Serikali ya Rais John Magufuli yathibitisha umahiri wake katika kupambana na corona na kuwalinda wananchi wake

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Ugonjwa wa Corona umeanza December 2019 katika mji wa Wuhan nchini China.Mpaka hivi sasa ugonjwa huu umeshasambaa kwa watu takribani 819,025 na kusababisha vifo vya watu wapatao 39,794 duniani kote akiwemo raia mmoja wa Tanzania.

Kusambaa kwa ugonjwa huu duniani kumeleta taharuki kubwa kwa viongozi wa nchi mbalimbali duniani.Nchi nyingi zimechukua maamuzi ambayo wataalamu wamebaini madhara makubwa ya hatua zilizochukuliwa zaidi ya madhara halisi ya janga la corona katika nchi hizo.

Mfano zipo nchi zilizochukua maamuzi ya kuwazuia watu wake kutoka nyumbani na kufunga kabisa shughuli za uzalishaji,na zipo nchi zilizochukua maamuzi ya kufunga mipaka yake kutokuruhusu kuingia na kutoka kwa wananchi wake.Lakini cha kustaajabu nchi hizi zimeendelea kukabiliwa na maambukizi na kuongeza ukubwa wa tatizo kwa wananchi wake.Ukubwa wa tatizo hili katika baadhi ya nchi unaongezwa na msongo wa mawazo na kukata tamaa kwa wananchi,uchumi wa familia unaoambatana na ukosefu wa chakula kutokana na kutokuwepo maandalizi stahiki na mlipuko wa magonjwa mengine ya kijamii.

Anasema Professor Lina Lindhard wa International University of Professional Studies, namnukuu

”If what is happening in Europe is anything to go on, we really do not know how many confirmed cases there are for people who have it at home are not being tested. Also in France and I believe Germany, unless the person dies in a hospital from the corona virus, it is is not counted amongst the deaths. So people dying at home and old age homes are not included. As this moves to less developed countries the statistics will also become more confused.”

Ni wazi kuwa kuna maambukizi yanayoweza kuendelea kwa kufungia watu ndani,kujifungia ndani kwa watu ambao wamepima na kutokuwa na maambukizi yanaweza kusaidia,lakini kufungia watu ndani na ikatokea miongoni mwa mwanafamilia aliejifungia anamaambukizi anaweza kuwaambukiza wengine na kuendeleza maambukizi kwa haraka bila taarifa kuifikia serikali au mamlaka husika.

Wataalamu mbalimbali wa ugonjwa huu wanatoa maoni juu ya namna nzuri ya kukabiliana na janga la ugonjwa huu hatari wa corona.Mbinu ya kwanza ni kutoa elimu sahihi juu ya mbinu za kukabiliana na ugonjwa huu kwa ngazi ya mtu mmoja mmmoja,familia,kikundi na nchi kwa jumla.Mbinu ya pili ni kuhakikisha wananchi wanafuata kanunu za afya na tahadhari zingine ili kuepuka maambukizi mapya.Mbinu ya tatu ni kuthibiti maambukizi yaliyopo na kutokomeza kabisa ugonjwa.

Njia hizi hata kabla ya kutolewa na wataalamu ndizo zilizotumika Tanznaia na zinazoendela kutumika chini ya uongozi imara wa Raisi Dr. John Pombe Magufuli .Tofauti na nchi zingine njia hizi zimeweza kuleta matuamaini makubwa kwa Watanzania kwani idadi ya maambukizi mapya imekua kwa kiwango kidogo kulinganisha na nchi zingine.Maamuzi haya ya Raisi John Magufuli yamepunguza na kudhibiti madhara ambayo sio ya moja kwa moja yatokanayo na janga la ugonjwa wa corona,madhara hayo ni kama vile kufa na njaa kwa wananchi wanaotegemea kipato cha siku,msongo wa mawazo,kupoteza ajira,kuvunja uchumi wa mtu mmoja mmoja,familia na nchi kwa ujumla.

Kutokana na maamuzi haya ya serikali ya Raisi wetu Dr John Magufuli unadhirisha wazi kwa Watanzania na dunia kwa ujumla kuwa uzalendo,hofu ya Mungu na umakini katika maamuzi yenye mustakabali mwema na nchi unahitajika na sio kuiga wanachofanya viongozi wa nchi zingine ambao wana mazingira tofauti na ya kwetu.

Nisije nikawa mwizi wa fadhila,kwa kutokushare na ninyi sifa za kiongozi wetu Raisi Dr,John Magufuli katika mapambano haya:

1.Kiongozi bora ni yule anayetoa matumaini na kuweza kuthibitisha yale matumaini wakati wale anaowaongoza wakiwa wamekata tamaa.

Madhara yanayoweza kupatikana kwa hofu kubwa ya jambo yanaweza kuwa makubwa kuliko madhara yanayoweza patikana kutokana na lile janga.Mfano janga la kinu cha kuzalisha umeme cha Fukushima Daichi Japan.Professor Fred Peace anasema namnukuu.

“In Fukushima accident for many, the psychological damage is far more profound than the health effects”

Kwa maana kuwa madhara yaliypatikana kwa uoga,na hofu baada ya ajali yalikuwa makubwa kuliko madhara madogo yaliyotokea kutokana na ajali ya kinu cha nuklia.Hili linajidhihirisha kwenye janga la corona baada ya ugonjwa huu kuaza kusambaa na kuonekana madhara yake,na baadhi ya watanzania kupata maambukizi ilitokea taharuki ambayo kama sio busara na hekima za Raisi madhara ya taharuki hii yangekua makubwa kuliko athari za ugonjwa wenyewe.

Tunajua mazigira halisi ya wanachi wetu wengi,wanategemea kazi za kila siku kujipatia kipato,kuwafungia ndani kungewakosesha chakula,huduma za afya na huduma nyingine muhimu.Ndio maana Raisi akiwa Dodoma alisema maneno haya,nanukuu
“Watu tusitishane,tunatishana mno.Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa madhehebu yote,huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote,tuendelee kuchapa kazi,tuendelee kujenga uchumi wetu,hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu.”

2.Kiongozi bora ni yule anayeweza kuyasoma mazingira yake na kukabiliana na changamoto zinazomkabili kulingana na mazingira yaliyopo na ya baadae.
Siku zote uelewa sahihi juu ya madhara yanayopatikana kutokana na janga fulani unaweza kuondoa hofu inayoweza kusababisha madhara zaidi yanayoweza kupatikana ziada ya madhara ya lile janga.Mfano,watu wanauoga wa kupima afya zao kwa khofu ya kujua hali ya afya yake lakini wanasahau kuwa madhara ya kuchelewesha kutibu tatizo la kiafya ni makubwa kuliko kulifahamu mapema.

Jukumu kubwa la serikali chini ya uongozi wa Rais John Magufuli ulikua ni kuwaelimisha watu juu ya madhara ya ugonjwa huu na tahadhari stahiki.Jambo hili lilifanyika kwa umakini na kwa kutumia mbinu za kisayansi kufikisha ujumbe.

3.Kiongozi imara huweka njia sahihi na thabiti za mawasiliano na kupashana habari katika kipindi cha taharuki.

Tunafahamu kuwa,katika jamii yeyote hawakosekani wahalifu wenye nia mbaya ambao hutumia majanga au taharuki kufanikisha malengo yao.Wapo viongozi wa kisiasa walianza kutumia mlipuko huu wa ugonjwa kuleta madhara makubwa katika jamii,wapo ambao walipinga maamuzi ya Raisi na baada ya kupingwa na wananchi kuunga maamuzi sahihi ya Raisi.

Kitaalamu,wakati wa taharuki,ujumbe unaotoka katika malaka sahihi na inayoaminika kwa umma unasaidia kuongeza usalama wa nchi,kuweka tahadhari stahiki ya ugonjwa,kuongeza imani na matumaini ya wananchi na kuunganisha jamii kupambana na janga.

Raisi amelidhirisha hili ndani ya serikali yake na kiwango cha taharuki na tahadhari imechukuliwa kwa hali ya juu.

Ombi langu kwa Watanzania, tunaye kiongozi Mcha Mungu, Mzalendo na mwenye huruma kwa wanachi wake.Tuendelee kumuombea na kumsikiliza kwa kila analotuambia.
Mungu inusuru Tanzania na Watu wake, Mungu wanusuru walimwengu na ugonjwa huu wa corona.
 
Nakuunga mkono. Ni kweli ugonjwa ni wa hatari na viongozi wetu wanalifahamu hilo, lakini hofu na paniki ina hatari zaidi. Tunamshukuru Mungu rais wetu ni mcha Mungu.

Kwa nafasi yake kutambua nafasi ya Mungu kwenye kuleta uponyaji na ushindi dhidi ya corona virus hilo ni Baraka kubwa sana kwa Taifa! Mungu huguswa na kauli kama hizo kwa viongozi.
 
Sijamaliza kuisoma yote ila nakubaliana na wewe
Tena chapeni kazi tu iko siku watajua huku msimamo wenu huko
Big up maana kufungiwa ndani muisikie tu
Mtu unakaa ndani wiki tu na tumbo linafunga huendi choo maana movement ya kazi hakuna
Acha tu nianze kukimbia hali si hali


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ushindi ni mpaka dakika ya 90 au kipyenga cha mwisho na refa anaweka mpira kwapani. Naona tunashangilia ushindi mapema mno.

Ni wajibu wetu kumwomba Mungu awape hekima viongozi wetu wote.
 
Bora ya sisi Rais wetu kawa mkweli wengine wanaumbuka kwa fake news na tweet zao kuondolewa kabisa
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Katika mambo ya Msingi kama haya ambayo yanahitaji Umakini mkubwa kutokana na Janga lenyewe lilivyo duniani kwa sasa na linavyozidi Kupukutisha Watu kila Uchao ' Logically ' sidhani kama COVID-19 imekuja Kutupulizia Filimbi ya Kusifia ( Kupamba ) na Kuanza Kampeni kabla ya wakati hivi.

Nakubali kwamba chini ya Serikali yake wanapambana na Elimu inatolewa mara kwa mara kwa Watanzania ila bado Serikali yake ina Safari ndefu katika Kupambana na Kuutafutia Suluhisho ama la muda au la kudumu la huu Ugonjwa ambao sasa nao unaanza Kuzoeleka ndani ya Watanzania kwa idadi ya Walioupata na huyu Mmoja aliyetutangulia kutuwekea Makazi yetu mema huko Mavumbini na baadae Ahera kabisa.
 
Wamruhusu Daktari mkuu wa muhimbili awe anatoa taarifa zote za wagonjwa wa corona kwa uwazi pasipo kuingiliwa na waziri wa Afya hapo ndipo tutaujua ukweli wote
Kwanini wameajiliwa wasemaji wa taasisi uhusika?
 
Ni mapema sana kumwaga hii misifa na kutukuza,mpaka sasa hakuna anayeweza kujiita bingwa wa approach dhidi ya Corona katika taifa lake!Tuombe Mungu atunusuru na janga hilo!
 
Wamruhusu Daktari mkuu wa muhimbili awe anatoa taarifa zote za wagonjwa wa corona kwa uwazi pasipo kuingiliwa na waziri wa Afya hapo ndipo tutaujua ukweli wote
Kuna ndugu yako ana CORONA jina halijatajwa? Au www mwenyewe una Corona haujatangazwa mbona una roho mbaya sana weewee
 
Naunga mkono hoja kwenye mapambano dhidi ya Corona, Magufuli ni shujaa na Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano sio kwa jinsi inavyopambana na Corona bali kwa jinsi inavyomtegemea Mungu, na kiukweli kwenye hili janga la Corona kwa Tanzania,

Ni Mungu tu ametuwekea mkono wake tena ni kwa neema tuu na sio kwa matendo, maana just think of Italy yalipo makao makuu ya kanisa Katoliki, nchi nzima ni watu wa Mungu lakini wameteketea, sisi Tanzania tumefanya nini kustahili.
P
 
Halafu mwitikio Wa Taifa kwa kunawa mikono na kuitakasa kwa kutumua sanitizers ni mkubwa mno! Halafu Rsis akahimiza maombi!! Kwa nini nisimpende rais Magufuli;! Rais anayetambua nafasi ya Mungu kwenye Taifa ni zawadi kubwa sana.

..Burundi haina mgonjwa hata mmoja.

..Now, guess what?

..Raisi wao ni mlokole.

Cc Kiranga 😂
 
Au sio lakini Muda bado na corona bado lipo linawapoteza watu tayari mbongo mmoja kashaondoka kama likija kuripuka baadae naomba usije kukana kauli zako na kumkana mzee nijambo la muda omba sana lisiripuke mkuu
Kinacho jadiliwa ni mwanzo mzuri na juhudi ambazo matunda yake yanaonekana wazi.Je, hujui kuwa kuna nchi zimeshasababisha madhara makubwa kwa wananchi wake kwa maamuzi yasiyo sahihi?.Ndio maana nikasisitiza mwisho kuwa tuendelee kumwombea Raisi wetu Mungu azidi kumpa Afya na busara za kuendelea kuwapigania watanzania.
 
Back
Top Bottom