AbaMukulu
JF-Expert Member
- Jan 1, 2018
- 2,048
- 3,568
Bei ya sukari 2015 ilikuwa 1800-2200 kwa kilo. Baada ya tangazo la marufuku ya kuingiza sukari toka nje bei ilipaa na hadi sasa hivi iko kuanzia 2600-3000 kwa kilo.
Marufuku ile ililenga kulinda uzalishaji wa ndani wa sukari kitu ambacho ni nia njema kabisa.
Matokeo ya uamuzi hayajawa mazuri hadi leo. Hapa kuna swala kubwa la kujifunza kwa utawala wa Magufuli.
Rais inabidi abadilike namna anavyofanya maamuzi yake.
Bei ya sukari isingepanda kama kulikuwa na mipango madhubuti ya kutuvusha kipindi cha mpito ambacho tungekuwa tunajenga kiwanda kipya au tunaongeza uzalishaji wa vilivyopo huku tukiendelea kuagiza nje.
Baada ya kupita kipindi cha mpito na kuna uhakika wa uzalishaji ndipo serikali ingepiga marufuku uagizwaji wa sukari toka nje sababu tungekuwa tunajitosheleza uzalishaji wa ndani.
Tukirudi kwenye suala la mafuta ya kula naona maamuzi mabovu yaliyofanyika yanajirudia tena kwenye serikali ambayo ina zaidi ya miaka miwili na nusu madarakani.
Na Waswahili wanasema "Kosea njia wakati wa kwenda sio wakati wa kurudi"
Kabla ya kupiga marufuku mafuta ya nje ingebidi serikali ijiridhishe yafuatayo
1. Uhakika wa Viwanda vya uzalishaji
2. Malighafi za uzalishaji kwa viwanda hivyo
3. Upatikanaji wa Nishati ya uhakika
Mambo yote hayo hayako kwenye mazingira mazuri ili kukidhi uzalishaji wa ndani. Serikali iyafanyie kazi kwanza kwa matokeo chanya.
Naunga mkono uzalishaji wa viwanda vya ndani lakini maamuzi ya kufikia lengo hilo yanafanyika hovyo na kuleta matokeo hasi.
Uamuzi mbovu kwenye suala mafuta ya kula ndio unasababisha bei kupanda na kumuumiza mwananchi.
Kwa wale wachezaji wa draft wanajua kwamba kila kete utakayosogeza basi ina athari kwenye ushindi/kushindwa kwako.
ANGALIZO
EAC imepiga marufuku uagizwaji wa mitumba ifikapo 2019.
Mitumba kupigwa marufuku Afrika Mashariki
JUHUDI ZIANZE MAPEMA, TUKICHELEWA TUTAVALISHWA NGUO NA WANYARWANDA WAKATI TUNA PAMBA NA UWEZO WA KUTOSHA WA UZALISHAJI.