Serikali ya Msumbiji imesema viongozi wa Kundi la Kigaidi waliouawa nchini humo ni Watanzania

Mkuu, kweli kabisa hata mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara amesikika akilalamika ktk misafara yake wapo waandishi wa habari wanaonekana wakinakili habari kwa kalamu, peni na kurekodi kwa machine za kunasa sauti na video lakini mwenyekiti huyo wa chama dola anashangaa jioni au hata kesho yake habari za korosho au matishio ya kiusalama hazirushwi wala kuandikwa magazetini.

Hapo nakubaliana nawe kuna tatizo linalotufanya ku connect dots
Hii ni hatari sana
 
'Inaelezwa kuwa Njoroge ndiye aliyeanza mashambulizi Mocimboa da Praia tarehe 5 mwezi Oktoba mwaka 2017,'' Waziri alieleza akinukuliwa na shirika la habari la DW Afrika.

Naona Njoroge amewakilisha hapo mkuu.
Hivi tz tunao akina njoroge?
 
17 October 2020
Kitanya, Nanyamba
Mtwara
Tanzania

Hiki ndio kinachoendelea Mtwara kwa sasa, hali ni tete​

Maftaha Nachuma mbunge wa Mtwara aliyemaliza muda wake asimulia yaliyotokea kijijini Kitaya baada ya kijiji hicho kilichopo mpakani mwa Tanzania na nchi ya Mozambique
Hatari Sana hii
 
29 Juni 2019
Kitaya, Mtwara
Tanzania

2019 Kitaya waaswa kutokwenda Msumbiji

Wananchi wafunguka mauaji ya mwaka 2019 kijijini Kitaya
 
Ni maajabu sana kuona hiyo habari inatangazwa kwenye mitandao pamoja na vyombo vya habari vya nje, kama una akili timamu lazima u connect dots, kuna mambo mengi sana ambayo serikali imezuia vyombo vya habari kutangaza, na kwa mazoea tuliyo nayo watanzania ni kwamba jambo lisipokua covered na vyombo vyetu vya habari basi kuna katazo
Inawezekana unachosema ni kweli, maana hata hapa jf uzi uliokuwa unatoa updates umefungwa.
 
Taarifa za lini hizi mkuu?... Au ni redio mbao (habari ambazo hazijathibitishwa)?
Ingia hata YouTube andika kijiji cha kitaya utapata maelezo kiasi. Vyombo vya nje vinatangaza ila vyombo vya ndani vipo kimya
Habari ililetwa humu mod wakaifunga japo watu ambao tupo nao mtaani ndugu zao wametekwa na wengine kuuawa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom