"Serikali ya Pemba": suluhisho la "mpasuko"?

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
208
Wakubwa hii nimeipata BBC jioni hii, wazee wa Pemba wamewasilisha madai yao kwenye ofisi za UN zilizoko Dar na kwenye ubalozi wa Marekani, wakitaka waungwe mkono waweze kuwa na serikali ya Pemba, ili Zanzibar iweze kuwa na serikali mbili, yaani ya Unguja na ya Pemba. Wanataka shirikisho kama lile la Comoro ambako kila kisiwa kina serikali yake. Ingawa kimsingi wanachodai wazee hawa sio secession ama jamhuri yao ya kipekee, nadhani wapo watakaodai labda watataka baadae waelekee huko (kumbukeni kisa cha ngamia hemani, alianza kuingiza mguu wa mbele, lakini mwishowe alifanikiwa kuingia mzima!). Wengine najua watadai kuwa hii ndio njia ya pekee ya kuiwezesha CUF kuwa na serikali yao Zanzibar, kwani hakuna ubishi kuwa Pemba yote ni CUF. Na mmojawapo wa wawakilishi wa wazee hao aliyehojiwa ameweka wazi kuwa kisa cha wapemba kutengwa katika utawala na kisiwa cha Pemba kunyimwa fursa za maendeleo ambazo wenzao wa Unguja wanapata, kinatokana na wapemba kuunga mkono chama cha CUF.

Je kuna uwezekano wowote kwa Pemba kuwa na serikali yake? Athari na faida zake ni zipi? Je itamaliza "mpasuko" wa kisiasa ama itauzidisha? Karibuni wakuu.
 
Kithuku,
Haya yanayotokea sasa hivi siyo mambo mapya, japo yamekuwa hayazungumzwi bayana hadharani. Lakini kubwa hapa ni nini maalim Seif anachotaka? Maalim Seif anataka kuwa na himaya na ndiyo maana aliaanza matayarisho ya kuigawa Zanzibar akiwa na nyadhifa ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Amefanikiwa kuifanya Pemba au wapemba wajione kuwa siyo sehemu ya Zanzibar au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, zaidi ya 80% ya misimamo au maamuzi ya CUF yanatokana na utashi au ushawishi wa Maalim Seif.

Sasa je yapi ni madhara yake?

Hii ni dalili fika kabisa ya mawazo ya utawala wa ki-imla yaliyopo ndani fikra za maalim Seif, kwa maana hiyo Pemba ikijitenga:

wale wabantu wenzagu kama mimi in the long run watakuwa ni second citizen kamili kwa maana dhambi ya kujitenga haitaishia kwa Pemba na Unguja tu.

Kama Pemba yote majority ni CUF, then demokrasia ya kweli ndani ya kisiwa hicho itakuwa imefungasha virago na huenda ndiyo itakuwa imerudisha influence ya utawala ulikuwapo kabla ya Mapinduzi ya Mwaka 1964, ambapo inaelezwa kuwa waliopinduliwa bado wanahangaika kurudisha utawala wao.
 
Toa boriti ndani ya jicho lako kabla hujaelekeza kidole kwa mwenzio
 
Pemba si Tabora kwmba gari na treni zinazoelekea Mwanza na Kigoma zinapita hapo na hivyo utaweza kuuza chama choma ,asali na miwa kwa abiria ,Pemba ni kisiwa kidogo tu ambacho kimezungukwa na bahari ,hivyo kinahitaji kutazamwa kama mtoto mchanga na Serikali lakini Serikali ya CCM Zanzibar na vibaraka wao CCM Bara wanaweka chuki binafsi za kutokupeleka maendeleo na kufika hata kuishusha bei ya zao kuu la Karafuu ,wananchi wakidai waachwe wauze karafuu yao watakako pata bei nzuri ,serikali inawazamisha baharini eti wanauza karafuu kwa magendo ,(kumbuka serikali inapiga makelele kuwa karafuu haina bei),kubwa wanajaribu kujemge sijui barabara ,dispensary ,sasa utamjengea mtu barabara na hospitali wakati hana njia za kupata feza ya kula ,majisifu makubwa ni kusema tumejenga barabara kilometa moja ,yaani mwaka mzima unajisifu umepeka maendeleo ya kujenga barabara yenye urefu wa kilometa moja. Wazee wameshituka wanataka kieleweke.
Hongera wazee wa Pemba sasa tunawasubiri wazee wa Kigoma na wao waliwahi kuonya iwapo serikali haitapeleka maendeleo huko sio wataomba wawe na serikali ya shirikisho bali wao watadai nchi na utawala huru kabisa na hapo walipo ni pazuri maana kuna jamaa wa mipakani bado wananuka baruti.
 
Hao wazee wa pemba ni bora wakakaa na vijana wa Pemba kabla ya kukurupuka na maneno mazito kama hayo...!

Simply ni kuongeza mpasuko
 
Kithuku,
Haya yanayotokea sasa hivi siyo mambo mapya, japo yamekuwa hayazungumzwi bayana hadharani. Lakini kubwa hapa ni nini maalim Seif anachotaka? Maalim Seif anataka kuwa na himaya na ndiyo maana aliaanza matayarisho ya kuigawa Zanzibar akiwa na nyadhifa ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Amefanikiwa kuifanya Pemba au wapemba wajione kuwa siyo sehemu ya Zanzibar au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, zaidi ya 80% ya misimamo au maamuzi ya CUF yanatokana na utashi au ushawishi wa Maalim Seif.

Sasa je yapi ni madhara yake?

Hii ni dalili fika kabisa ya mawazo ya utawala wa ki-imla yaliyopo ndani fikra za maalim Seif, kwa maana hiyo Pemba ikijitenga:

wale wabantu wenzagu kama mimi in the long run watakuwa ni second citizen kamili kwa maana dhambi ya kujitenga haitaishia kwa Pemba na Unguja tu.

Kama Pemba yote majority ni CUF, then demokrasia ya kweli ndani ya kisiwa hicho itakuwa imefungasha virago na huenda ndiyo itakuwa imerudisha influence ya utawala ulikuwapo kabla ya Mapinduzi ya Mwaka 1964, ambapo inaelezwa kuwa waliopinduliwa bado wanahangaika kurudisha utawala wao.

Pemba walianza kutengwa na kunyanyaswa kabla hata Seif Shariff hajawa na ndoto zakuingia katika siasa - wanaojua watakueleza nini kilikuwa kinatokea wakati wa utawala wa Karume Sn.

Kuhusisha kila uamuzi unaochukuliwa na wananchi wa Pemba kuwa ni matakwa ya Seif Shariff ni kuwafanya Wapemba ni wajinga na wasioweza kufikiri na kupima jinsi ya kutatua matatizo yao.

Ama uamuzi waliochukua mimi nahisi utazidisha mpasuko na kufarakana visiwani lakini wafanye nii ikiwa kila juhudi wanazofanya zinagonga ukuta, wabaki wawasubiri CCM wawaamulie kuwa sasa tayari kufaidi matunda ya Mapinduzi? Naamini wakishindwa hili watatafuta njia nyengine na sijui itakuwa ipi lakini inaweza kuwa na athari zaidi ya hii.
 
Mrengo wa siasa wa upande wowote unategemea mobilization, ya mtu mmoja, anaeongoza.
Kama ni CUF au CCM, watu wa kawaida watafuata tu, ndio sababu wanakaa majukwaani kuhimiza sera zao, hata wangekuwa Seif hana tofauti na Kikwete, wote wanatamani ukubwa, ni kiasi cha kuchagua tu we mwananchi unataka uongozwe na nani.
Labda CCM imewachosha wanataka kujaribu vingine, au mpaka ufisadi uingie pemba ndio watapata akili kuwa ccm si mali?
mi naona maadam mataifa makubwa yanapenda vipande vya nchi vijitenge, na wanasaidia, basi wasaidie pia pemba ijitenge na makucha ya uonevu ya Tanzania.
 
Mkapa uzalendo umemshinda
Ashangaa kwa nini wapemba hawarudi kwao
Wananchi wasema CCM haiuheshimu tena Muungano
Na Mwandishi Wetu
KAULI ya Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Benjamin Mkapa kuwashangaa Wapemba ni kwa nini hawawekezi kwao Kisiwani Pemba, imeshutumiwa vikali na wananchi kwa madai kuwa Bw. Mkapa, kama Mtanzania mwenzao amekosa uzalendo.

Bw. Mkapa anadaiwa kutoa kauli hiyo katika mkutano wake wa kampeni alioufanya Micheweni, mkoa wa Kaskazini Pemba, Oktoba 19, mwaka huu.

Wananchi waliozungumza na gazeti hili katika nyakati tofauti kufuatia kauli hiyo ya mgombea urais wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake wamesema ni jambo la kusikitisha kuona Rais mwenyewe ameshindwa kufanya uchambuzi wa kina kuweza kujua tatizo halisi la kisiwa cha Pemba kuwa nyuma kimaendeleo.

Wamesema wapemba ni sehemu ya raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo wana haki kamili ya kuishi sehemu yoyote ile ya Jamhuri.

"Watanzania sote ni kitu kimoja ndio sababu Wahaya na Wamachinga wanafanya biashara zao hapa Dar es Salaam lakini hakuna anayewagusa; kadhalika, Wachaga wanaendesha biashara zao Mwanza, Tabora na kwingineko lakini hakuna anayestaajabia jambo hilo", alieleza mwananchi mmoja mkazi wa Sinza Madukani jijini ambaye hakutaka atajwe gazetini.

Akichambua sababu za kitaalamu zenye kumfanya mtu yeyote atake kuwekeza sehemu fulani , Mwalimu mmoja katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), pia cha jijini, amesema ni kuwepo kwa huduma za kiuchumi ambazo ni pamoja na njia bora za uchukuzi, mawasiliano, huduma za kibenki, maji na umeme.

"Lakini huduma hizi za kiuchumi katika nchi zetu hizi ni jukumu la serikali... barabara zote hizi hapa Dar es Salaam au Arusha au Moshi au mkoa mwingine wowote ule zimejengwa na serikali, vivyo hivyo vituo vya kuzalisha umeme na network zake (mitandao yake) ni kazi ya serikali", alisema mwalimu huyo na kuongeza kuwa mambo hayo ndiyo yenye kupelekea mji kukua na watu kukimbilia kuanzisha biashara mbalimbali.

Wananchi hao wamesema alichotakiwa kusema Bw. Mkapa ni kwa nini serikali ya CCM kwa miaka yote hii tangu muungano mwaka 1964 haikukiendeleza kisiwa hicho cha Pemba kiasi cha kuwavutia watnzania wakimbie kuwekeza kisiwani humo.

"Kama yeye Rais (Mkapa) aliona chama chake hakina sababu ya msingi za kushindwa kuanzisha huduma za kukuza uchumi huko kwa wapemba, angekiri tu kwamba walizembea na akaahidi kuwa jambo hilo litarekebishwa", alisema Bw. Valentine Muro wa Mwenge Dar es Salaam na kuongeza: "...lakini tabu ya rais wetu anataka kuhalalisha hata lisilo halali".

Aidha, wananchi hao wamesema hakuna mfanyabishara anayeweza kufungua biashara mahali ambapo wakazi hawana uwezo wa kununua bidhaa anazoiuza.

"...unapotaka kuanzisha biashara ni lazima ugalie purchasing power (uwezo wa watu kumudu kununua bidhaa), bila hivyo bidhaa zitadorora dukani ... matokeo yake ni mabaya na kama ulikopa mtaji ujue ndio umekwisha kwa sababu benki watakufilisi kwa kushindwa kulipa hela yao."

Kadhalika, wananchi hao waliuozungumza na gazeti hili pia wamehoji ni kwa nini serikali haijafanya juhudi za makusudi za kuinua kipato cha wakazi wa Pemba.

"Kwa kawaida serikali huwa inaiinua miji fulani ili kuwaletea hali bora wakazi wake; kwa mfano serikali iliamua kujenga kiwanda cha nguo cha Mutex katika mji wa Musoma ingawa kiuchumi kiwanda hicho hakikufaa kuwekwa huko kwa vile tayari kulikuwa na kiwanda kingine cha nguo cha Mwatex pale Mwanza... lakini ile ilikuwa ni njia ya kuwapiga jeki wakazi wa Musoma", alidai mwalimu huyo wa CBE.

Mwishoni mwa wiki vyombo vya habari viliripoti habari kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Bw. Mkapa amesema hali ya umasikini iliyopo kisiwani Pemba haikutokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na akaongeza kuwa wapemba walioko nje ya kisiwa hicho warudi kuja kuwekeza.

Likiripoti habari hizo gazeti moja la kila siku toleo la Oktoba 21, mwaka huu lilimnukuu mkapa akisema: "wafanyabiashara wapemba wamejaa toka Kinondoni hadi Kahama Shinyanga, wapinzani wangewashauri hao wote warudi kuweka vitega uchumi hap kisiwani".
 
...Kuhusisha kila uamuzi unaochukuliwa na wananchi wa Pemba kuwa ni matakwa ya Seif Shariff ni kuwafanya Wapemba ni wajinga na wasioweza kufikiri na kupima jinsi ya kutatua matatizo yao.
]

Mimi Pundamilia nasema kuwa huu ni mtazamo wako na wala si maneno yangu.
 
Ona wanaserikali wanavyosema! Nilijua tu!

Wapemba kutaka kuwa na utawala wao ni uhaini-Waziri

2008-05-10 11:29:18
Na Dunstan Bahai

Serikali imesisitiza kwamba hatua ya wananchi wa Pemba kutaka kisiwa hicho kiwe na utawala wake, ni uhaini na ni kosa la kijinai.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Omar Yussuf Mzee.

Alisema hatua hiyo ni kosa kubwa sana linaloweza kuchukuliwa dhidi ya wanaoendeleza harakati hizo.
Hata hivyo, aliviomba vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi hao kwani inawezekana hawajui wanachokifanya kuwa ni kosa.

Naibu Waziri huyo alisema visiwa hivyo vipo kihistoria na hakuna siku inayoonyesha kwamba viliungana, hivyo unavyovitenganisha ni kosa na kwamba vitaendelea kuwa chini ya Rais mmoja.

``Visiwa vya Unguja na Pemba, havijawahi kuungana, sote tulivikuta hivyo wote ni wamoja,`` alisisitiza Naibu Waziri .

Bw. Mzee alisema hawezi kuzungumzia kisheria zaidi lakini anachojua ni kosa la jinai kwa wanaoendeleza harakati hizo.

Juzi baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba zaidi ya Wapemba 10,000 wamepeleka maombi yao kwa Umoja wa Mataifa wakitaka kisiwa hicho kijitegemee kiutawala.

Aidha wananchi hao waliwakilishwa na wenzao 12 wakiongozwa na katibu wao, Bw. Hamad Ali Mussa, kuwasilisha barua ya maombi hayo kwenye ofisi za mwakilishi wa umoja huo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Bw. Muhammed Seif Khatibu, naye alinukuliwa akisema kitendo hicho ni cha kihaini.

SOURCE: Nipashe
 
...Kuhusisha kila uamuzi unaochukuliwa na wananchi wa Pemba kuwa ni matakwa ya Seif Shariff ni kuwafanya Wapemba ni wajinga na wasioweza kufikiri na kupima jinsi ya kutatua matatizo yao.
]

Mimi Pundamilia nasema kuwa huu ni mtazamo wako na wala si maneno yangu.

Pundamilia, mimi sikufanya citation ya maneno ulosema isipokuwa kama ukisoma maelezo yako huko ndiko ulikoelekea kwani petition ya kutaka serikal ya Pemba ilipelekwa na wananchi wa Pemba na wewe katika maelezo yako ulitaka tufahamu kuwa ni mbinu/hila/mikakati ya Seif Shariff kutaka madaraka sasa nikueleweje kama sikuwaona wapemba hawana uwezo wa kufikiri jinsi ya kutatua matatizo yao?

Wengine husema jicho lina mtoto na anayesema jicho lina mwana hueleweka vile vile na wewe ujumbe wako umeeleweka.
 
Nasikia hata Mafia na Ukerewe nao wanataka serikali zao!!

Bila shaka Ukerewe tutataka kuwa jimbo itakapo fika wakati...Ndio matatizo ya mfumo wa Majimbo..
Kwa hiyo tunapojaribu kuwatazama Pemba muhimu sana pia tuangalie kwa mapana mfumo mzima wa Majimbo..
Nategemea viongozi wa Chadema wataweza kuja na jibu zuri ktk swala hili kama ni solution ama ndio mwanzo wa kugawanyika.
Tanganyika > Tanzania <> Gawanyiika
 
Back
Top Bottom