Wakubwa hii nimeipata BBC jioni hii, wazee wa Pemba wamewasilisha madai yao kwenye ofisi za UN zilizoko Dar na kwenye ubalozi wa Marekani, wakitaka waungwe mkono waweze kuwa na serikali ya Pemba, ili Zanzibar iweze kuwa na serikali mbili, yaani ya Unguja na ya Pemba. Wanataka shirikisho kama lile la Comoro ambako kila kisiwa kina serikali yake. Ingawa kimsingi wanachodai wazee hawa sio secession ama jamhuri yao ya kipekee, nadhani wapo watakaodai labda watataka baadae waelekee huko (kumbukeni kisa cha ngamia hemani, alianza kuingiza mguu wa mbele, lakini mwishowe alifanikiwa kuingia mzima!). Wengine najua watadai kuwa hii ndio njia ya pekee ya kuiwezesha CUF kuwa na serikali yao Zanzibar, kwani hakuna ubishi kuwa Pemba yote ni CUF. Na mmojawapo wa wawakilishi wa wazee hao aliyehojiwa ameweka wazi kuwa kisa cha wapemba kutengwa katika utawala na kisiwa cha Pemba kunyimwa fursa za maendeleo ambazo wenzao wa Unguja wanapata, kinatokana na wapemba kuunga mkono chama cha CUF.
Je kuna uwezekano wowote kwa Pemba kuwa na serikali yake? Athari na faida zake ni zipi? Je itamaliza "mpasuko" wa kisiasa ama itauzidisha? Karibuni wakuu.
Je kuna uwezekano wowote kwa Pemba kuwa na serikali yake? Athari na faida zake ni zipi? Je itamaliza "mpasuko" wa kisiasa ama itauzidisha? Karibuni wakuu.