Serikali ya nyerere si ya kuigwa ktk kupambana na ufisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya nyerere si ya kuigwa ktk kupambana na ufisadi!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by NasDaz, Oct 16, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  WAAFRIKA tuna desturi zetu! Ikiwa wewe ni kijana mdogo, umekaa na watu wazima halafu ikatokea mtu mzima mmoja amepiga ushuzi! Sasa, endapo mmoja wa watu hao atakushutumu ni kwamba umepiga ushuzi; basi hutakiwi kupinga! Hata kama unamfahamu ni babu gani kapiga ushuzi; unatakiwa kukubali kwamba ni wewe ndie uliyechafua hali ya hewa!!! Na kama hamna aliyekushutumu ni kwanini umepiga ushuzi; basi unatakiwa kuuchuna kana kwamba hakuna mtu aliyepiga ushuzi hata kama ushuzi huo unakaribia kukutoa damu puani kutokana na ukakasi wake!
  Kiafrika, mtu mzima hakosei!
  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere ni mtu mzima hapa nchini hivyo hata kama akipiga ushuzi Watanzania wote hatuna budi kuuchuna haidhuru hata kama pua zetu zinakaribia kunyofoka! Lakini pamoja na hayo, bado sihisi kigugumizi chochote kusema wazi kwamba mgombea yeyote(hususani wa Urais) atakayefuata nyayo za Baba wa taifa; basi kamwe hatamaliza tatizo la ufisadi nchini! Hayati Baba wa Taifa alichukia sana ufisadi lakini watendaji wake walikuwa mafisadi wa kutupwa!
  Mathalani, nasikia kijijini kwetu kulikuwa na duka kubwa la kijiji! Hata hivyo duka hilo lilikufa wakati hata Rais Mstaafu Ally H. Mwinyi hajafikiria kuwa Rais URT(United Republic of TZ)! Pamoja na duka hilo, kulikuwa na ng'ombe kadhaa wa kijiji pamoja na lori la kijiji! Hata hivyo, vyote hivyo vilikufa wakati wa utawala wa Hayati Baba wa Taifa! Aidha, kulikuwa na duka kubwa(mithili ya ghala) la RTC(Regional Trading Company)! Nalo lilikufia mbali wakati wa utawala wa Baba wa Taifa!
  Katika ngazi ya mkoa, kulikuwa na maduka(maghala) kadhaa ya RTC yaliyokuwa yametapakaa sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wetu. Aidha kulikuwa na kampuni ya uchukuzi iliyoitwa KAULI( Kampuni ya Uchukuzi/Usafirishaji Lindi)! Kampuni ilikuwa na mabasi na malori kadhaa! Vyote hivyo vimechinjiwa baharini wakati wa utawala wa Hayati Baba wa Taifa!
  Vitega uchumi nilivyovitaja hapo vilikuwa vimetapakaa nchi nzima lakini vyote hivyo vimefia mikononi mwa utawala wa Hayati Baba wa Taifa! Karibu nchi nzima kulikuwa na vyama vya ushirika ambavyo vilikuwa tajiri kwelikweli! Lakini vyote hivyo akina sisi hatukuvikuta mbali ya kusikia na kusoma! Sitaki kutaja viwanda na mashirika kadhaa ambayo Baba wa Taifa alianzisha lakini vilevile vikafia mikononi mwake!
  Ni nini basi tafsiri ya mambo yote hayo kama sio ufisadi uliokuwa unafanywa na viongozi pamoja watendaji wa serikali ya Hayati Baba wa Taifa?! Pamoja na ukweli kwamba Hayati Baba wa Taifa alikuwa adui mkubwa wa ufisadi, lakini bado watendaji wake walikuwa mafisadi wa kutupwa vinginevyo vitega uchumi ambavyo alivianzisha visingekufa wakati wa utawala wake mwenyewe.
  Hivyo basi, ikiwa kweli Dokta Slaa ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi ni lazima atuambie atapambana nao vipi! Inawezekana kabisa kwamba yeye mwenyewe (Dr. Slaa) akawa anauchukia ufisadi kama ilivyokuwa kwa Hayati Baba wa Taifa lakini kwavile watendaji watakuwa wengine basi ni lazima atuambie atawashughulikia vipi mafisadi badala ya kujigamba tu kwamba atakomesha ufisadi! Nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria(hata kama ni kwa nadharia na kuwa more practical pale itakapoonekana kuwa-favor watu fulani). Hivyo basi, ni dhahiri kwamba ktk utaratibu wa sasa, ni lazima PCCB/Polisi na mahakama waachwe wafanye kazi yao ili sheria ichukue mkondo wake! Je, Mheshimiwa Slaa ataachana na utaratibu huu wa kisheria? Je, Dk Slaa atakuwa anaamuru fulani akamatwe na kuwekwa ndani bila kufuata taratibu za kisheria pale muhusika anapotuhumiwa kuifisadi nchi yetu? Kama ndiyo, basi bila shaka huo hautakuwa utawala wa kisheria. Inauma sana, lakini ni sisi wenyewe tulioupigia upatu utawala wa kisheria ambao kama wasemavyo wapinzani wa masuala ya sheria kwamba haki na sheria na vitu viwili tofauti! Inawezekana kabisa mtu akawa amefanya kosa lakini tuhuma dhidi yake zikashindwa kuthibitishwa beyond reasonable doubt! Huu, ndio upuuzi wa sheria kwani mara nyingi wakosaji wanaachwa huru kwa kigezo cha kutopatikana na hatia kisheria!
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  wewe endelea kupigia debe mafisadi wa ccm lakini uelewe safari hii hatudanganyiki
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Jiteteee kukamatwa nako si kuzuli kabisaaa! unaweza kunyongwa kama wafanyavyo CHINA1 Fisadi mkubwa wewe!
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  nikiona kuna mdomo unafunguka na kutoa harufu chafu huwa sipati shida kufahamu ni domo la uelekeo upi!!!
   
Loading...