine wanarejeshwa makwao bila makosa yao.
Hakika,tunarudi enzi zile zile. Kwa mwanzo mzuri na wa kuvutia ule,Serikali ya Rais Magufuli imefikaje hapa?
Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam